TCRA naombeni majibu haya kabla ya kuhitaji alama za vidole za kila mmiliki line, je technology ya kisasa imewashinda?

Watanzania lazima tusimame tuseme enough of this nonsense.

Matamko kila kukicha
Mwingine juzi alisema hairuhusiwi kutumia laini mbili za mtandao mmoja

Najiuliza hii security ya namna hiyo ni kwaajili gani?

Najaribu kufikiri nje ya box

Nadhani hii ni kwaawaajili ya kuwatisha watu wasiikosoe serikali mitandaoni kwasababu mitandao imekuwa mwiba mkali sana kwa serikali hasa baada ya kuzuia mikutano ya siasa.

Ikumbukwe kwamba rais alikuwa anatamani mitandao ya kijamii ifungwe..(kwa maoni yangu) hii ni gia nyingine.

Bado kidogo,
Tunakaribia kufika Sudan!

Sent using Jamii Forums mobile app
Inamaana nikitaka kuweka laini kwenye modem ya laptop kudownload movie nisubiri hadi movie iishe kudownload ndio niweze kuirudisha kwenye simu kwa ajili ya kupiga na kupokea simu?
 
1073902





Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema lengo la mfumo mpya wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole linatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wananchi waliosajili laini kwa kutumia vitambulisho feki.



Kuanzia Mei Mosi mwaka huu, wananchi wote wanatakiwa kusajili laini zao kwa mfumo huo, na laini ambazo hazitasajiliwa zitafungiwa pindi tutakapotangaza muda wa ukomo.



“Tunatambua kwa kutumia mfumo huu, itaondoa udanganyifu mkubwa unaosababisha kuwepo kwa ugumu wa TCRA katika kudhibiti vitendo vya uhalifu kwa kutumia mitandao,” amesema Mhandisi Mihayo.



Aidha Mihayo amesema katika mfumo huo wananchi watatakiwa kwenda na kitambulisho cha uraia au namba ya kitambulisho kwa ajili ya kusajili laini zao.



Hayo yamelezwa leo na Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa, Francis Mihayo, wakati wa kuzindua kampeni ya kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mfumo huo mkoani wa Simiyu.
 
Fingerprint is best than anything you know..
MTU anaweza akatumia Simu yako vibaya akidhaniwa Ni wewe but Finger print wakati wakitumia Na njia ulizotaja Ndo halisi Zaidi..
Pia Sio kwa matumizi ya Simu tu serikali wanaweza tumia kuingiza kwenye mfumo (Data Base)
Hivyo kuweza kusaidia Hata kwenye uhalifu and Alike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TCRA KUWENI OPEN KIDOGO

KUNA TATIZO LA UELEWA HAPA MFANO MTALII AMESHUKA PALE AIRPORT ANAWEZA KUSAJILI SIMCARD KWA FINGER PRINT ONLY
 
Watanzania kwa kulalamika, tunaongoza duniani. Hata wangesema, kuanzia sasa hakuna kusajili line, unanunua na kutumia hapo hapo, tungelalamika. Kwa taarifa yako, kusajili line kwa finger print hakujaanza Leo, huu mwaka wa pili sasa na wananchi washaelewa. Makampuni ya simu wanao mawakala walioanza kusajili line kwa mfumo huo toka kitambo. Unga mkono juhudi, tusonge mbele. Tengeneza makala kuonesha faida za finger print badala ya kulalamika, Huu ni ujenzi was Tanzania mpya, utapata stress bure kupinga pinga maendeleo
M
Siyo kila kitu lazima uchangie, Mawakala wanaohusika kusajili line wanatumia Simu tena android phonea na deaigned apps za kusajilo simu karibu mitamdao yote nazifahamu/nishaziona maana wapo watu ninaofahamiana nao since wayback wanasajili line so hiyo finger print wanascan kupitia nini?

Anyway jina lako tuu lina sadifu yaliyomo akilini.

Kataa kubali kwa hili serikali/TCRA wamebugi maana nida hawajatoa vitambulisho kwa Raia nadiriki kusema vitambulisho ambavyo vimetolewa mpaka sasa ni vichache mno yaani mno, tena vingi vina errors za kutosha , .
Kuna watu Ni ME ila Kwenye National Identity Zao Inasomeka KE kama kuna watu kumi wamepata hizo errors Ni wangapi watakuwa nazo mpaka Wananchi wote wapatiwe Vitambulisho.

Kwa kuhitimisha Ni wananchi wachache sana waliojiandikisha na kujaza Fomu za kuchukua hivyo vitambulisho, .So hiyo kitu ni ndoto kukamilika au Kuna mpango wa kupigwa hapo .

Serikali itoe vipaumbele kwa mambo ambayo ni threat kwa wananchi kwanza mengine baadae , ............

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikawaida fingerprint ni utaratibu unaotumiwa polisi kuwatambua wahalifu, ina maana watanzania wote wanatakiwa kufanyiwa surveillance kama watu waliokwisha kufanya matukio ya kihalifu!? kwa hili wengi tutafungiwa laini zetu
 
Hellow watu wa Mungu, salam..

