SoC03 TEHAMA imepewa kisogo na Wizara ya Afya. Je, ndoto ya huduma bora kwa kila Mtanzania itafanikiwa?

Stories of Change - 2023 Competition

MulegiJr

Senior Member
Sep 5, 2018
125
88
Wakati Rwanda inajikita katika kuboresha Matumizi ya Tehama kila eneo ambalo limekuwa na changamoto ya Tehama, usambazaji wa Dawa( kwa ndege isiyo na Rubani, Usambazaji wa Damu maeneo yasiyofikika kirahisi, usambazaji wa Chanjo katika maeneo ambayo hayafikiki kirahisi) mwana afrika mashariki mwenzetu, Tanzania inapiga hatua 10 nyuma na kuipa kisogo Tehama kwenye mazingira ambayo tunahitaji Tehama katika kuratua changamoto nyingi katika kufikisha Huduma bora kwa kila mtanzania, kipindi ambacho tunapambana kupeleka mswada wa BIMA KWA WOTE na kwa lengo kuu la kila mtanzania kuweza kupata usawa na matibabu stahiki kulingana na Kifurushi cha Bima yake, tunahitaji kutokomeza vifo vya mama na mtoto nchini tunahitaji kufikisha huduma kila kona ya nchi yetu, tunahitaji kupeleka Damu kila kona ya nchi, tunahitaji kupeleka vifaa tiba kila kona ya Tanzania, usafirishaji wa Dharura kwa mama wajawazito na watoto wachanga kufikishwa Rufaa katika Maandalizi ya haraka na uhakika.

LENGO
Kuikumbusha Serikali juu ya Jitihadi zake ambazo ilikuwa imeamua kuzichukua kuhakikisha Tehama inatawala na inachukua nafasi kubwa katika kuboresha upatikanaji wa Huduma sawa kwa watu wote maeneo yote nchini.

CHANGAMOTO KUENDESHA IDARA YA AFYA BILA TEHAMA
  1. Usambazaji wa vifaa tiba na Dawa ni eneo kubwa ambalo linaonyesha kusudi la serikali kufikia lengo la Huduma Bora kwa kila mtanzania, eneo ambalo limebaki katika njia zile zile miaka yote tangu uhuru hadi leo. Kuna halmashauri nchi hii zina magari yasiyozidi Matano magari haya yatumike na Idara zote ikiwemo ya Afya, idara hii yenye Ambulance Mbili, ambazo kuna muda zinaacha majukumu yake ya msingi na kufanya kazi ya kusambaza na kumsafirisha DMO kutokana na uhaba wa magari Ambulance inatumika kusafirisha wagonjwa na hiyo hiyo inatumika kusambaza Vifaa tiba na Dawa, kwenye halmashauri yenye Kata 25 na Vijiji zaidi ya 90, na vituo visivyopungua 50, yenye Jiografia tata ambapo kutoka kituo kimoja kwenda kingine unatumia Masaa mawili.
  2. Rufaa kushindwa kuandaliwa mazingira stahiki kabla ya kufika kutokana na kutokuwa na matumizi ya AUTOMATED Digital application kutoka kituo A-B ni moja ya sababu inayoipa serikali kutokutimiza lengo lake la kupeleka Huduma Bora ya Afya kwa watanzania, mfumo wa M-mama lengo kuu la kuokoa maisha ya mama na mtoto lakini aina ya Tehama inayotumika inahitaji miaka mingi kufikia hilo lengo la Tamisemi.
  3. Gharama kubwa kuendesha shughuli za kila siku za Vituo vyetu vya kutolea Huduma, Mfano ni lazima Idara iwe na Mafuta kila mwezi kwa ajili ya kusambaza Chanjo, Dawa , vitendanishi na kufanya usimamizi shirikishi kwa team ya afya Wilaya, kila mwisho wa mwezi lazima wasimamizi wa vituo wasafiri kwenda halmashauri/ Hospitali za wilaya kupeleka taarifa ya kila mwezi ya mwenendo wa Magonjwa (MTUHA) hii pia inaiingiza serikali kwenye gharama kubwa.
  4. Usimamizi na uthibiti wa Mapato, Eneo hili limetelekezwa kitu kinachopelekea kupoteza uhalali wa makusanyo ya kile kinachoingia kituo cha kutolea Huduma, kwa sasa ni (nini?)921 tu, vilivyo na Mfumo wa uthibiti taarifa za Vituo vya kutolea Afya (GOTHOMIS). Siyo rahisi mtu aliyepo IYUMBU awe na Fedha wiki nzima ambazo hazipo katika mfumo na asitumie Fedha mbichi, ni rahisi sana kuingia majaribuni anapokuwa na hiyo fedha ( ukizingatia hamna waasibu) katika vituo vyetu.
NINI KIFANYIKE (SOLUTION)
1. Mwekezaji tafutwe eneo la Ufungaji Wa Mifumo Ya GOTHOMIS katika Vituo vyote vya Kutolea Huduma
.
Kupata mwekezaji makini atakae saidia ufungaji wa miundombinu ya tehama katika vituo vyote nchini kama ambavvyo tunatafuta wadau katika maeneo mengine. Hii itaondoa upotevu wa Mapato, nakufanikisha kuongeza mapata yatakayofanya vituo viweze kujiendesha mijini na vijijini, tehama itaongeza uwajibikaji wa watoa huduma hususani mfumo wa GOTHOMIS ambao unatakiwa ufungwe hadi kwenye zahanati, ufungwaji wa mfumo huo utaleta Tija stahiki katika ukusanyaji wa Fedha na kupunguza upotevu na matumizi ya fedha mbichi kwenye vituo.

