Tegeta Escrow: Stanbic Bank yatoa Press Statement

Mkombozi haijaeleza kuhusu wanabodi wake waliopokea kitita, umesahau na wametajwa?

Kama walilipwa kwa njia ya TISS bado sioni walipokosea kwa mujibu wa sheria, sheria inasema pesa zaidi ya 15M transactions zake zinatakiwa kufanyika electronically na ndio maana PAC na CAG and may be PCCB waliweza kujua nani kaingiziwa ngapi kutoka kwa JR, shida iko hapo Stanbic wao walifanya manually and this is why huwezi jua nani alipata ngapi. Nimeandika haya nikiwa ninauhakika kwamba haya unayaelewa vizuri sana lakini kwakua wewe hua na aleji na kanisa hasa la RC umejifanya kupindisha ufahamu.
 
TAARIFA KWA UMMA:

Stanbic Bank Tanzania inayo taarifa ya ripoti ya Bunge inayohusu IPTL na akaunti ya Tegeta Escrow na tuhuma kwa Stanbic kutakatisha fedha haramu kwa kujihusisha na wahusika wakuu wa kashfa hiyo.

Tunapenda kuthibitisha kwamba Stanbic Bank Tanzania ilizingatia sheria kanuni na taratibu zote zinazotakika za kupambana na fedha haramu, na pia kuweza kushirikiana vyema na mamlaka yanayohusika katika uchuguzi wao.

Tungependa kuwahakikishia wateja wetu kwamba Stanbic Bank Tanzania siku zote inafuata masharti yote pamoja na sheria za maadili na udhibiti zilizowekwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tutaendelea na nia yetu thabiti ya kuwatumikia wateja wetu siku zote.

UTAWALA
STANBIC BANK TANZANIA


SOURCE: NIPASHE, pg. 04

MY TAKE:

Hebu linganisha taarifa hii ya Stanbic ambayo imechelewa na inatoka leo wakati bunge limeisha wiki iliyopita na wabunge wako majumbani mwao, kisha linganisha na taarifa ya MKOMBOZI BANK iliyotoka wakati Bunge bado linaendelea.

Taarifa ya Mkombozi Bank si tu kwamba tuliiona, tuliijadili humu vya kutosha na wale ambao hawakuipata wasome thread hii (Bonyeza hapa).

Taarifa ya Mkombozi Bank inaeleza hadi tarehe yaani mtiririko wa matukio. Mkombozi Bank imeonyesha kwamba kila mtu aliingiziwa hela kwa TISS, yaani kwenye account yake na hivy hakuna mtu aliyeingiziwa hela kwa cash akajaze kwenye viroba, magunia au mifuko ya rambo na marbolo.


Stanbic hawasemi hilo. Wanasema tu walifuata taratibu bila kutaja mtiririko wa utaratibu na ku-dispute tuhuma za bungeni.


Mkombozi Bank walieleza jinsi walivyoshinikiza fedha zkatiwe kodi na ikapatikana Bilioni 38. Stanbic haisemi hilo wala haitaji kama kupitia Stanbic tumepata walau senti tano!

Kupitia Mkombozi Bank, tumeweza kujua majina ya waliopokea kama Tibaijuka, Kilaini, Nzigilwa, Ngeleja na wengine tele.

Stanbic haikutaja kabisa hili na hadi hii statement yao hatujajua ni akina nani walilipwa na kwa nia gani.

Hivyo, kwangu statement hii haiwasaidii lolote na badala yake imeonekana kwamba Mkombozi Bank imefanya jambo hili kwa uwazi kuliko kwa kifichoficho kama walivyofanya Stanbic na kama wanavyoendelea kufanya hata leo kwenye statement yao.


