TCRA naombeni majibu haya kabla ya kuhitaji alama za vidole za kila mmiliki line, je technology ya kisasa imewashinda?

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
16,850
16,747
Hellow watu wa Mungu, salam..

TCRA wamenishangaza sana, wanataka alama za vidole kwa kila mmiliki wa line ya simu.. Nimejiuliza maswali mengi mno sijapata jibu sababu sioni sababu yoyote ya msingi kufanya hivyo ukilinganisha na technology ya kisasa iliyopo.. Let's get down to details kwanini nawashangaa

1: Ukimiliki simu, TCRA wanajua line yako, simu yako, na IMEI ya simu yako..

2. Hata ukibadili line katika simu nyingine, ukawasha, still wanajua, unatumia simu gani, IMEI ipi, uko wapi at present position etc

3. Ukiamua, utumie mtandao kwa line yako, still TCRA wanajua IP address yako, uko wapi and a precise location.

4: Simu unazopiga, kuingia, sms, data usage, etc etc wanazo, hata utumie line mpya lakini haina jina still watapata details zote hizo..

5: Utaratibu wa sasa wa kusajili line mpya, unapigwa picha iliyo clear kabisa na ku upload ktk system, kisha kitambulisho ulichosajilia line kinapigwa picha na inaingizwa ktk system ya kampuni ya simu husika, na majibu yanarudi instantly, kuwa picha na kitambulisho vimekubalika, je picha ya passport size ya mmiliki wa line si zaidi ya finger print.

Swali rahisi kabisa, je alama ya vidole ndio security sign kubwa zaidi kuliko hizo correct digital details kama ni security mnahitaji? The answer is BIG NO definitely..

Je, alama ya vidole nchi nzima, let's say only 40% wenye line wamejiweza wakaenda, 60% hawajaweza, na mkawafungia tuseme, Serikali hawaoni watapoteza matrilioni ya shilingi kwa kuwapoteza hawa ambao hawajaenda kutoa alama ya vidole..?

Swali la mwisho na kubwa kabisa lenye kikwazo haswa, ukisema mwananchi aende na IDs za NIDA wengi hawana, IDs za Mpiga kura wengi hawana na wenye umri wa 18 and below hawana, ID za shule labda sekondari hapo wanazo ila akimaliza tu shule wanaacha so hizo hazifai, hili tu la IDs watapoteza wateja mamilioni, hii ina maana serikali itapoteza matrilioni ya shilingi kwa kupoteza wateja wengi mnooooo

Kama issue ni security, finger print sio realible these days, njia za kisasa za kidigitali nilizotaja hapo juu ndio very correct one and world wide are using..!!

Sijaelewa TCRA wamekaa na kujadili hasara kubwa itakayojitokeza sbb tu ya kutafuta finger prints za watu... Nimeshangaa sana. Siku hizi kumkamata mhalifu finger prints is nothing, just unatakiwa kujua line yake tu, basii. TCRA, msaidieni mh Rais wetu, apate mapato ya kutosha, hizi ideas zenu za kuja kuleta hasara kubwa unreasonably acheni. TCRA tayari mna TTMS, inawapatia kila kitu at your finger tips. Ukianzisha project hasa kama hii ya finger print nchi nzima lazima ufikiri mara elfu na elfu, big question is, DOES IT REALLY WORTH THE INVESTMENT? You can rethink again, mtapoteza trillions kwa maamuzi yasiyo na umuhimu mkubwa..!! Ni ushauri tu

👏👆 Asante Mh. Rais wetu, atleast umesikia kilio cha wanyonge
 
JE KUMEFANYIKA TATHIMINI YA KUTOSHA AU MATAMKO YA MVUA

NAJUA KUNA FAIDA LAKINI TUANGALIE HASARA ZIFUATAZO

1.MAPATO KUSHUKA –hapa ni kwamba sasa hakutakuwa na wageni kutumia mawasiliano ya simu za mkononi,awali passport hasa pale airport zilitumika sasa ununuzi wa vocha kushuka

2.MAWAKALA KUKOSA KAZI –hili zoezi linafanyika kwa simu maalumu na mawakala wote hawana hizi simu unategemea hao mawakala watakula nini,BOMU la MAJOBLESS linaibuka .

3. ZOEZI LIMEKUJA KAMA MVUA YA VULI- hapa nakumbuka maamuzi ya mwakyembe kutaka ndoa zifungwe kwa kutumia cheti cha kuzaliwa wakati hata yeye hakuwa nacho kwa wakati huo.

4. HAKUNA ANALYSIS YA KUTOSHA KWA NINI WATU HAWANA VITAMBULISHO-hapa nashanga kwa nini hivi vitambulisho mtu asiletewe mtaani kwake ofisi za serikali za mitaa itarahisisha mpaka vijijini kule kwenye nyumba za tope.

5.WATEJA KUTOELEWA NINI NI NINI-hapa tutegemee queue ya nguvu katika callcentre za makampuni ya simu ,wateja wengi watapiga simu kuuliza maswali

:rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes:

6.SIM CARD KUUZWA BEI ZA JUU-hapa itatokea watu kusajiri sim card na kuuza kwa bei kubwa kwa sababu demand yaani soko litakuwa kubwa na kitakacho tokea ni yaleyale watu kutumia simcard siyo yake

7.HUDUMA ZA MPESA,TIGOPEA KUPUNGUA-hapa wateja wataanza kutoa fedha zao kwenye simu kwa kuhofia kufungiwa simcard zao, huduma za simBanking zitapungua na serikali kukosa kodi zinazotokana na miamala ya electronic money transfer na pay bill mbalimbali .
 