Na kama yupo basi mwekezaji/mdau huyu kuna namna anatakiwa kuongezewa nguvu maana kazi yake haionekani vijijini wala mijini. Picha na maelezo hapo chini ni mwaka 2018, hadi leo hakuna matokea ya mdau huyu.

NUKUU 2018: Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto na Taasisi isiyo ya kiserikali ya PATH chini ya Mpango wa kuboresha Matumizi ya Takwimu za Afya (Data Use Partinership -DUP) imejiwekea mikakati ya kuongeza ufanisi katika utoaji huduma ya Afya kwa kuiweka Mifumo ya TEHAMA katika ngazi ya huduma ya Afya ya Msingi ili Wananchi waweze kupata huduma bora za afya.

TEHAMA kuongeza ufanisi kwa mtumishi wa afya ngazi ya zahanati

1686857979314.jpeg

Imewekwa Tar 12th September, 2018
2. Wizara ikaribishe Ubunifu eneo la Taarifa (Wazawa wapewe nafasi ya kuonyesha uzalendo kwa nchi yao)

Ubunifu uanzie katika matumizi ya kutunza na kutuma taarifa za wagonjwa na magonjwa na shughuri nyigine zinazoendelea katika kituo husika, ujenzi, kampain mbali mbali na kumbukumbu zake kwa gharama nafuu.

Mnakumbuka mtumishi bora wa Mbeya ambae ni Mtaalumu wa Tehama? Watu kama hawa wanapewa zawadi tu na kuishia kupata zawadi lakini hawapewi nafasi ya kufanya kazi na kuendeleza ubunifu wao.
Tehama italeta Tija katika kupunguza gharama za kupeleka taarifa kila mwisho wa mwezi, pia itatoa fursa kwa vituo vinavyotoa huduma kuwa na utulivu wa kufanya kazi, na kupunguza gharama za uendeshaji wa kituo, kupunguza kusafiri kila mwisho wa mwezi au ndani ya mwezi wakati kituo kikiwa na uhaba wa watumishi.

Wabunifu waelekezwe kutegeneza mifumo itakayoishia Wilayani/mikoani kabla ya kwenda na ngazi za maamuzi (Mfumo utafanya pre-audit kabla ya kufika Wizarani) ni Imani yangu kubwa kuwa mifumo yao local italeta tija kusaidia mifumo ya wizara ambayo ni ngumu kufika vijijini na ikafanya vizuri.

3. Ndege bila Rubani, eneo la usambazaji wa vifaa tiba na dawa vijijini
Matumizi ya Ndege zisizo na Rubani, Rwanda kwa sasa inasambaza vifaa tiba na Dawa kutumia ndege zisizo na rubani, wakati tunaazimisha uchangiaji Damu kwa Watanzania kwa ajili ya kuokoa maisha ya wahitaji kama mama wajawazito na wahanga wa ajali, kuna sehemu ya nchi hii ni ngumu kuona tone la hiyo damu iliyokusanywa kwa sababu ya miundombinu ya utunzaji wa hiyo damu katika mazingira haya, serikali ikiamua kuwekeza kwenye tehama ni rahisi damu kufika kwa kutumia ndege za dharula hata katika maeneo ambayo ni ngumu kufika (HARD TO REACH AREA).

