TCRA, Tunaomba ufafanuzi


mkunashukuru kwa kuendelea kufafanua swali langu la msingi.naona pasco anahangaika sana kutoa details ambazo hatuhizihitaji kwa sasa.
 
As usual, ntarudi baada ya muda. Ngoja niwatafutie (watoto wangu) king'amuzi kitakachoonyesha ITV vizuri ili waangalie michezo ya kuigiza waipendayo, wananisumbua hamna mfano. King'amuzi nilichonaco ITV hola!
 
nani anayeamua station flani ijiunge na kinga'muzi flani?ni TCRA au Wamiliki wa station husika?
 
Hapo uvivu unakujaje? Hayo matangazo ya TCRA yemsolve nini? hutajakaa madiriko na hata hatuogopi hizo changamoto, elewa issue ni nini siyo unakurupuka just for the sake of it

acha uvivu. inaonyesha hukuwa unafuatilia matangazo ya tcra. changamoto zipo lakini baadhi yetu hatupendi mabadiliko.
 
mkunashukuru kwa kuendelea kufafanua swali langu la msingi.naona pasco anahangaika sana kutoa details ambazo hatuhizihitaji kwa sasa.

Mimi nilinunua tv yenye king'amuzi kama walivyokuwa wamesema mwazoni matokeo yake uki search unapata channel zote lakini hazionyeshi picha wa sauti.
 
Serikali ya JK bana imejaa viongozi wasanii tupu,wengi wao wanatuongoza kama wanavyoziongoza familia zao.
 
nani anayeamua station flani ijiunge na kinga'muzi flani?ni TCRA au Wamiliki wa station husika?
Ukinunua king'amuzi cha kampuni yo yote, free local channels zote unazipata b'cause TCRA wametoa license kwa local providers ikiwa na condition hiyo,
 
usanii mtupu hamna digitali wala nini ni mfumo wa tu wa malipo kwa matangazo ya televisheni umebadilika ila katika ubora wa picha na sauti mambo ni yaleyale,tcra wametufanyia usanii tu.
 
Pasco

nakumbuka awali uliwahi sema ni dereva tax sasa mwandishi sikuelewi mkuu
 
Wanatakiwa wajipange upya... Ghafla kupata habari Tanzani kunageuka kuwa ni bidhaa adimu......

Wanataka tusijue kinachoendelea maana Kila dili la ufisadi hata halija kamilika mshajua
 
startimes nao wanarusha matangazo ya ki-analojia kwa mtindo wa ki-dijitali.
 
startimes nao wanarusha matangazo ya ki-analojia kwa mtindo wa ki-dijitali.
Duuuu!!!Hii kali aisee!!!Mimi nadhani tuwape mwez mmoja kama mambo yenyewe ni magumashi hivi tuingie mtaani tudai haki yetu ya kupata habari,nina wiki mbili hata sijui dunia ikoje tena!!!
 
Habari zenu/

kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania mitambo ya analogia imezimwa mnamo tarehe 31.12.2012 saa 5.59 usiku, kwa kweli ni maendeleo katika technologia, tuna wapongeza sana TCRA kwa hili. lakini pamoja na pongezi hizi nafikiri TCRA hamkuwa mmejiandaa ipasavyo kwani sasa badala watu kuwa wanafurahia mfumo wa DIGITALI imekuwa kero kubwa kwao kulingana na huduma wanazopata

ni kweli TCRA hamuhusiki na kusambaza huduma za digitali nyie ni wasimamizi tu! Kama sijakosea mmetoa leseni kwa Makampuni Matatu, TING, STARTIMES na BASIC TRANSMISION. Na mpaka sasa inaonyesha ni Startimes tu ndio wanaotoa huduma hizo. kwani TING wameshindwa kabisa kusimamia soko lao, na hao BTL mpaka sasa haijulikani itaanza lini

sasa tatizo linakuja kwamba mitambo ya analogia imezimwa wakati kampuni moja tu ya DIGITAL inatoa huduma hizo nchini (startimes), kiasi kwamba kila mwenye TV ili ahamie huko kwa DIGITALI ni lazima anunue king'amuzi cha hao Startimes. SASA JE HAO STARTIMES WAMEWEZA/WANAWEZA KULIMUDU SOKO KWA TANZANIA NZIMA??

Kila kukicha malalamiko mengi kutoka kwa wateja wa STARTIMES kuhusu Ubora wa ving'amuzi vyao, upatikanaji wa ving'amuzi, na pia huduma zao kulalamikiwa kuwa mbovu kupita maelezo. sio hivyo tu Tanzania kwa sasa kuna chanel zaidi ya 25 za television lakini katika king'amuzi cha startimes ni chanel 7 tu za Tanzania zinapatikana ikimaanisha kuna chanel za tanzania ambazo baada ya kuzimwa mfumo wa analogia zimepotea/zimekufa kwani hazipo tena hewani na hazijaingizwa katika king'amuzi cha startimes.

'Gharama' za manunuzi pia hazieleweki kwa hao startimes kwani mara wanakwambia 48000 mara ununue antena, mara 39000, mara 62000 yaani kero tupu. LAKINI KWA KUWA HAKUNA ALTENATIVE YEYOTE YA KUINGIA DIGITALI MPAKA UNUNUE HICHO KING'AMUZI CHAO INABIDI TU WATU WANUNUE HICHO KING'AMUZI pamoja na kwamba matatizo chungu mzima

sasa nauliza kwa nini TCRA msingehakikisha huduma ya digitali inapatikana sehemu zote na kuwe na machaguo tofauti ambayo mteja atakuwa nayo ndio mzime hiyo analogia?

AU TCRA mna-share pale STARTIMES??? kama makampuni hayo mengine TING na BTL wameshindwa kutoa huduma kwa nini mnayakumbatia?

mbona tunakuwa na kiherehere cha kuhamia DIGITALI wakati miundombinu yetu ni BOMU???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…