SoC01 Teknolojia ndio sulushisho la mambo yote yanayotukabili hapa nchini Tanzania kuanzia ajira, afya, elimu nk.

Stories of Change - 2021 Competition
Jan 15, 2018
79
65
Suluhisho la kudumu kuhusu changamoto nyingi zinazotukumba hapa nchini zinaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwekeza kwenye teknolojia.

Leo nitazungumzia teknolojia kwenye nyanja tofauti tofauti kama vile kwenye ajira, afya,kuleta nidhamu kazini,vyuoni,kuongeza mapato serikalini ,kupunguza rushwa,kuongeza usalama nk.

1)Billing System.
Billing System ni system ya ulipaji bili kwa njia ya kieletroniki.
Ili serikali iweze kupata taarifa sahihi za mapato na matumizi ya huduma mbalimbali wanazozitoa basi inabidi wahame kutoka mfumo wa analojia na watumie mfumo wa kielectroniki.

Mfano kwenye huduma za utoaji maji .
Billing System inasaidia kujua idadi sahihi ya watu wanaotumia maji ,inasaidia kujua idadi ya watu waliolipa bili na ambao hawajalipa,Pia inachukua muda mfupi kuhudumua idadi kubwa ya watu kwa muda mfupi .
Kwa namna hii ni rahisi kuboresha mapato.

2)Malipo mengine ya kieletroniki kama vile kwenye michezo haswa mpirà wa miguu.
Mpira wa miguu ndio mchezo wenye mashabiki wengi sana.Mara kwa Mara tumekuwa tukisikia hasara wanayoipata serikali kupitia viingilio, sasa suluhiso ni ukataji wa tiketi kwa njia ya kidigitali.
Tiketi zikikatwa kwa njia ya kidigitali ni rahisi sana kwa serikali kuboresha mapato pia ni rahisi kudhibiti mianya ya upigaji.

3)Pipeline Detection System.
Mfumo huu ni muhimu haswa kwa sehemu za vijijini na uzuri tayari kuna miradi ya usambazaji maji vijijini RURAL WATER SUPPLY AND SANITATION SYTEM (RUWASA) hii itasaidia kujua mkondo wa maji ulipopita na ni rahisi kukagua vituo (Domestic Water Points)vinavyotoa maji na vituo ambavyo maji hayatoki bila kupata shida ya kuzunguka zunguka kupata taarifa kutoka kwa wanakijiji.
Pia kupitia mfumo huu ni rahisi kujua sehemu ambazo maji yanavuja (mabomba yamepasuka) hivyo ni rahisi kwenda kurekebisha haraka bila kupoteza maji mengi zaidi na kupoteza muda.


Mbali na matumizi ya kiteknolojia kwenye kuboresha mapato,serikali inaweza ikaboresha huduma za kiafya kwa njia zifuatazo.

1)Electronic Medical Records System.
Huu ni mfumo wa kutunza taarifa za mgonjwa kwa njia za kielectroniki ,miongoni mwa taarifa hizo ni umri,jinsia,health history ,allergies, immunization status,lab test results, hospital discharge instructions &billing informations
Kupitia mfumo huu ,inamrahisishia kazi daktari kumfanyia matibabu mgonjwa wake kwa usahihi zaidi maana atakuwa na taarifa muhimu kuhusu historia ya mgonjwa wake .

Mfumo huu ni rahisi kupata taarifa zote za mgonjwa ndani ya muda mfupi kuliko mfumo wa kujaza taarifa za mgonjwa kwenye madaftari maana mpaka faili la mgonjwa lipatikane itachukua muda mrefu na muda mwingine linaweza lisionekane.

2)Telehealth Teknolojia.
Huu ni mfumo ambao unaweza kuwaunganisha daktari anayeishi mkoa X kumtibu mgonjwa anayekaa mkoa Y pasipo na mgonjwa kupata tabu ya kupanda gari kumfuata daktari alipo.
Hata kama daktari anaishi nje ya nchi,kupitia mfumo huu ni rahisi kumuhudumia mgonjwa wake anayeishi hapa nchini.
Kwa njia hii itapunguza SOCIAL DISTANCING .