JADILI

Pamoja na maelezo yako mareefu bali ukweli unakuwa hivi. Stanbic wameshindwa kisema uongo kuwa hawajatakatisha fedha kwa hilo liko wazi. Kwa maneno mengine hawakuwa na haja ya kukanisha jambo la kweli. Pia walishachukua hatua kwa watumishi waliohusika. Taarifa ya Mkombozi bank ni mwendelezo wa kuwasafisha na kuwalinda mafisadi ambao ndio wateja wao wakuu wa kuwasafishia hela. Hiv kama maaskofu wa kanisa wanaomiliki bank ya mkombozi walihusika kufanikisha uharamia huu, je ulitarajia vimeneja pale mkombozi viseme ndio viwachafue maasikofu? Rafiki yangu anapenda kusema "with money i can buy even a police man". Na huu ndio ukweli that;5 "a bishop was bought".
Hizi taarifa mbili zinaeleweka tu mkombozi ni ya kupika na hii ya stanbic iko njia panda maana kukiri ni ukweli mchungu
 
Hii Meridien ndiyo iliwahi kuwaliza watu miaka ya tisini. Bila shaka ndicho kinachoelekea kwa Stanbic ndio maana wanatoa taarifa za kujiumauma.

Hivi nani alikuwa waziri wa Fedha wakati huo? Sio bwana majanga?
 
Taarifa ya bank hiyo haijafafanua kama bank ya Ukombozi ifuatayo hapo chini ilivyofanya

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AKAUNTI YA VIP ENGINEERING AND MARKETING ILIYOPO KATIKA BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI
Utangulizi


Taarifa hii inatolewa kwa umma kutokana na ripoti mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari mitandao ya kijamii na taarifa iliyotolewa kwenye mjadala katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Ufunguzi wa akaunti ya VIP engineering and Marketing (VIP)


Kampuni ya VIP engineering and Marketing ni kampuni ambayo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Kampuni hii ilifungua akaunti katika benki ya biashara ya Mkombozi na hivyo kuwa moja kati ya wateja wa benki. Benki ilijiridhisha na ilizingatia taratibu zote za ufunguzi wa akaunti husika kwa kuzingatia sheria za nchi na kanuni zinazozitaka benki kupata nyaraka muhimu kutoka kwa mteja wakati wa ufunguzi wa akaunti hiyo.

Nyaraka hizo ni pamoja na kuwepo kwa cheti cha usajili wa kampuni, kanuni za kampuni, idhinisho la kampuni kumruhusu moja kati ya wanahisa wake kuendesha akaunti pamoja na picha na hati ya kusafiria ya mhusika wa kuendesha akaunti hiyo.

2.0 Mauzo ya hisa za VIP

Kampuni ya VIP ilileta mkataba kwenye benki ya Mkombozi wa mauziano ya hisa za asilimia 30 baina ya VIP na kampuni ya Pan Africa Power Solutions (PAP) ambazo inamiliki katika kampuni ya IPTL. Mkataba huo ulisainiwa tarehe 19 Ogasti, 2013. Bei ya asilimia 30 ya hisa hizo ilikuwa ni dola za Marekani milioni 75. Katika kifungu namba 2.4 cha mkataba wao kinaelekeza fedha za mauzo ya hisa zilipwe kwenye akaunti ya VIP iliyopo benki ya Mkombozi. Mkataba huo wa mauziano ya hisa baina ya kampuni hizi mbili ulitambuliwa na hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa na Jaji J.H.K Utamwa tarehe 5 Septemba, 2013.

3. Mchakato wa kulipa kodi ya serikali


Benki ilitambua kwamba katika mauziano hayo ya hisa ni lazima kodi ya Serikali ilipwe na hivyo iliizishauri pande zote mbili kupeleka mkataba husika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufanyiwa makadirio ya kodi husika. Tarehe 20 Januari, 2014 TRA iliiandikia barua kampuni ya VIP na nakala ya barua hiyo kuletwa kwenye benki ya Mkombozi. Katika barua hiyo TRA iliitaarifu kampuni ya VIP kuwa makadirio ya kodi yatokanayo na mauzo ya hisa ni shilingi 38,186,584,322.00 ikiwa ni kodi ya mauzo ya hisa ya asilimia 30 za mauzo ya hisa kutoka VIP kwenda kwa PAP.(Capital gains and stamp duty).

