namba ya NIDA kutumika kusajili line nyingi bila muhusika kujua kinachoendelea.

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
7,325
9,186
HABARINI ZA WEEKEND WA NDUGU!

TCRA mnipe ufafanuzi inakuwaje namba ya NIDA nimeihangaikia kwa kupanga lifoleeeeni kubwa na kutumia ma finger print yangu hadi picha mkanipiga ili nipate kitambulisho kwaajili ya matumizi yangu binafsi. kwa jinsi mlivyotuelimisha zile finger print ni kama password ya mhusika hawezi kutumia mtu mwingine kitambulisho chako (kwa uelewa nilioupata),,,,.

swali inakuwaje NIDA yangu inatumika pasi na mimi kujua?

haya wakala (msajili line) alibaki na namba yangu ya NIDA kwa uhuni wake akasajilia watu bila kujua je! mlimuacept vipi wakati alipoweka dole lake asajili laini zile fingerprint haziendani na mwenye NIDA?

wahusika mje mnijibu haya maswali haiwezekani mtuchezee akili kusajili line nyingi kwa NIDA ya mtu bila kujua wakati kuna fingerprint.
la sivyo haya matamko yenu ya shuruti tutakuwa tunayapuuza ikiwemo sensa hamna maana yoyote ni danganya danganya na janja janja nyingi....

NB: mnaouliza nimejuaje bonyeza *106# kujua NIDA yako imetumikaje.
 
Finger print yako walipata wapi? Wewe wakala kakuona zoba akakwambia urudie kuweka kidole mara nyingi kumbe anasajili laini nyingi.
mkuu labda kipindi cha kurasimisha line mtandao ulikuwaga shida maana wengi ndio walikuwa wanasajili pale nakumbuka ndio nilirudia kama mara mbili nayo ni baada ya kuonekana haija aceptiwa kutokana na mtandao
 
Anapokusajilia line anakwambia Network inasumbua rudia kuweka Finger Print,utarudia kuweka Finger Print hata mara 3 au 5 ndio anakwambia imekubali,kumbe zile mara nyingine zote alizokuwa anakwambia inakataa ilikuwa inakubali vizuri tu,kisha hizo line anaenda kuziuza
nafanyaje sasa kwa ungese wa huyu wakala hata sizani kama namkumbuka maana ni mda ila leo tu msg zilinichosha za kusajili kwa alama za vidole au ni bonyeze no hiyo kujua km tyr ile nacheki nakuta kuna mi namba,mingine kibao tyr ipo huku sijui.
 
Finger print yako walipata wapi? Wewe wakala kakuona zoba akakwambia urudie kuweka kidole mara nyingi kumbe anasajili laini nyingi.
Mkuu usiwe mjinga kiasi hicho kuna kipindi kwenye application ya usajili ya VODA ilikuwa imewekewa udhaifu uliowawezesha vijana wa kusajili kuhifadhi fingerprint yako hata kwa zaidi ya siku 7 sijui kama wamesishairekebisha kiufupi kampuni hasa vodacom wanaweka mazingira wezeshi kwa mafreelensa kufanya udanganyifu
 
nafanyaje sasa kwa ungese wa huyu wakala hata sizani kama namkumbuka maana ni mda ila leo tu msg zilinichosha za kusajili kwa alama za vidole au ni bonyeze no hiyo kujua km tyr ile nacheki nakuta kuna mi namba,mingine kibao tyr ipo huku sijui.
unaweza kuzifungia hizo no nyingne, angalia hapo hapo ulipozipatia utaona option ya kuzifutia usajiri
 
