Duh, kumbe inazingua siku nyingi? Basi watuongezee deadline kama ndiyo hivyo. Haiwezekani kuwa na karibu siku tatu za bila huduma, yet wakomae na deadline yao? Huu si ustaarabu kabisa. Halafu ni bora hata wangetuomba msamaha, sasa wamebaki tu, na wala hawaonyeshi kujali. Ukienda kusoma kwenye vyuo vyao mamboa ya public administration wanakufundisha umhimu wa communication. Hivi hawa wanawezaje kusimamia vyuo vinavyofundisha utawala bora halafu wao wenyewe ni watawala wa hovyo kabisa? Yaani, kwa style hii, wale waombaji waliopo kijijini imekula kwao. Na hii ni style nyingine ya ubaguzi ambao serikali ya CCM na institutions zake imekuwa ikiufanya. Na wanajua kabisa kwamba end of the day anaumia mtoto wa mkulima asiyekuwa na uwezo wa kuaccess internet wakati wote.