TRA pia iliiagiza benki ya Mkombozi kuhakikisha kuwa inalipa kodi hiyo kwa niaba ya VIP mara tu fedha zitakapoingia kwenye akaunti yake.

Malipo ya kodi ya shilingi 38,186,584,322.00 yalilipwa TRA kwenye akaunti 11120100 iliyopo katika Benki Kuu ya Tanzania na TRA ilikiri kupokea kodi hiyo kwa barua yake yenye kumbukumbu namba 3-4/100/100/223/4 ya tarehe 24 Januari, 2014.

4. Ufafanuzi wa mambo mbalimbali


4.1 Benki ya mkombozi kuhusika katika kusafisha fedha chafu

Fedha zote zilizoingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo kwenye benki ya Mkombozi zilitokana na mauziano ya hisa kati ya VIP na PAP kwa mkataba uliotambuliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania. Chanzo cha malipo hayo ni kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya PAP iliyopo katika benki ya Stanbic na kuingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo katika benki ya Mkombozi.

Fedha hizo zilihamishwa katika mafungu mawili. Fungu la kwanza ilikuwa ni shilingi 73,573,500,000.00 zilihamishwa kwa njia ya TISS kwa kumbukumbu namba 000000050720 ya tarehe 23 Januari, 2014 na fungu la pili ni dola za Kimarekani 22,000,000.00 zilihamishwa kwa TISS kwa kumbukumbu namba000000050812 ya tarehe 23 Januari, 2014. Malipo mengine ya asilimia kumi ya mauzo ya hisa yalilipwa kwenye akaunti ya Mkombozi iliyopo Benki Kuu ya Tanzania. Kutokana na mchakato huo benki ya Mkombozi ilijiridhisha kuwa fedha hizo ni malipo halali na siyo fedha chafu.

Benki ya Mkombozi haijihusishi na utakasishaji wa fedha chafu na haramu katika uchumi wa Tanzania.

4.2 Malipo yatokanayo na akaunti ya VIP

Malipo toka kwenye akaunti ya mteja hufanywa kutokana na maelekezo ya mteja. Benki ikishajiridhisha kuwa fedha ya mteja ni halali na ipo kwa mujibu wa sheria na hamna zuio lolote toka katika mahakama hapa nchini hutekeleza malipo kwenye akaunti ya mteja kutokana na maelekezo yake.

Benki ilijiridhisha kuwa malipo yote yaliyofanywa kutoka kwenye akaunti ya VIP ni halali kwa kuwa chanzo cha pesa hizo ilikuwa ni halali kutokana na mauzo ya hisa na ulipwaji wa kodi ya Serikali kama ilinyoelezwa hapo juu. Kutokana na sababu hiyo benki haikuwa na shaka juu ya malipo hayo.

4.3 Malipo taslimu kwa wateja na kubeba fedha kwenye viroba, mifuko ya rambo na magunia

Benki inatoa tamko kuwa malipo yote yaliyofanywa katika akaunti ya VIP yalilipwa kupitia akaunti za walipwaji. Hakuna fedha zilizolipwa taslimu kwa wateja na kubebwa kwenye viroba au magunia kama ilivyoripotiwa Bungeni. Pesa iliyotoka kwenye akaunti ya VIP tarehe 6 Februari, 2014 kiasi cha shilingi 3,314,850,000.00 ililipwa kwenye akaunti nane za wateja tofauti na siyo kubebwa kwenye viroba au magunia.

Na zile zilizotoka toka benki ya Stanbic zilizotajwa hapo juu zilitumwa kwa njia ya TISS na siyo kubeba kwenye magunia au viroba.

4.4 Malipo kwa mfanyakazi wa benki ya Mkombozi

Gazeti la Mawio la tarehe 20-26, Novemba, 2014 tolea namba 0122 liliandika kuwa mwanasheria wa benki ya Mkombozi ajulikanaye kwa jina la Rweyengeza Alfred alipokea malipo toka akaunti ya VIP ya shilingi milioni 40.2.

Benki inatoa tamko kuwa haina mfanyakazi anayetambuliwa kwa jina hilo na wala hakuna mfanyakazi yeyote wa benki aliyelipwa fedha toka kwenye akaunti ya VIP.

Wito kwa umma

Benki ya Mkombozi inachukua fursa hii kuwatarifu wateja wake na umma kutopotoshwa na taarifa au tuhumma zilizofafanuliwa hapo juu na kuwataka wateja wake wote kutokuwa na hofu yeyote kwani benki ipo imara na inafanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa na Benki Kuu ya Tanzania. Benki inawataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kutoyumbishwa na tuhumma hizo ambazo hazina ukweli ndani yake na badala yake waitumie benki yao kwa shughuli za maendeleo ya nchi yetu.

Pamoja tunajenga nchi na uchumi wa nchi yetu.

Hitimisho

Benki ya biashara ya Mkombozi haijihusishi na haitajihusisha na utakasishaji wa fedha chafu.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI
 
Hawa Stanbic wanaleta ujeuri wa kikaburu. Nchi hii ingekuwa na viongozi makini,mpaka sasa leseni yao ingekuwa imeshafutwa na Benki zote duniani kujulishwa kuwa hii ni benki ya kutakatisha fedha haramu za rushwa. Kwangu mimi hii ni Tegeta Escrow Bank. Warudishe pesa zetu walizitoa kwa magunia.
 

Attachments

  • Picture11.jpg
    Picture11.jpg
    101.4 KB · Views: 138
kweli nchi hii hatuko serious hata hawa tuliodhani ni waadilifu wanatoa taarifa kama mume anayemwachia mkewe taarifa kuwa yeye kasafiri. shame on them
 
...mie najiuliza haya yanatokea vipi kwenye nchi yenye yenye serikali makini.
Wakati 'wajanja' wanakwapua yale mabilioni pale Stanbic kwa kushindilia manoti kwenye viroba na kwenye magunia ya lumbesa, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, vilikuwa vimechukua 'unpaid' leave!
 
Naona Citizen wametenda haki, kwa kutujulisha aliyehusika article hii hapo, Ni Mganda Mmoja kwa jina la Paul Omara, ndio aliyewezesha mambo yote. Article chini
Dar es Salaam. Stanbic Bank Tanzania is at a crossroads following Parliament's resolution that the bank be investigated and tasked to help recover the Tegeta escrow account billions after it was accused of gross violation of anti-money laundering rules.
All the $122 million (Sh207 billion) which was deposited in the account that was under the watch of the Bank of Tanzania (BoT) was paid into two accounts operated by Pan African Power Solutions Tanzania Limited (PAP) at Stanbic Bank in November and December, last year.
PAP falsely claimed it had acquired 70 per cent of Independent Power Tanzania Limited (IPTL) in 2010 from the Malaysian company Mechmar. This enabled PAP to win the trust of some top government officials, who, in turn, helped it to secure the remaining 30 per cent from the local shareholder, VIP Engineering, for $75 million. An audit by the Controller and Auditor General (CAG) has established that PAP did not legally acquire a 70 per cent stake in IPTL as claimed by the firm. It was stated during a heated debate in Parliament last week that the bank failed to prevent money laundering when it allowed the transfer of millions of dollars to Australia and South Africa.
MPs said the transactions were questionable because they were not backed by proper documentation to justify the movement of such vast sums.
Stanbic was also accused of allowing withdrawals totalling Sh73 billion within a "very short period", prompting investigators from the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) to question the bank's top executives.
The transactions, Parliament was told, were captured on the bank's closed circuit televisions, whose footage showed individuals withdrawing large amounts of cash from PAP's accounts.
Parliament now wants the bank investigated, penalised and forced to return the Tegeta escrow billions.
In what could tarnish the image of one of Africa's biggest banks, especially in South Africa, Stanbic Tanzania is at a crossroads as it seeks to clear its reputation as well as cooperate with PCCB officials in tracing the whereabouts of the escrow monies.
Last Friday, Stanbic Bank Tanzania CEO Ken Cockerill wrote an internal email directing staff on how to handle the aftermath of the escrow saga
"There has been a lot of hype over the last few days in respect of the Tegeta escrow account saga, which is currently being discussed in Parliament," he wrote.
"I would like to take this opportunity to reassure you that the bank has complied with all of its fiduciary and regulatory obligations. In addition we have given our full cooperation to the relevant authorities.
"I am confident that our business will not be affected, and count on your support to convey this message to our customers…If any of you are approached by the media, please refer these queries to Desideria Mwegelo, our Head of Marketing & Corporate Affairs," Mr Cockerill concluded in his email.
But Mr Cockerill could not be reached for further clarification yesterday.
The Citizen has reliably established that after a series of interrogations by PCCB officials on how Stanbic handled the two accounts belonging to PAP, one of the bank's top officials, Mr. Paul Omara, who was the head of personal and business banking (PBB), was forced to resign last month.
The Ugandan national, who had been with the bank for 11 years, was accused of sanctioning questionable transfers from PAP accounts to overseas accounts.
He was also accused of failing to notify or alert the relevant authority responsible for curbing money laundering. Mr Omara was briefly detained by PCCB officials after his resignation before he was bailed out by a local businessman, pending the final report on the escrow probe.
Speaking when Parliament was debating the escrow saga on Friday, Finance deputy minister Mwigulu Nchemba ordered the two banks that were involved in the transactions to issue official statements to the government and general public on how they handled the monies.
Only Mkombozi Commercial Bank has so far issued an official public statement detailing how it handled VIP Engineering's account as well as transfers from the account to lawyers, judges,
MPs, journalists, ministers and religious leaders, among other recipients
Source: Stanbic at a crossroads over escrow billions - National - thecitizen.co.tz
 