Mkuu usiwe mjinga kiasi hicho kuna kipindi kwenye application ya usajili ya VODA ilikuwa imewekewa udhaifu uliowawezesha vijana wa kusajili kuhifadhi fingerprint yako hata kwa zaidi ya siku 7 sijui kama wamesishairekebisha kiufupi kampuni hasa vodacom wanaweka mazingira wezeshi kwa mafreelensa kufanya udanganyifu
asante shahidi maana nilishatunukiwa jina la UZOBA
 
k

wakweli waje waseme maana hapa na wale wazee wa tuma hela wanatuchezea kwa mtindo huu bila,kujua halaf unakuta NIDA yako inachapishwa gazetini na licha yako kuwa we ni tapeli wa TUMA HELA kupitia no hii.
Najiuliza mno, wale wazee wa tuma kwenye namba hii, huwa wanapata wapi namba zetu? Mamlaka husika zimeshindwa kabsa kudhibiti hili
 
nahisi ni wao,,,, baada ya kuliona hili la kutumiwa NIDA Bila kujua hapa nimeamini ni wao TCRA ndo wazee wa TUMA HELA

la sivo waje wajibu kwa vitendo namna ya kudhibiti uhuni uhuni na janjajanja za hovyo.
 
Anapokusajilia line anakwambia Network inasumbua rudia kuweka Finger Print,utarudia kuweka Finger Print hata mara 3 au 5 ndio anakwambia imekubali,kumbe zile mara nyingine zote alizokuwa anakwambia inakataa ilikuwa inakubali vizuri tu,kisha hizo line anaenda kuziuza
... ni suala la taasisi na makampuni kuwa wabunifu tu! Katika namba zote zilizosajiliwa kwa the same finger print lazima kuna at least mojawapo itakuwa ya mhusika sahihi. Makampuni na TCRA wanashindwa nini ku-scan namba zote zenye usajili wa fingerprints moja na kutuma ujumbe wa kuonekana multiple fingerprints kwa namba hizo?

Then kumtaka mhusika kufika ofisi zao au kitengo maalumu cha polisi kuthibitisha? Then wakala aliyehusika na usajili akakamatwa na kushtakiwa? Mbona rahisi tu kukomesha huu ujinga? Tatizo nchi ya vilaza hii; ya wananchi na watendaji wasiopenda kuumiza ubongo ila kulalamika hawajambo.

Alternatively, kutoa option kwa kila mwenye namba iliyosajiliwa, kutuma ujumbe fulani wa kusaidia kucheki namba ambazo zimesajiliwa kwa fingerprints zake. Kama kuna ambayo haitambui, atoe taarifa kwa hatua zaidi. Mbona ni very easy? Tunalalamika kwa vitu vidogodogo ambavyo viko ndani ya uwezo wetu? Hilo nalo tunahitaji msaada kutoka nje kulikomesha?
 
Ukisajili mitaani hiyo ndiyo shida ?

Issue yoyote ya usajili we nenda kwenye ofisi zao kuu

Hivi unajua watu wananunua info za NIDA(matumizi ya mjinimjini)

Ova
 
... ni suala la taasisi na makampuni kuwa wabunifu tu! Katika namba zote zilizosajiliwa kwa the same finger print lazima kuna at least mojawapo itakuwa ya mhusika sahihi. Makampuni na TCRA wanashindwa nini ku-scan namba zote zenye usajili wa fingerprints moja na kutuma ujumbe wa kuonekana multiple fingerprints kwa namba hizo?

Then kumtaka mhusika kufika ofisi zao au kitengo maalumu cha polisi kuthibitisha? Then wakala aliyehusika na usajili akakamatwa na kushtakiwa? Mbona rahisi tu kukomesha huu ujinga? Tatizo nchi ya vilaza hii; ya wananchi na watendaji wasiopenda kuumiza ubongo ila kulalamika hawajambo.

Alternatively, kutoa option kwa kila mwenye namba iliyosajiliwa, kutuma ujumbe fulani wa kusaidia kucheki namba ambazo zimesajiliwa kwa fingerprints zake. Kama kuna ambayo haitambui, atoe taarifa kwa hatua zaidi. Mbona ni very easy? Tunalalamika kwa vitu vidogodogo ambavyo viko ndani ya uwezo wetu? Hilo nalo tunahitaji msaada kutoka nje kulikomesha?
sahihi mkuu,, mbona wameweza swala kuweka vocha iliyotumika unatumiwa ujumbe tayari imetumika sasa we mtu tyr ana line na keshaisajili anatokea mwingine aina ya,line ileile anasajiliwa kwanini wasiseme imeshatumika?

matamshi yao ya kibabe na vitisho utendaji ZERO.
 
Back
Top Bottom