TCRA wamenishangaza sana, wanataka alama za vidole kwa kila mmiliki wa line ya simu.. Nimejiuliza maswali mengi mno sijapata jibu sbb sioni sbb yoyote ya msingi kufanya hivyo ukilinganisha na technology ya kisasa iliyopo.. Let's get down to details kwanini nawashangaa

1: Ukimiliki simu, TCRA wanajua line yako, simu yako, na IMEI ya simu yako..

2. Hata ukibadili line katika simu nyingine, ukawasha, still wanajua, unatumia simu gani, IMEI ipi, uko wapi at present position etc

3. Ukiamua, utumie mtandao kwa line yako, still TCRA wanajua IP address yako, uko wapi and a precise location..

4: Simu unazopiga, kuingia, sms, data usage, etc etc wanazo, hata utumie line mpya lakini haina jina still watapata details zote hizo..

Swali rahisi kabisa, je alama ya vidole ndio security sign kubwa zaidi kuliko hizo correct digital details kama ni security mnahitaji? The answer is BIG NO definitely..

Je, alama ya vidole nchi nzima, let's say only 40% wenye line wamejiweza wakaenda, 60% hawajaweza, na mkawafungia tuseme, serikali hawaoni watapoteza matrilioni ya shilingi kwa kuwapoteza hawa ambao hawajaenda kutoa alama ya vidole..?

Swali la mwisho na kubwa kabisa lenye kikwazo haswa, ukisema mwananchi aende na IDs za NIDA wengi hawana, IDs za Mpiga kura wengi hawana na wenye umri wa 18 and below hawana, ID za shule labda sekondari hapo wanazo ila akimaliza tu shule wanaacha so hizo hazifai, hili tu la IDs watapoteza wateja mamilioni, hii ina maana serikali itapoteza matrilioni ya shilingi kwa kupoteza wateja wengi mnooooo

Kama issue ni security, finger print sio realible these days, njia za kisasa za kidigitali nilizotaja hapo juu ndio very correct one and world wide are using..!!

Sijaelewa TCRA wamekaa na kujadili hasara kubwa itakayojitokeza sbb tu ya kutafuta finger prints za watu... Nimeshangaa sana. Siku hizi kumkamata mhalifu finger prints is nothing, just unatakiwa kujua line yake tu, basii. TCRA, msaidieni mh Rais wetu, apate mapato ya kutosha, hizi ideas zenu za kuja kuleta hasara kubwa unreasonably acheni.
Hata mimi haya maswali nilikuwa nayo...tunaenda mbele au nyuma
 
Kikawaida fingerprint ni utaratibu unaotumiwa polisi kuwatambua wahalifu, ina maana watanzania wote wanatakiwa kufanyiwa surveillance kama watu waliokwisha kufanya matukio ya kihalifu!? kwa hili wengi tutafungiwa laini zetu
JE WEWE MHALIFU
 
Mtoa mada una hoja nzuri sana ..... INTEGRATION ya hizi system automatically ingefaa zaidi kuliko sisi wananchi kupoteza muda mwingi kwenye foleni

Yaani kwa kuwa ID ya NIDA ina fingerprint zetu na zimehifadhiwa kwenye kanzidata(database) basi ni rahisi kuzihamishia kwenye mfumo wao hao TCRA... yaani akiingiza namba yangu ya kitambulisho mfano 19900101-5897569-123456 inaleta details zote na hizo alama za vidole, kwa hiyo ni kitendo cha kuzihamishia hizo taarifa kwenye profile mpya ya TCRA as SIMPLE as that..


SEMA SASA SIJUI WATANZANIA TUNAKWAMA WAPI?
 
Nimeenda kusajiri line wakachukua saini yangu, wakapiga picha yangu passport size, copies za IDs zangu

Alafu naona sms kuwa niende tena kusajiri upya
Kiukweli SITAENDA wacha wafunge tu line

NIDA walichukua alama za vidole
NEC walichukua alama za vidole
bado TCRA nao tena?

Kwani alama za vidole huwa zina tabia ya kubadilika baada ya muda?

Hawawezi kuchua kutoka kwa wenzao NEC, NIDA?

Alama za vidole ni unique
kila mtu na zake dunia nzima!

sasa zimewachanganya?
Hapa kwa kweli kila mtu ana mwisho wa uvumilivu wake


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
IKUMBUKWE 2016 MAKAMPUNI YA SIMU YALITOZWA FAINI YA MAMILIONI KWA USAJILI MBAYA


Kampuni zilizotozwa faini hiyo na kiwango kikiwa kwenye mabano ni Airtel (Sh1.08 bilioni), Smart (Sh1.3 bilioni), Vodacom (Sh945 milioni), Zantel (Sh105 milioni) na Halotel (Sh1.6 bilioni).
 
Mkuu hutaki kutambuliwa? Fingerprints ni kwa ajili ya kukutambua in relation to that Simcard. Bado fingerprints zinatumika nchini mwetu kumtambua mtu hata huko ulaya bado wanawatambua raia wao kwa njia ya fingerprints na DNA. Acha waanze kwanza kututambua kwa fingerprints. We need to start from somewhere mkuu!

Huko Ulaya wanawatambua kwenye nini na nini kuhitaji hizo fingerprints?
 
Back
Top Bottom