4. Mfumo wa rufaa ubadilike
Matumizi ya rufaa ya karatasi tuachane nayo twende kidijitali kuna faida nyingi kuliko mfumo huu tulionao leo ni dhaifu sana kuhamia katika Tehama itaongeza ufanisi, kupunguza vifo vya mama na mtoto, ajali na magonjwa mengine yanayohitaji uangalizi mkubwa ( intensive care) tehama ni Suluhu katika eneo hili.

Niipongeze serikali katika eneo hili imeanza kuchukua hatua kuhakiksha mama na mtoto wako salama , ambapo imeamua kuanzisha mfumo wa Dharula kwa mama na mtoto lakini mfumo huu bado unachangamoto kubwa sana kiasi ambacho unahitaji ubunifu mkubwa uweze kuleta Tija katika mikoa na wilaya zenye mazingira magumu kama vile Mbeya, Mwanza, na Singida.

Mwisho naomba kuwasilisha andiko langu, tehama italeta mapinduzi makubwa katika ufanisi wa tiba, matibabu, taarifa na itaongeza kasi ya usimamizi katika mapato yanayopotea mikononi wa watumishi katika kila kona ya nchi hii.

Piga kura tukalete mabadiliko, afya ni mifumo bora ya huduma, chezea pesa usichezee afya.
 
Nitaendelea kukuletea Attachment, za Maandiko mbali mbali yanayoonyesha umuhimu wa Tehama katika maisha ya sasa.

Wakati huu ambao tunahitaji kufanya kazi kwa Weledi na kuzifanya huduma za afya zisiwe kikwazo cha maendeleo yetu.

Screenshot_20230616-095634_Chrome.jpg
 
Mapato ya vituo yatalindwa na mifumo ya tehama, Ufungwaji wa GOTHOMIS, katika vituo vyote vinavyotoa Huduma, italeta Tija sana, itavipa vituo nguvu kujitegemea na kujiendesha.
 
Ni rahisi kufanya matibabu kwa kutumia Tehama, mawasiliano ya vitengo katika Taasisi moja yataboreshwa na mifumo imara ya Kidigitali.
 
Mapato ya vituo yatalindwa na mifumo ya tehama, Ufungwaji wa GOTHOMIS, katika vituo vyote vinavyotoa Huduma, italeta Tija sana, itavipa vituo nguvu kujitegemea na kujiendesha.
Mfumo wa sasa wa GOTHOMIS ni gharama sana kwa vituo kuafford installation na maintanance yake,mfumo ungekua web based ingekua rahisi na affordable
 
Ni kweli Gharama ya installlation na mantanace ni kubwa na inategemea kituo chenyewe.

Naomba tukupe fursa hapa hapa ya kwanini Webbased ni rahisi kuliko ulivyosaivi.??

Nimeona Mfumo huu wa Tausi ipo hivyi ni webbased, unautumia kirahisi sana. Sina uhakika na Security yake, wataalumu watatupitisha tuone.
 
Ubunifu, Wapewe Wazawa tunavyuo vya Ufundi vingi sana, na wanafanya vizuri sana, wapewe nafasi kuhakikisha wanachagiza katika kukuza Mifumo ya Huduma ya Afya.
 
Hapa chini nimekuwekea Picha kutoka Website ya Kitengo cha Damu salama cha nchi, Ukiitizama Website ya Kenya ukatizama website ya Tanzania utajisikia Vibaya au utaona kuna namna ambavyo tunaendesha mambo kienyeji pasipo kuwa na improvements yoyote ya kidigitali.

Inaonyesha vituo ambavyo mtu anaweza kwenda kuchangia Damu kwa hiari na pia inaonyesha uhitaji wa Damu kwa nchi pia utaona kuna Vituo kwenye kila eneo ambalo ni collection and supplier to needy. Why not us...inatulazimu kutumia gharama kubwa sana kupata Damu lakini Damu inabaki mijini...??
Screenshot_20230618-233509_Chrome.jpg
Screenshot_20230618-233455_Chrome.jpg
Screenshot_20230618-233428_Chrome.jpg
 
Wakati Rwanda inajikita katika kuboresha Matumizi ya Tehama kila eneo ambalo limekuwa na changamoto ya Tehama, usambazaji wa Dawa( kwa ndege isiyo na Rubani, Usambazaji wa Damu maeneo yasiyofikika kirahisi, usambazaji wa Chanjo katika maeneo ambayo hayafikiki kirahisi) Tanzania inapiga hatua 10 nyuma na kuipa kisogo Tehama kwenye mazingira ambayo tunahitaji Huduma bora kwa kila mtanzania, kipindi ambacho tunapambana kupeleka mswada wa BIMA KWA WOTE na ambao tunahitaji kutokomeza vifo vya mama na mtoto nchini.

