Temeke: DC Jokate Mwegelo aagiza kuwekwa chini ya ulinzi, Viongozi wa Chuo cha Lubondo Training College

Viongozi wetu naona huwa wanapenda kukurupuka sana. Ukiona chuo, hospitali au shule binafsi inaendeshwa kimya kimya bila usajili ujue kwa asilimia mia kuwa mamlaka za udhibiti zinawakwamisha mahali fulani ili Serikali isipate halali yake bila watendaji kupata chochote.

Cha kufanya siyo kukifungia chuo,bali ni kukirasimisha kwanza na kukiwezesha kufanya kazi maana kina wanafunzi tayari... Kisha kuchunguza chanzo cha kufanya shughuli zake bila vibali, uhalali na stahili ya vyeti vya kitaaluma. Baada ya kujiridhisha chanzo cha mtafaruku ndio adhabu itolewe kwa anayestahili.
 
kwa hiyo kuwaweka ndani ndiyo wanafunzi watapata vyeti? issue ilikuwa kuwapa muda wahakikishe kila kitu kimekaa sawa
Walishapewa muda, kama unakumbuka mwaka 2016 TCU walifungia baadhi ya vyuo, vigezo vya kufungua vyuo ni muwe hata na PhD holder hata wawili kutegemea na ukubwa wa chuo.

Sasa leo hii kuna watu wanafungua vyuo unakuta mtu anayesoma bachelor anafungundishwa na bachelor mwenzake au mtu mwenye mastaers, wapi na wapi? Siyo sahihi, chuo kinafundisha hakina vifaa, ni lazima chuo kijipange maana kinaelimisha watu wa Taifa la kesho.
 
Walishapewa muda, kama unakumbuka mwaka 2016 TCU walifungia baadhi ya vyuo, vigezo vya kufungua vyuo ni muwe hata na PhD holder hata wawili kutegemea na ukubwa wa chuo, sasa leo hii kuna watu wanafungua vyuo unakuta mtu anayesoma bachelor anafungundishwa na bachelor mwenzake au mtu mwenye mastaers, wapi na wapi? Siyo sahihi, chuo kinafundisha hakina vifaa, ni lazima chuo kijipange maana kinaelimisha watu wa Taifa la kesho.
Hizo zipo chini ya NACTE na VETA
 
Kama watu wanakosea unataka wafanywe nini? Wale wanafunzi baada ya kumaliza Chuo ina maana vyeti vyao havitatambulika na hawatapata ajira. Hili likiachwa na Serikali ikakaa kimya ni sawa na kuwapotezea muda wale vijana ambao wamewekeza muda wao na pesa zao kwa kitu ambacho hakina faida. Wezi ni wengi sana, ache ni tu Mhe DC Jokate asimamie majukumu yake.
Kwani hakuna sheria? Bila shaka sheria zimeelekeza hatua za kuwachukulia. Haya mambo ya wakuu wa wilaya kuagiza watu wawekwe mahabusu ni ujinga. Tunakose sana tunapoangalia mambo kama haya kijuujuu bila kuchimba mizizi yake.

Mpaka chui kiendeshe mafunzo bila kufuata sheria ina maana kuna watendaji hawakufanya kazi yao ipasavyo. Zinapochukuliwa hatua basi zilenge kuondoa wote waliokosea kwa mujibu wa sheria na siyo kukurupuka kwa kuweka watu ndani.
 
Hawa wapenda kiki dawa ni kuwapa kitumbo tu bila kujali jinsia zao
Hawa mimi huwaita vinyamkera. Wapo kuongeza matumizi ya serikali tu na hawana msaada wowote kwenye maendeleo ya nchi. Matokeo yake wananchi ndiyo wanakamuliwa kwa kuongezewa tozo zisizo na maana yoyote.
 
Walishapewa muda, kama unakumbuka mwaka 2016 TCU walifungia baadhi ya vyuo, vigezo vya kufungua vyuo ni muwe hata na PhD holder hata wawili kutegemea na ukubwa wa chuo, sasa leo hii kuna watu wanafungua vyuo unakuta mtu anayesoma bachelor anafungundishwa na bachelor mwenzake au mtu mwenye mastaers, wapi na wapi? Siyo sahihi, chuo kinafundisha hakina vifaa, ni lazima chuo kijipange maana kinaelimisha watu wa Taifa la kesho.
PhD holder ana msaada gani kwenye ujasiliamali wa kitaaluma? Tatizo mmeweka mkazo kwenye vyeti kama kwamba ndivyo vinavyotoa elimu. Kuna PhDs lundo nchi hii hawana kabisa msaada zaidi ya kutumia vile vyeti kama kitegauchumi wakati wanapwaya kwenye nafasi walizopewa kusimamia.
 
