em tuanzie mbali kidogo nini maana ya internet, internet = interconnected network , yaani mtandao ndani ya mtandao, lengo ni kurahisisha mawasiliano
kama vile mtandao wa barabara kurahisiha usafiri(mawasailiano) kati ya bukoba mpaka dsm
kuna ile triki unatumia vikombe viwili , na kamba ( nyuzi za kiroba) alaf mnakua mnaongea watu wawili
pale tayari na mtandao wa watu-2, ukiongeza kamba na kikombe ukamvutia mtu wa 3 tayari pale ni mtandao wa watu-3
chukualia 'internet' tuliyonayo ni mtandao wa watu bilioni 7 ivi

lengo ni mawasiliano ( kutuma na kupokea taarifa )
so ni lazima uwe na barabara ( route) ambayo ni moja ya miundombinu, kusafirisha taarifa point moja adi nyingine
chukulia mfumo wa dawasco bomba zile zinazotoka Ruvu kuja DSM zinakua ni kubwa (thick) mno, ila kila zikisambaa zaidi kwa 'watuamiaji' zinapungua ukubwa wake ( diameter )
ndicho icho kilicho kwenye mfumo wa 'internet'
kwa level ya juu kabisa (mwanzo) , level-1, tuna:
a. Tier 1 network ambayo ni haya hapa
en.wikipedia.org
hawa wamejiunganisha wenyewe ( peering) kwa kutumia mabomba makubwa (route ) na hakuna anaelipa kwa mwenzake
so kila mmoja kwenye iyo level-1 network, ina 'tap' bomba na kumuuzia anaefuata kwa level ya chini yake, level-2
so walio kwenye level-2 wananunua 'IP transit' kutoka kwa level-1, sawa na wewe uunganishiwe umeme kutoka kwenye nguzo au uunganishiwe bomba la maji kutoka bomba la mchina
hawa level-2 wanaitwa Tier 2 network ambao ni hawa hapa
en.wikipedia.org
ukicheki vizuri hapo utaona hawa Tier 2 wananunua 'transit' kutoka kwa Tier 1 ( hawanunui Bandwidth aka MBs)
b. Distribution bado inaendelea, hawa level-2 wanawaungia bomba (route) ambao wanaitwa mid-sized ISPs
na kuwauzia 'IP transit', yaani unalipia gharama za kuungiwa bomba (sio bandwidth) na gharama za kuwa katika 'mtandao'
kumbuka members wote waTier 2 mabomba yao yote yameungwa pamoja (peering) ( kama ilivyo kwa Tier 1) na hawachajiani.
lengo la 'peering' ni kuongeza 'connectivity enhancement'
kabla sijaenda mbali bomba hapa namaanisha 'barabara za kimawasiliano' ambayo ni kwa njia ya waya (fiber) au no- waya (satelliite)
Baadhi ya mid-sized ISPs ni Etisalat ( Zantel inachukua transit uko) Vodafone ( kama Tier / Tier 2 pia, Vodacom Tz inachukulia transit uko ) , nk
halafu tunakuja kwa Tier 3 network, izi ndo zile ndogo kabisa akina Zantel, Tigo, Airtel, ambao huungia 'transit' na makampuni mama yao
mf: Airtel Tz inaungwa na Bharti ya India, anachokifanya Airtel Tz ni kuwa na 'Internet Gateways' kujiunga kama bomba linalotoka India ( again kwa njia ya waya(fiber) au wireless(Satellite)
Baadhi ya ISPs hapa Tz wanatumia gateways (on lease) za ISPs wengine ( mf: Tigo kwa Zantel )
chain bado inaendelea, hawa Tier 3 network wanachofanya ni kujenga BTS (minara), BSC ( visimamizi vya minara), MSC ( mfumo wa taarifa ipi iende wapi na kwa nani ), links( fiber kupitishia data) , nk kwenda kwa wateja wa mwisho (end users)
then inauza Bandwidth kwa akina sisi (end users ) , Bandwidths ni MBs