Mkuu hutaki kutambuliwa? Fingerprints ni kwa ajili ya kukutambua in relation to that Simcard. Bado fingerprints zinatumika nchini mwetu kumtambua mtu hata huko ulaya bado wanawatambua raia wao kwa njia ya fingerprints na DNA. Acha waanze kwanza kututambua kwa fingerprints. We need to start from somewhere mkuu!
 
JE KUMEFANYIKA TATHIMINI YA KUTOSHA AU MATAMKO YA MVUA

NAJUA KUNA FAIDA LAKINI TUANGALIE HASARA ZIFUATAZO

1.MAPATO KUSHUKA –hapa ni kwamba sasa hakutakuwa na wageni kutumia mawasiliano ya simu za mkononi na ununuzi wa vocha kushuka

2.MAWAKALA KUKOSA KAZI –hili zoezi linafanyika kwa simu maalumu na mawakala wote hawana hizi simu unategemea hao mawakala watakula nini,BOMU la MAJOBLESS linaibuka .

3. ZOEZI LIMEKUJA KAMA MVUA YA VULI- hapa nakumbuka maamuzi ya mwakyembe kutaka ndoa zifungwe kwa kutumia cheti cha kuzaliwa wakati hata yeye hakuwa nacho kwa wakati huo.

4. HAKUNA ANALYSIS YA KUTOSHA KWA NINI WATU HAWANA VITAMBULISHO-hapa nashanga kwa nini hivi vitambulisho mtu asiletewe mtaani kwake ofisi za serikali za mitaa itarahisisha mpaka vijijini kule kwenye nyumba za tope.

5.WATEJA KUTOELEWA NINI NI NINI-hapa tutegemee queue ya nguvu katika callcentre za makampuni ya simu ,wateja wengi watapiga simu kuuliza maswali

6.SIM CARD KUUZWA BEI ZA JUU-hapa itatokea watu kusajiri sim card na kuuza kwa bei kubwa kwa sababu demand yaani soko litakuwa kubwa na kitakacho tokea ni yaleyale watu kutumia simcard siyo yake
Hiyo # 2 nmekuelewa zaidi

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshangaa Sana Tunatia Aibu kuwa nyuma kwa Technology😁😁😁yaani miaka hi ya kupoteza Muda kukaa foleni eti usubiri kuchukuliwa fingerprint
Wakati tulisha poteza Muda wakati wa vitambulisho vya NIDA,😁😁 Na Tunajua ID hizo ndizo zenye taarifa zote Hadi fingerprint😊😊😊😊 dah Kweli TCRA Mambo yenu yajayo Yanasikitisha 😎
 
Watanzania lazima tusimame tuseme enough of this nonsense.

Matamko kila kukicha
Mwingine juzi alisema hairuhusiwi kutumia laini mbili za mtandao mmoja

Najiuliza hii security ya namna hiyo ni kwaajili gani?

Najaribu kufikiri nje ya box

Nadhani hii ni kwaawaajili ya kuwatisha watu wasiikosoe serikali mitandaoni kwasababu mitandao imekuwa mwiba mkali sana kwa serikali hasa baada ya kuzuia mikutano ya siasa.

Ikumbukwe kwamba rais alikuwa anatamani mitandao ya kijamii ifungwe..(kwa maoni yangu) hii ni gia nyingine.

Bado kidogo,
Tunakaribia kufika Sudan!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hutaki kutambuliwa? Fingerprints ni kwa ajili ya kukutambua in relation to that Simcard. Bado fingerprints zinatumika nchini mwetu kumtambua mtu hata huko ulaya bado wanawatambua raia wao kwa njia ya fingerprints na DNA. Acha waanze kwanza kututambua kwa fingerprints. We need to start from somewhere mkuu!
Mkuu tatizo la Tanzania ni kutokuwa na mipango, malengo na mikakati. Na hii inasabishwa na wanasiasa kuwa ndiyo waongoza kila kitu. Wanajivika kila utaalam. Kinachotakiwa kufanyika Tanzania ni hiki: Wahakikishe kila raia ana kitambulisho chenye data zake kama jina lake, jinsia, tarehe ya kuzaliwa, finger print nk.... Kwenye kila kitambulisho iwepo namba ya kumtambulisha mhusika na vyote viwekwe kwenye database. Sasa ukishakuwa na data hizo vitu vingine kama huu usajili wa SIM card nk nk vinakuwa rahisi kusajili kwa kutumia kitambulisho tu... ambacho ndicho chenye data zote za mhusika. Hata kwenye kutoa passport kazi haitakuwa tena kubwa kwani watatumia kitambulisho kutoa passport. Kwa kifupi vitu vingine vyoooote vitakuwa vina depend kwenye kitambulisho.
 
Unaonaje wakianza sasa na wale ambao tayari wana NIDA ID?
 
Cha ajabu kwenye requirement za ID wanataka tutumie national ID ambako tayari kuna fingerprints zetu. Why wasifanye integration ya hizo systems mbili. Why kuwe na duplicate fingerprints TCRA na NIDA?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio utajua kuna watu walienda shule kukua na wengine kusoma. Kupotezeana muda tu na hela

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom