Rahma Salum
Member
- Sep 7, 2020
- 30
- 59
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imetoa tamko kuwa, kuanzia tarehe 1/5/2021 Televisheni na Redio hazitaruhusiwa kucheza wala kuonesha kazi yoyote kwenye vituo vyao bila kazi hiyo kuhakikiwa na BASATA (Muziki wa kusikika na kuona/audio na video) na TFB (Filamu), na kusajiliwa COSOTA kwa ajili ya ulinzi wa hakimiliki.
Tamko hilo limeambatana na maelekezo kwa mashirika ya utangazaji (Vituo vya Televisheni na Redio) Tanzania Bara, Wasanii, Waandaaji wa kazi za muziki na filamu na yeyote anayehusika. Juu ya vifungu vya sheria namba 23 ya Mwaka 1984 ya Baraza la Sanaa la Taifa na marekebisho yake ya Mwaka 2019 na kanuni zake za Mwaka 2018.
Vifungu hivyo vinamuelekeza mtu, chama, shirikisho, asasi, chombo cha habari au mtandao wa jamii unaohitaji kusambaza (kuonesha) kazi za filamu au mchezo wa kuigiza utapaswa kujiridhisha kuwa filamu au mchezo husika umepewa ithibati ya uhakiki kutoka Bodi ya filamu na atapaswa kuusambaza kwa kuzingatia alama ya daraja la filamu au mchezo husika.
Aidha, COSOTA imewasisitiza Wasanii, waandaaji na Wamiliki wa kazi za muziki na filamu kuhakiki na kusajili kazi kwa ajili ya manufaa na ulinzi wa kazi zao.