LENGO
Kuikumbusha Serikali juu ya Jitihadi zake ambazo ilikuwa imeamua kuzichukua kuhakikisha Tehama inatawala na inachukua nafasi kubwa katika kuboresha upatikanaji wa Huduma sawa kwa watu wote maeneo yote nchini.

CHANGAMOTO KUENDESHA IDARA YA AFYA BILA TEHAMA
  1. Usambazaji wa vifaa tiba na Dawa ni eneo kubwa ambalo linaonyesha kusudi la serikali kufikia lengo la Huduma Bora kwa kila mtanzania, eneo ambalo limebaki katika njia zile zile miaka yote tangu uhuru hadi leo. Kuna halmashauri nchi hii zina magari yasiyozidi Matano magari haya yatumike na Idara zote ikiwemo ya Afya, idara hii yenye Ambulance Mbili, ambazo kuna muda zinaacha majukumu yake ya msingi na kufanya kazi ya kusambaza na kumsafirisha DMO kutokana na uhaba wa magari Ambulance inatumika kusafirisha wagonjwa na hiyo hiyo inatumika kusambaza Vifaa tiba na Dawa, kwenye halmashauri yenye Kata 25 na Vijiji zaidi ya 90, na vituo visivyopungua 50, yenye Jiografia tata ambapo kutoka kituo kimoja kwenda kingine unatumia Masaa mawili.
  2. Rufaa kushindwa kuandaliwa mazingira stahiki kabla ya kufika kutokana na kutokuwa na matumizi ya AUTOMATED Digital application kutoka kituo A-B ni moja ya sababu inayoipa serikali kutokutimiza lengo lake la kupeleka Huduma Bora ya Afya kwa watanzania, mfumo wa M-mama lengo kuu la kuokoa maisha ya mama na mtoto lakini aina ya Tehama inayotumika inahitaji miaka mingi kufikia hilo lengo la Tamisemi.
  3. Gharama kubwa kuendesha shughuli za kila siku za Vituo vyetu vya kutolea Huduma, Mfano ni lazima Idara iwe na Mafuta kila mwezi kwa ajili ya kusambaza Chanjo, Dawa , vitendanishi na kufanya usimamizi shirikishi kwa team ya afya Wilaya, kila mwisho wa mwezi lazima wasimamizi wa vituo wasafiri kwenda halmashauri/ Hospitali za wilaya kupeleka taarifa ya kila mwezi ya mwenendo wa Magonjwa (MTUHA) hii pia inaiingiza serikali kwenye gharama kubwa.
  4. Usimamizi na uthibiti wa Mapato, Eneo hili limetelekezwa kitu kinachopelekea kupoteza uhalali wa makusanyo ya kile kinachoingia kituo cha kutolea Huduma, kwa sasa ni (nini?)921 tu, vilivyo na Mfumo wa uthibiti taarifa za Vituo vya kutolea Afya (GOTHOMIS). Siyo rahisi mtu aliyepo IYUMBU awe na Fedha wiki nzima ambazo hazipo katika mfumo na asitumie Fedha mbichi, ni rahisi sana kuingia majaribuni anapokuwa na hiyo fedha ( ukizingatia hamna waasibu) katika vituo vyetu.
NINI KIFANYIKE (SOLUTION)
1. Mwekezaji tafutwe eneo la Ufungaji Wa Mifumo Ya GOTHOMIS katika Vituo vyote vya Kutolea Huduma
.
Kupata mwekezaji makini atakae saidia ufungaji wa miundombinu ya tehama katika vituo vyote nchini kama ambavvyo tunatafuta wadau katika maeneo mengine. Hii itaondoa upotevu wa Mapato, nakufanikisha kuongeza mapata yatakayofanya vituo viweze kujiendesha mijini na vijijini, tehama itaongeza uwajibikaji wa watoa huduma hususani mfumo wa GOTHOMIS ambao unatakiwa ufungwe hadi kwenye zahanati, ufungwaji wa mfumo huo utaleta Tija stahiki katika ukusanyaji wa Fedha na kupunguza upotevu na matumizi ya fedha mbichi kwenye vituo.

Na kama yupo basi mwekezaji/mdau huyu kuna namna anatakiwa kuongezewa nguvu maana kazi yake haionekani vijijini wala mijini. Picha na maelezo hapo chini ni mwaka 2018, hadi leo hakuna matokea ya mdau huyu.