Wenye chuo na walimu mkatunze familia zenu kwa jembe sasa.
Mjini hakufai kuishi bila kazi unaweza kwa kupumuliwa nyuma..!
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo @jokatemwegelo ameagiza kuwekwa chini ya ulinzi kwa Viongozi wa Chuo cha Lubando Training College kilichopo Mtaa wa Butiama, Kata ya Mtoni Kijichi baada ya kubaini Chuo hicho kinaendeshwa kinyume cha Sheria.

DC Jokate ametoa agizo hilo wakati alipoungana na Wataalamu katika ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo ambapo aliambatana pia na Mkurugenzi-Uthibiti, Ufuatiliaji na Tathmini kutoka NACTE Dkt. Joefrey Oleke.

Baada ya kufanya mahojiano na Mkuu wa Chuo hicho, DC Jokate alibaini kuwa kwa muda sasa Chuo hicho kimekua kikitoa mafunzo bila kupata usajili, pamoja na kutoa mafunzo kwenye mazingira yasiyo rasmi .

"Hamna kitu kibaya kama kufanya utapeli halafu ukadhani hutagundulika, Serikali ina macho kila sehemu, NACTE kaeni hapa na Polisi, lazima tupate 'information', Chuo hakijasajiliwa lakini hata mandhari yake haistahili, kuna Watu wanatoa huduma ambazo kiuhalisia hawastahili kutoa, tushirikiane katika ufuatiliaji, hawa wachukuliwe hatua kali huu ni utapeli"———-DC Jokate

Kwa upande wake Dkt. Jofrey Oleke amesitisha shughuli zote zinazoendelea katika chuo hicho, huku akielekeza taratibu nyingine za kisheria kufuatwa huku akisema kwa ukaguzi uliofanyika, chuo hicho hakitambuliki NACTE wala VETA.

IMG-20210901-WA0208.jpg

IMG-20210901-WA0210.jpg

IMG-20210901-WA0209.jpg

IMG-20210901-WA0207.jpg

IMG-20210901-WA0206.jpg

IMG-20210901-WA0205.jpg
 
Viongozi wetu naona huwa wanapenda kukurupuka sana. Ukiona chuo, hospitali au shule binafsi inaendeshwa kimya kimya bila usajili ujue kwa asilimia mia kuwa mamlaka za udhibiti zinawakwamisha mahali fulani ili Serikali isipate halali yake bila watendaji kupata chochote.
Cha kufanya siyo kukifungia chuo,bali ni kukirasimisha kwanza na kukiwezesha kufanya kazi maana kina wanafunzi tayari... Kisha kuchunguza chanzo cha kufanya shughuli zake bila vibali, uhalali na stahili ya vyeti vya kitaaluma. Baada ya kujiridhisha chanzo cha mtafaruku ndio adhabu itolewe kwa anayestahili.
Serikali ilishatoa muda kwa vyuo kama hivi kwenda kujisajili na kufuata taratibu zote ila wamiliki hawakufuata taratibu. Shida inakuja pale wamiliki hawataki kujulikana ili wasilipe kodi na kwa sababu wanajua uwezo wao kuwa kujiendesha ni mdogo ndiyo wanaamua kujifichaficha sana, mwisho wa siku elimu wanayotoa inakuwa haitambuliki na inakuwa ni hasara kwa wahitimu hasa wanapoambiwa vyeti vyao havitambuliki.
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. JOKATE MWEGELO Aagiza Kuwekwa Chini ya Ulinzi Mkali Viongozi wa Chuo cha LUBANDO TRAINING COLLEGE

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ameagiza kuwekwa chini ya ulinzi kwa Viongozi wa Chuo cha Lubando Training College kilichopo Mtaa wa Butiama, Kata ya Mtoni Kijichi baada ya kubaini Chuo hicho kinaendeshwa kinyume cha Sheria.

DC Jokate ametoa agizo hilo wakati alipoungana na Wataalamu katika ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo ambapo aliambatana pia na Mkurugenzi-Uthibiti, Ufuatiliaji na Tathmini kutoka NACTE Dkt. Joefrey Oleke.

Baada ya kufanya mahojiano na Mkuu wa Chuo hicho, DC Jokate alibaini kuwa kwa muda sasa Chuo hicho kimekua kikitoa mafunzo bila kupata usajili, pamoja na kutoa mafunzo kwenye mazingira yasiyo rasmi .

