Team nzima ya CHADEMA ndani ya Kahama leo mapokezi ya James Lembeli

Team nzima ya CHADEMA ndani ya Kahama leo mapokezi ya James Lembeli

11800224_899956853395741_2754373531902966419_n.jpg
 
Kwa mapokezi aliyoyapata huko Kahama,James Lembeli ni moto mkali. Kuanzia msafara wa pikipiki na magari,kubebwa kichifu na umati kwenye mkutano wake Lembeli hazuiliki.

Kujipambanua kwake kama mpambanaji dhidi ya ufisadi kunamtunza na kumhakikishia ushindi. Iliripotiwa humu kuwa Lembeli alizomewa. Leo walioripoti wameumbuka na kuonekana waongo.
Kila la heri Mh. James Lembeli

Tahadhari: Yasije kujirudia mambo ya Dr. Aman Walid Kaborou wa Kigoma ambaye naye alibebwa kichifu. CHADEMA wawe makini.
 
Mleta mada ushahabiki usikufanye hadi uwe mvivu wa kufikiri. Unaonyesha hujawahi hata miliki baiskeli. After all, matumizi ya mtu mwingine wewe yanakuhusu nini?
 
FaizaFoxy Elungata Kinjekitile junior Ritz LAKI si pesa wakipata koment yako watakasirika sana

Watu ni wengi ajabu, jamaa kabebwa juu juu...
Watu wanafurahia sana... hakika nimeamini CDM/ Ukawa wana nguvu sana kama mpenda mabadiliko nitakuwa kati ya wale tutaopiga kura ili tuitoe CCM na ikitoka tu nafanya sherehe nyumbani..
Haiwezekani tutawaliwe na mtu miaka 53 hata kama ni ndoa basi tumechoka
 
Last edited by a moderator:
Kwa kheri ccm kwa heri.......
Mola yu nasi Mungu endelea kuipigania chadema
 
Duuu yani watu wanafurahia hii kitu ya mtu kubebwa na kiti kama enzi za utumwa?
 
CHADEMA wamepanga kuandamana kwa bodaboda kutoka Kahama - Tinde - Kahama umbali wa km 150 kwa lengo lisilojulikana, bodaboda nyingi ni nzee zinatumia mafuta litre moja kwa km tatu hivyo kila pikipiki itatumia litre 50 sawa na shs 150,000/= ambazo waendesha bodaboda hawana labda wafadhiliwe na chama.

Itabidi kila pikipiki iwe na dumu mbili za litre 20 kila moja kwani hakuna kituo cha mafuta zaidi ya isaka na kahama na kila pikipiki inauwezo wa kujazwa mafuta litre nane tu.

Pikipiki hizi sio sport na hazina rejeta hivyo huhitaji kupozwa kwa masaa matatu kila inapotembea km 15 kwa hiyo safari hii itachukua siku tatu au nne huku shughuli za kiuchumi zikiwa zimesimama kwa msongamano wa watu na magari, hii itasababisha watoto kuwa katika hatari ya kugongwa na magari hili lilitokea katika uchaguzi mdogo wa Igunga mtoto aligongwa na fuso na kufa palepale.

Kwa mtizamo huu nashindwa kuelewa viongozi wa CHADEMA ni watu wa namna gani, safari hii akifa mtu mbowe lazima uwajibike.
Hizi siasa za kwenye mitndao duh! Kuna watu wanaami n i kila kinachoandikwa hapa hata kama hakiingii akilini!
 
ha ha ha,bavicha kwa maigizo bana....
wale wagombea udiwani wa ukawa kishimba kishawatafutia kazi africa kusini kwenye supermarket zake,wala hata hawagombei,wanazuga tu..

brother unaota ndoto za majinamizi,pole sana brother unatia huruma
 
Watu ni wengi ajabu, jamaa kabebwa juu juu...
Watu wanafurahia sana... hakika nimeamini CDM/ Ukawa wana nguvu sana kama mpenda mabadiliko nitakuwa kati ya wale tutaopiga kura ili tuitoe CCM na ikitoka tu nafanya sherehe nyumbani..
Haiwezekani tutawaliwe na mtu miaka 53 hata kama ni ndoa basi tumechoka

watu wa kahama wamefanya chaguo sahihi kuibwaga ccm mchana kweupe
 
Back
Top Bottom