Vyama vya wasanii na uelewa mfinyu wa wasanii juu ya haki zao

Feb 6, 2024
40
50
VYAMA VYA WASANII NA UELEWA MFINYU WA WASANII JUU YA HAKI ZAO.
_______________________

Katika kitendawili kinachoendelea katika tasnia ya muziki na filamu ni swala la vyama vya wasanii,
Pamoja utambuzi ama uelewa Mdogo wa Haki zao kama wasanii.

Kuna aina nyingi ya vyama, vya kitaaluma kama vile Chama cha wapiga bezi au cha wapiga trumpet, vyama vya aina za muziki, kwa mfano muziki wa dansi, taarab, hiphop na kadhalika kisha vyama vya haki mbalimbali katika hakimiliki.

Na vyote hivi huanzishwa KWA lengo la kusimamia Haki na miongozo / sheria ambazo zitawalinda wao pale litakapokuja swala mikataba nk.

Bila kusahau pia kwenye upande wa filamu pia wana vyama vyao pia . Kwenye filamu sitaki kuingia deep sana Mimi najikita zaidi na wasanii wa Bongo fleva.

Kuna vyama vya haki za wanamuziki kama wafanya kazi na kadhalika. Kumekuwa na mkanganyiko wa vyama kuanzishwa na kuwa vinafanya kazi nyingi kwa pamoja hivyo hatimae kujikuta vikishindwa kazi.

Mfano KWA sasa kuna chama cha wasanii kinaitwa " Tuma"

Tatizo jingine ni uelewa mfinyu wa wasanii kuhusu haki zao na hivyo kutokuona umuhimu wa kujiunga na chama chochote Mfano kama vile kwenye "Baraza la SANAA la TAIFA ( BASATA) au kudhani vyama ni vingi mno kwa mtu mmoja. Wafanyabiashara wasiowaaminifu wamekuwa wakiwakataza wanamuziki kujiunga kwa kuwa wanajua umoja ni nguvu ya vyama hivyo.


Wasanii wakishindwa kutambua ama kufahamu Haki zao nadhani
Tunarudi hadi Enzi za mdosi ( mhindi) alivyokuwa akiwanyonya wasanii HAKI zao.

Ebu wasanii jitambueni
Kuna vyama vyingi vimeanzishwa kwaajili ya kusimamia Haki zenu.

Maana tumeona wasanii ambao wametangulia mbele zake na familia zao zimeshindwa kunufaika na kazi zilizofanywa na wapendwa wao Enzi za Uhai wao Na kubaki tu Historia


Nadhani wasanii wakijiunga kwenye vyama MBALIMBALI vinavyosimamia Haki zao nadhani itasaidia sana kupunguza wimbi la wasanii ambao wanadhulumiwa Haki zao angali wakiwa bado hai lakini pia hata pale wanapotangulia mbele za Haki .

Kinanisitikisha sanaa mtu kukumbukwa na kupewa Heshima pale anapokuwa ametangulia mbele za Haki angali uwezo wa kumsaidia mtu angali alipokuwa Hai uwezo mlikuwa nao na kingine zaidi hao hao ndio walikuwa wananyonyaji wakuu wa kazi za msanii huyo huyo Enzi za Uhai wake.

KWA leo naishia hapa.

Ni mtazamo wangu tu ..

#funguka
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    46.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom