Tegeta Escrow: Stanbic Bank yatoa Press Statement

Tegeta Escrow: Stanbic Bank yatoa Press Statement

tatizo mwiguru aliwaambia watoe taarifa kukanusha,sababu wakikaa kimya wataonekana kweli.hamkumuelwewa MWIGURU
 
hii riport iko shallow either kwa makusudi kuficha kitu au stanbic kuna vilaza sana inafaa kufungiwa maandazi hiii
 
Kwanza walichofanya ni dharau kwa bunge na kwa Naibu Waziri. Wanatoa statement muda wanaojisikia wao.
 
Kama ni wasafi CEO wao wamemtimua kwasababu gani, waache siasa wakati huu sisi Watanzania tunauchungu sana. Kama walifuata sheria je unaruhusiwa kutoa mabilioni hayo kwa siku mbili tena katika viroba na magunia.
Siyo tu CEO hata yule dogo aliyefungua ac hiyo ametimukiwa. Why wawatimue km taribu zilifuatwa?
 
Pesa imelipwa kutoka kwenye account BOT kwenda stanbic.

Ilipotoka BOT ilikuwa safi,ilipofika Stanbic ikachafuka.

Wewe utakuwa na akili nyingi sana kama mimi, nilikuwa najiuliza hivyo hivyo. Kwanini tusianzie BOT kwanza, kwa sababu kama BOT walizitoa hizo kwenda benki nyingine maana yake zilikuwa safi, kosa ambalo naona Stanbic wamefanya pengine ni kurusu hele hizo kuchukuliwa kama Cash zaidi ya kiwango cha cash kinachotakiwa, vinginevyo wangefanya TISS wangekuwa clean kama wenzao Mkombozi.
 
Huku Ni kuwakosea heshima Na adabu watanzania nilikua nawaheshimu Sana hii bank lakini kwa statement hii Ni wazi wametudharau Sana hii ni statement ya kihuni Ni dawa Na tangazo la mkutano WA kijiji. Nilitegemea wangekuja Na statement ya kitaalamu inayotoa uchambuzi WA kina kwa haya yalitokea. Kwa statement hii Ni wazi kuwa WA ehusika kikamilifu katika utakatishaji WA fedha haramu.period
 
Lol, nimekimbilia kufungua uzi..kumbe ni utoto mtupuu...

Jamani huyo aliyetoa hilo tamko kweli anajua anachofanya kweli..??

Kwann wasielezee kama wenzao wa mkombozi bank??...

Walau hata kuonyesha mtiririko wa matukio ulivyokwenda???

Kweli mmetuona sio wananchi ni majinga mpaka mnatudanganya kiasi hiki...kweli kweliii inauma sanaa...
 
TAARIFA KWA UMMA:

Stanbic Bank Tanzania inayo taarifa ya ripoti ya Bunge inayohusu IPTL na akaunti ya Tegeta Escrow na tuhuma kwa Stanbic kutakatisha fedha haramu kwa kujihusisha na wahusika wakuu wa kashfa hiyo.

Tunapenda kuthibitisha kwamba Stanbic Bank Tanzania ilizingatia sheria kanuni na taratibu zote zinazotakika za kupambana na fedha haramu, na pia kuweza kushirikiana vyema na mamlaka yanayohusika katika uchuguzi wao.

Tungependa kuwahakikishia wateja wetu kwamba Stanbic Bank Tanzania siku zote inafuata masharti yote pamoja na sheria za maadili na udhibiti zilizowekwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tutaendelea na nia yetu thabiti ya kuwatumikia wateja wetu siku zote.

UTAWALA
STANBIC BANK TANZANIA

SOURCE: NIPASHE, pg. 04

MY TAKE:

Hebu linganisha taarifa hii ya Stanbic ambayo imechelewa na inatoka leo wakati bunge limeisha wiki iliyopita na wabunge wako majumbani mwao, kisha linganisha na taarifa ya MKOMBOZI BANK iliyotoka wakati Bunge bado linaendelea.

Taarifa ya Mkombozi Bank si tu kwamba tuliiona, tuliijadili humu vya kutosha na wale ambao hawakuipata wasome thread hii (Bonyeza hapa).

Taarifa ya Mkombozi Bank inaeleza hadi tarehe yaani mtiririko wa matukio. Mkombozi Bank imeonyesha kwamba kila mtu aliingiziwa hela kwa TISS, yaani kwenye account yake na hivy hakuna mtu aliyeingiziwa hela kwa cash akajaze kwenye viroba, magunia au mifuko ya rambo na marbolo.

Stanbic hawasemi hilo. Wanasema tu walifuata taratibu bila kutaja mtiririko wa utaratibu na ku-dispute tuhuma za bungeni.

Mkombozi Bank walieleza jinsi walivyoshinikiza fedha zkatiwe kodi na ikapatikana Bilioni 38. Stanbic haisemi hilo wala haitaji kama kupitia Stanbic tumepata walau senti tano!