Nimeisoma hii statement ya Stanbic bank, ni hovyo kabisa hamna kitu hapa. Yaani hajajibu tuhuma za kutoa mabilioni ya pesa kwa cash suala ambalo ni kinyume na sheria za BOT
 
Pamoja na maelezo yako mareefu bali ukweli unakuwa hivi. Stanbic wameshindwa kisema uongo kuwa hawajatakatisha fedha kwa hilo liko wazi. Kwa maneno mengine hawakuwa na haja ya kukanisha jambo la kweli. Pia walishachukua hatua kwa watumishi waliohusika. Taarifa ya Mkombozi bank ni mwendelezo wa kuwasafisha na kuwalinda mafisadi ambao ndio wateja wao wakuu wa kuwasafishia hela. Hiv kama maaskofu wa kanisa wanaomiliki bank ya mkombozi walihusika kufanikisha uharamia huu, je ulitarajia vimeneja pale mkombozi viseme ndio viwachafue maasikofu? Rafiki yangu anapenda kusema "with money i can buy even a police man". Na huu ndio ukweli that;5 "a bishop was bought".
Hizi taarifa mbili zinaeleweka tu mkombozi ni ya kupika na hii ya stanbic iko njia panda maana kukiri ni ukweli mchungu

Mkuu kwenye hiyo red nina maswali kadhaa naomba unijibu
  • Je pesa ya VIP ilikuwa ni malipo halali ya hisa au haikuwa halali?
  • Je TRA walipokea kodi bilioni 38 au hawakupokea?
  • Je pesa chafu inapiwaje kodi wakati chanzo chake ni kichafu?
  • Mwenye mamlaka ya kutoa agizo la kutolewa pesa kwenye akaunti ya mteja ni mteja mwenyewe au ni benki?
  • Kama suala ni kuwakingia kifua maaskofu, kwa nini wakubali kutoa bank statement ambayo inaonyesha majina ya maaskofu?
  • Kama suala ni kutakatisha fedha haramu, kwa nini waliopata pesa walikubali kufungua akaunti kwa majina yao halisi huku wakijua pesa wanazochukua ni za wizi?
  • BOT kama msimamizi mkuu wa mabenki nchini, kwa nini aliziangalia tu bilioni 73 zikitoka Stanbic kwenda Mkombozi bila kuhoji maswali yoyote?
 