"Hamna kitu kibaya kama kufanya utapeli halafu ukadhani hutagundulika, Serikali ina macho kila sehemu, NACTE kaeni hapa na Polisi, lazima tupate 'information', Chuo hakijasajiliwa lakini hata mandhari yake haistahili, kuna Watu wanatoa huduma ambazo kiuhalisia hawastahili kutoa, tushirikiane katika ufuatiliaji, hawa wachukuliwe hatua kali huu ni utapeli"———-DC Jokate

Kwa upande wake Dkt. Jofrey Oleke amesitisha shughuli zote zinazoendelea katika chuo hicho, huku akielekeza taratibu nyingine za kisheria kufuatwa huku akisema kwa ukaguzi uliofanyika, chuo hicho hakitambuliki NACTE wala VETA.​

View attachment 1919666

Wanawekwa ndani kisha wanachukuliwa dhamana...faili linapelekwa kwa mwanasheria mkuu in a one kana mashtaka hayakidhi kupelekwa mahakamani kesi inamalizwa juu kwa ju...uhasama mpya unazaliwa

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Viongozi wetu naona huwa wanapenda kukurupuka sana. Ukiona chuo, hospitali au shule binafsi inaendeshwa kimya kimya bila usajili ujue kwa asilimia mia kuwa mamlaka za udhibiti zinawakwamisha mahali fulani ili Serikali isipate halali yake bila watendaji kupata chochote.
Cha kufanya siyo kukifungia chuo,bali ni kukirasimisha kwanza na kukiwezesha kufanya kazi maana kina wanafunzi tayari... Kisha kuchunguza chanzo cha kufanya shughuli zake bila vibali, uhalali na stahili ya vyeti vya kitaaluma. Baada ya kujiridhisha chanzo cha mtafaruku ndio adhabu itolewe kwa anayestahili.
Hayo yote unayoyasema yalishafanywa na kutolewa maelekezo, sema wabongo ni wagumu kutii sheria na kufuata utaratibu uliowekwa na Mamlaka zao. Serikali kwa upande wake ilishajitahidi kuweka utaratibu wa kumiliki taasisi za Elimu binafsi. DC JOKATE amefanya kwa mujibu wa Sheria.
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. JOKATE MWEGELO Aagiza Kuwekwa Chini ya Ulinzi Mkali Viongozi wa Chuo cha LUBANDO TRAINING COLLEGE

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ameagiza kuwekwa chini ya ulinzi kwa Viongozi wa Chuo cha Lubando Training College kilichopo Mtaa wa Butiama, Kata ya Mtoni Kijichi baada ya kubaini Chuo hicho kinaendeshwa kinyume cha Sheria.

DC Jokate ametoa agizo hilo wakati alipoungana na Wataalamu katika ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo ambapo aliambatana pia na Mkurugenzi-Uthibiti, Ufuatiliaji na Tathmini kutoka NACTE Dkt. Joefrey Oleke.

Baada ya kufanya mahojiano na Mkuu wa Chuo hicho, DC Jokate alibaini kuwa kwa muda sasa Chuo hicho kimekua kikitoa mafunzo bila kupata usajili, pamoja na kutoa mafunzo kwenye mazingira yasiyo rasmi .

"Hamna kitu kibaya kama kufanya utapeli halafu ukadhani hutagundulika, Serikali ina macho kila sehemu, NACTE kaeni hapa na Polisi, lazima tupate 'information', Chuo hakijasajiliwa lakini hata mandhari yake haistahili, kuna Watu wanatoa huduma ambazo kiuhalisia hawastahili kutoa, tushirikiane katika ufuatiliaji, hawa wachukuliwe hatua kali huu ni utapeli"———-DC Jokate

Kwa upande wake Dkt. Jofrey Oleke amesitisha shughuli zote zinazoendelea katika chuo hicho, huku akielekeza taratibu nyingine za kisheria kufuatwa huku akisema kwa ukaguzi uliofanyika, chuo hicho hakitambuliki NACTE wala VETA.​

View attachment 1919666

Mh.Jokate yuko sahihi....

Hao ndio wanaharibu ELIMU YETU.....
 
Huyu dada kachemka vibaya!!!
mambo ya kuwekana ndani ni ushamba.....
unachotakiwa kufanya kama kiongozi.....
unawasaidia waweze Ku iprove/kukizi vigezo chini ya uangalizi maalumu.....
unawapa muda maalum wakishindwa kujiongeza unawaondoa kwenye drawing board......
mpaka watakapokidhi vigezo
 
Back
Top Bottom