3)Serikali itoe elimu kwa wananchi kuhusu vifaa vya kielectroniki vinavyoweza kutoa taarifa muhimu juu ya afya za wananchi na nini cha kufanya ili kuboresha afya.
Mfano vifaa vya kupima joto la mwili kama limepanda au la ,vifaa vya kupima uzito wa mwili , kwa wananchi wanaofanya mazoezi wajue vifaa ambavyo vitawasaidia kujua umbali waliokimbia na kiwango cha mafuta walichochoma.

Kupitia elimu hii itasaidia SOCIAL DISTANCING mahospitalini.

Mbali na hilo, serikali inaweza ikapunguza vifo vinavyotokea barabarani kupitia teknolojia kama ifuatavyo.

1)Askari wa barabarani wapatiwe elimu kuhusu matumizi ya Alcohol Detection Device ili kumtambua dereva anayeendesha gari hali ya kuwa amelewa ,hii itasaidia kupunguza pia ajari barabarani.

Mbali na hayo teknolojia inaweza ikatumika kuongeza uaminifu na nidhamu vyuoni haswa kwenye vyumba vya mitiani.

1)Matumizi ya CCTV Cameras vyuoni.
Ili tuzalishe wataalimu halisi wasiotokana na janja janja nyingi basi suala la kufunga CCTV Cameras vyuoni haliepukiki.
Cctv cameras itasaidia sana kudhibiti wanafunzi wasio waaminifu kwenye vyumba vya mitihani hivyo kila mmoja atapata kile anachokistahili na sio kutumia mgongo wa mwenzake kuweza kufaulu kwa namna hii wanafunzi watasoma haswa pia itawazuia wanafunzi kutofanya mambo ya ajabu kwenye mazingira ya vyuoni.

2)Matumizi ya CCTV Cameras maofisini.
Hii itasaidia kupunguza uwizi, udanganyifu,rushwa makazini , dharau makazini.
Kwa namna moja au nyingine hii itasaidia kuongeza uwajibikaji na ufanisi makazini .

3)Matumizi ya CCTV Cameras Sokoni MF Kariakoo ,barabarani nk.

Kwa siku za karibuni soko la kariakoo limekuwa likiwaka moto mara kwa mara na haijulikani chanzo haswa ni nini, ila kama kungekuwa na kamera ingekuwa rahisi zaidi kufuatilia kwa ukaribu zaidi.

Pia camera zisambazwe barabarani baada ya umbali fulani camera zifungwe hii itaimarisha usalama na pia itapunguzwa suala la polisi kuomba omba rushwa hivyo kwa kuhofia kuonekana.


Mbali na hayo teknolojia ikitumika vizuri inaweza ikawa chanzo kizuri cha mapato kwa wananchi.
MF

1)Mapping Technology.
Vijana wanaweza wakajiajiri kupitia mapping teknology .Si kila sehemu hapa nchini ukiitafuta kwenye ramani ya google utaipata .Sasa kama kuna sehemu mpya imezinduliwa na umefanya utafiti na ukagundua haipo ramani ya google cha kufanya utaichora vizuri hiyo sehemu kisha utawasiliana na google waingize kwenye ramani kisha utalipwa kupitia kazi hiyo.

2)Serikali ilifanye somo la kompyuta kuwa ni la lazima kwa wanafunzi wote kuanzia ngazi ya kidato cha kwanza mpaka vyuo vikuu.

Hii itasaidia kuzalisha wataalamu wengi ambao wana ujuzi wa kompyuta hivyo itakiwa rahisi kwenye sehemu zao za kazi kutoa huduma kwa njia za ki electronic kwa uweledi mkubwa sana.

Mbali na hayo.Serikali pia ijikite kuandaa jeshi la kisomi linalotumia njia za kidigitali kujilinda na kulinda wananchi.

Badala ya kuona kila mwaka makamanda wetu wakivunja matofali kwa vichwa sasa tunataka kuona mbinu za kidigitali watakazotumia kujilinda dhidi ya maadui zetu.
 
Back
Top Bottom