Kupitia Mkombozi Bank, tumeweza kujua majina ya waliopokea kama Tibaijuka, Kilaini, Nzigilwa, Ngeleja na wengine tele.

Stanbic haikutaja kabisa hili na hadi hii statement yao hatujajua ni akina nani walilipwa na kwa nia gani.

Hivyo, kwangu statement hii haiwasaidii lolote na badala yake imeonekana kwamba Mkombozi Bank imefanya jambo hili kwa uwazi kuliko kwa kifichoficho kama walivyofanya Stanbic na kama wanavyoendelea kufanya hata leo kwenye statement yao.

JADILI

Stanbic Bank ni wahuni ,Taatifa haijaitosheleza utafikiri imeandikwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ya Magogoni.
 
Ni kosa la kisheria kutoa bank account details.
 
hii taarifa atakuwa kaiandika assumpta mshana,lusinde,komba au hawa ghasia....stupid bank
 
Too general!!

Walitakiwa watoe specific answers for specified problems!!
 
Siamini hichi kilichoandikwa apa ndio kimeandikwa na bank kama bank au mtu kajifungia ofisini kaamua kuandika kama ana post kule facebook...duh kwa kweli inasikitisha sana
 
Stanbic Bank in Tanzania is a member of the Standard Bank Group of South Africa and was established in May 1995 when the Standard Bank Group acquired the operations of Meridien Biao Bank Tanzania Limited. About Stanbic Bank
Hii Meridien ndiyo iliwahi kuwaliza watu miaka ya tisini. Bila shaka ndicho kinachoelekea kwa Stanbic ndio maana wanatoa taarifa za kujiumauma.
 
TAARIFA KWA UMMA:

Stanbic Bank Tanzania inayo taarifa ya ripoti ya Bunge inayohusu IPTL na akaunti ya Tegeta Escrow na tuhuma kwa Stanbic kutakatisha fedha haramu kwa kujihusisha na wahusika wakuu wa kashfa hiyo.

Tunapenda kuthibitisha kwamba Stanbic Bank Tanzania ilizingatia sheria kanuni na taratibu zote zinazotakika za kupambana na fedha haramu, na pia kuweza kushirikiana vyema na mamlaka yanayohusika katika uchuguzi wao.

Tungependa kuwahakikishia wateja wetu kwamba Stanbic Bank Tanzania siku zote inafuata masharti yote pamoja na sheria za maadili na udhibiti zilizowekwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tutaendelea na nia yetu thabiti ya kuwatumikia wateja wetu siku zote.

UTAWALA
STANBIC BANK TANZANIA

SOURCE: NIPASHE, pg. 04

MY TAKE:

Hebu linganisha taarifa hii ya Stanbic ambayo imechelewa na inatoka leo wakati bunge limeisha wiki iliyopita na wabunge wako majumbani mwao, kisha linganisha na taarifa ya MKOMBOZI BANK iliyotoka wakati Bunge bado linaendelea.

Taarifa ya Mkombozi Bank si tu kwamba tuliiona, tuliijadili humu vya kutosha na wale ambao hawakuipata wasome thread hii (Bonyeza hapa).

Taarifa ya Mkombozi Bank inaeleza hadi tarehe yaani mtiririko wa matukio. Mkombozi Bank imeonyesha kwamba kila mtu aliingiziwa hela kwa TISS, yaani kwenye account yake na hivy hakuna mtu aliyeingiziwa hela kwa cash akajaze kwenye viroba, magunia au mifuko ya rambo na marbolo.

Stanbic hawasemi hilo. Wanasema tu walifuata taratibu bila kutaja mtiririko wa utaratibu na ku-dispute tuhuma za bungeni.

Mkombozi Bank walieleza jinsi walivyoshinikiza fedha zkatiwe kodi na ikapatikana Bilioni 38. Stanbic haisemi hilo wala haitaji kama kupitia Stanbic tumepata walau senti tano!

Kupitia Mkombozi Bank, tumeweza kujua majina ya waliopokea kama Tibaijuka, Kilaini, Nzigilwa, Ngeleja na wengine tele.

Stanbic haikutaja kabisa hili na hadi hii statement yao hatujajua ni akina nani walilipwa na kwa nia gani.

Hivyo, kwangu statement hii haiwasaidii lolote na badala yake imeonekana kwamba Mkombozi Bank imefanya jambo hili kwa uwazi kuliko kwa kifichoficho kama walivyofanya Stanbic na kama wanavyoendelea kufanya hata leo kwenye statement yao.

JADILI

Mkombozi haijaeleza kuhusu wanabodi wake waliopokea kitita, umesahau na wametajwa?
 
nadhan hii ilikuwa n memo kwenda kwa mwigulu co statement kwa ajili ya umma..
 
Back
Top Bottom