NUKUU 2018: Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto na Taasisi isiyo ya kiserikali ya PATH chini ya Mpango wa kuboresha Matumizi ya Takwimu za Afya (Data Use Partinership -DUP) imejiwekea mikakati ya kuongeza ufanisi katika utoaji huduma ya Afya kwa kuiweka Mifumo ya TEHAMA katika ngazi ya huduma ya Afya ya Msingi ili Wananchi waweze kupata huduma bora za afya.

TEHAMA kuongeza ufanisi kwa mtumishi wa afya ngazi ya zahanati

View attachment 2658925
Imewekwa Tar 12th September, 2018
2. Wizara ikaribishe Ubunifu eneo la Taarifa (Wazawa wapewe nafasi ya kuonyesha uzalendo kwa nchi yao)

Ubunifu uanzie katika matumizi ya kutunza na kutuma taarifa za wagonjwa na magonjwa na shughuri nyigine zinazoendelea katika kituo husika, ujenzi, kampain mbali mbali na kumbukumbu zake kwa gharama nafuu.

Mnakumbuka mtumishi bora wa Mbeya ambae ni Mtaalumu wa Tehama? Watu kama hawa wanapewa zawadi tu na kuishia kupata zawadi lakini hawapewi nafasi ya kufanya kazi na kuendeleza ubunifu wao.
Tehama italeta Tija katika kupunguza gharama za kupeleka taarifa kila mwisho wa mwezi, pia itatoa fursa kwa vituo vinavyotoa huduma kuwa na utulivu wa kufanya kazi, na kupunguza gharama za uendeshaji wa kituo, kupunguza kusafiri kila mwisho wa mwezi au ndani ya mwezi wakati kituo kikiwa na uhaba wa watumishi.

Wabunifu waelekezwe kutegeneza mifumo itakayoishia Wilayani/mikoani kabla ya kwenda na ngazi za maamuzi (Mfumo utafanya pre-audit kabla ya kufika Wizarani) ni Imani yangu kubwa kuwa mifumo yao local italeta tija kusaidia mifumo ya wizara ambayo ni ngumu kufika vijijini na ikafanya vizuri.

3. Ndege bila Rubani, eneo la usambazaji wa vifaa tiba na dawa vijijini
Matumizi ya Ndege zisizo na Rubani, Rwanda kwa sasa inasambaza vifaa tiba na Dawa kutumia ndege zisizo na rubani, wakati tunaazimisha uchangiaji Damu kwa Watanzania kwa ajili ya kuokoa maisha ya wahitaji kama mama wajawazito na wahanga wa ajali, kuna sehemu ya nchi hii ni ngumu kuona tone la hiyo damu iliyokusanywa kwa sababu ya miundombinu ya utunzaji wa hiyo damu katika mazingira haya, serikali ikiamua kuwekeza kwenye tehama ni rahisi damu kufika kwa kutumia ndege za dharula hata katika maeneo ambayo ni ngumu kufika (HARD TO REACH AREA).

4. Mfumo wa rufaa ubadilike
Matumizi ya rufaa ya karatasi tuachane nayo twende kidijitali kuna faida nyingi kuliko mfumo huu tulionao leo ni dhaifu sana kuhamia katika Tehama itaongeza ufanisi, kupunguza vifo vya mama na mtoto, ajali na magonjwa mengine yanayohitaji uangalizi mkubwa ( intensive care) tehama ni Suluhu katika eneo hili.

Niipongeze serikali katika eneo hili imeanza kuchukua hatua kuhakiksha mama na mtoto wako salama , ambapo imeamua kuanzisha mfumo wa Dharula kwa mama na mtoto lakini mfumo huu bado unachangamoto kubwa sana kiasi ambacho unahitaji ubunifu mkubwa uweze kuleta Tija katika mikoa na wilaya zenye mazingira magumu kama vile Mbeya, Mwanza, na Singida.

Mwisho naomba kuwasilisha andiko langu, tehama italeta mapinduzi makubwa katika ufanisi wa tiba, matibabu, taarifa na itaongeza kasi ya usimamizi katika mapato yanayopotea mikononi wa watumishi katika kila kona ya nchi hii.

Piga kura tukalete mabadiliko, afya ni mifumo bora ya huduma, chezea pesa usichezee afya.
Iko vizuri, hebu tujifunze na hapa SoC03 - Umuhimu wa kamera za ulinzi (cctv camera) katika vyombo vya usafiri wa umma na vituo vyake hapa nchini
 
Back
Top Bottom