Press Release hii imeandikwa na Mtanzania? Au ni Mhindi alikuwa akijifunza Kiswahili? Au ni Mtanzania ambaye ni mweupe kabisa kichwani? Should we call it "Press Release"? What a joke!
 
Huo mgao inawezekana hata rais wa nchi hii kachukua ndiyo maana kimyaaaaaaaaaaa
haya bwana yetu macho.
 
sometimes kukaa kimya kunatoa jibu la maana kuliko kuongea pumba. hawakuwa na shinikizo lolote la kutoa press statement. wangeendelea kujikalia kimya tu ingekuwa na maana zaidi kuliko hiki walichokifanya. after all uzoefu unaonesha kuwa 'news' yoyote haikai kwenye media kwa zaidi ya wiki mbili. itatokea news nyingine na kwa vile sisi ni watz tutaisahau za zamani na tutahamia kwenye mpya na maisha yataendelea!
 
Mkuu kwenye hiyo red nina maswali kadhaa naomba unijibu
  • Je pesa ya VIP ilikuwa ni malipo halali ya hisa au haikuwa halali?
  • Je TRA walipokea kodi bilioni 38 au hawakupokea?
  • Je pesa chafu inapiwaje kodi wakati chanzo chake ni kichafu?
  • Mwenye mamlaka ya kutoa agizo la kutolewa pesa kwenye akaunti ya mteja ni mteja mwenyewe au ni benki?
  • Kama suala ni kuwakingia kifua maaskofu, kwa nini wakubali kutoa bank statement ambayo inaonyesha majina ya maaskofu?
  • Kama suala ni kutakatisha fedha haramu, kwa nini waliopata pesa walikubali kufungua akaunti kwa majina yao halisi huku wakijua pesa wanazochukua ni za wizi?
  • BOT kama msimamizi mkuu wa mabenki nchini, kwa nini aliziangalia tu bilioni 73 zikitoka Stanbic kwenda Mkombozi bila kuhoji maswali yoyote?

Mlolongo mzima tangu kuuziana hisa uligubikwa na utata Kama ulisikia vizuri ripoti ya Pac lakini vilevile hata kodi iliyolipwa ilikuwa Ni Kama kujisafisha Ili likitokea lolote ijulikane hata kodi imelipwa hapa Kuna maafisa WA tra wanahusika. Suala la kutoa fedha au kuweka fedha halimuondolei banker kisheria kufuata taratibu za ufunguaji akaunti ,uwekaji au utoaji WA fedha za mteja. Ni lazima bank ijiridhishe to the maximum kuwa fedha yoyotte inayoingia katika akaunti ya mteja Ni halali Na hata inapotoka Ni lazima itolewe kwa utaratibu unaoeleweka Na Si Kama ilivyofanyika.
 
Mlolongo mzima tangu kuuziana hisa uligubikwa na utata Kama ulisikia vizuri ripoti ya Pac lakini vilevile hata kodi iliyolipwa ilikuwa Ni Kama kujisafisha Ili likitokea lolote ijulikane hata kodi imelipwa hapa Kuna maafisa WA tra wanahusika. Suala la kutoa fedha au kuweka fedha halimuondolei banker kisheria kufuata taratibu za ufunguaji akaunti ,uwekaji au utoaji WA fedha za mteja. Ni lazima bank ijiridhishe to the maximum kuwa fedha yoyotte inayoingia katika akaunti ya mteja Ni halali Na hata inapotoka Ni lazima itolewe kwa utaratibu unaoeleweka Na Si Kama ilivyofanyika.

Kwa mtazamo wako ni sheria ipi ambayo Mkombozi imekiuka? Je ulitaka Mkombozi wawaite TAKUKURU, Usalama wa Taifa, CAG na vyombo vingine vya dola vichunguze ndipo wapokee fedha za mauzo ya hisa? Kama benki ilifanya KYC ipasavyo unataka ifanye kipi cha ziada?
 
Back
Top Bottom