TCRA naombeni majibu haya kabla ya kuhitaji alama za vidole za kila mmiliki line, je technology ya kisasa imewashinda?

waweze kupata wezi vizuri ukihiiba tu wanacheki finger print
Hellow watu wa Mungu, salam..

TCRA wamenishangaza sana, wanataka alama za vidole kwa kila mmiliki wa line ya simu.. Nimejiuliza maswali mengi mno sijapata jibu sbb sioni sbb yoyote ya msingi kufanya hivyo ukilinganisha na technology ya kisasa iliyopo.. Let's get down to details kwanini nawashangaa

1: Ukimiliki simu, TCRA wanajua line yako, simu yako, na IMEI ya simu yako..

2. Hata ukibadili line katika simu nyingine, ukawasha, still wanajua, unatumia simu gani, IMEI ipi, uko wapi at present position etc

3. Ukiamua, utumie mtandao kwa line yako, still TCRA wanajua IP address yako, uko wapi and a precise location..

4: Simu unazopiga, kuingia, sms, data usage, etc etc wanazo, hata utumie line mpya lakini haina jina still watapata details zote hizo..

Swali rahisi kabisa, je alama ya vidole ndio security sign kubwa zaidi kuliko hizo correct digital details kama ni security mnahitaji? The answer is BIG NO definitely..

Je, alama ya vidole nchi nzima, let's say only 40% wenye line wamejiweza wakaenda, 60% hawajaweza, na mkawafungia tuseme, serikali hawaoni watapoteza matrilioni ya shilingi kwa kuwapoteza hawa ambao hawajaenda kutoa alama ya vidole..?

Swali la mwisho na kubwa kabisa lenye kikwazo haswa, ukisema mwananchi aende na IDs za NIDA wengi hawana, IDs za Mpiga kura wengi hawana na wenye umri wa 18 and below hawana, ID za shule labda sekondari hapo wanazo ila akimaliza tu shule wanaacha so hizo hazifai, hili tu la IDs watapoteza wateja mamilioni, hii ina maana serikali itapoteza matrilioni ya shilingi kwa kupoteza wateja wengi mnooooo

Kama issue ni security, finger print sio realible these days, njia za kisasa za kidigitali nilizotaja hapo juu ndio very correct one and world wide are using..!!

Sijaelewa TCRA wamekaa na kujadili hasara kubwa itakayojitokeza sbb tu ya kutafuta finger prints za watu... Nimeshangaa sana. Siku hizi kumkamata mhalifu finger prints is nothing, just unatakiwa kujua line yake tu, basii. TCRA, msaidieni mh Rais wetu, apate mapato ya kutosha, hizi ideas zenu za kuja kuleta hasara kubwa unreasonably acheni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabu yote ni vile hakuna national database...

Passport lazima uache finger prints, kwa national ID zoezi ni hilo hilo, sasa imehamia usajili wa simu, si ajabu ikaenda kwa mabenki na kwingineko...

Lets have kitu kama social security number, unatambuliwa na serikali pindi tu unazaliwa na vitu vingine vyote vina centralize hapo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaonaje wakianza sasa na wale ambao tayari wana NIDA ID?
Zoezi la vitambulisho linatakiwa limalizike ili kila mtu awe na ID. Vinginevyo ni kuwafanya watu wahangaike. Wangekaza misulu kwenye utoaji wa vitambulisho ili kila raia afikiwe.
 
Huu ni usumbufu tuu kwa watu.
Ila ni kamradi kwa wale mawakala maana ata sajili watu wote.....kila mmoja ikiwa buku huku tu.... ni noti ya kutosha.
 
Guys reduce some of these things which could be done when one is doing registration with government authorities.
Tumeenda NIDA.... Tume ya uchaguzi... TRA. Mnaturudisha tena kwenye foleni za line za simu.
How does some of these things work? No one package for all the rest? Tunarudi sana kwenye foleni bila sababu za msingi
 
Watanzania kwa kulalamika, tunaongoza duniani. Hata wangesema, kuanzia sasa hakuna kusajili line, unanunua na kutumia hapo hapo, tungelalamika. Kwa taarifa yako, kusajili line kwa finger print hakujaanza Leo, huu mwaka wa pili sasa na wananchi washaelewa. Makampuni ya simu wanao mawakala walioanza kusajili line kwa mfumo huo toka kitambo. Unga mkono juhudi, tusonge mbele. Tengeneza makala kuonesha faida za finger print badala ya kulalamika, Huu ni ujenzi was Tanzania mpya, utapata stress bure kupinga pinga maendeleo
Hellow watu wa Mungu, salam..

TCRA wamenishangaza sana, wanataka alama za vidole kwa kila mmiliki wa line ya simu.. Nimejiuliza maswali mengi mno sijapata jibu sbb sioni sbb yoyote ya msingi kufanya hivyo ukilinganisha na technology ya kisasa iliyopo.. Let's get down to details kwanini nawashangaa

1: Ukimiliki simu, TCRA wanajua line yako, simu yako, na IMEI ya simu yako..

2. Hata ukibadili line katika simu nyingine, ukawasha, still wanajua, unatumia simu gani, IMEI ipi, uko wapi at present position etc

3. Ukiamua, utumie mtandao kwa line yako, still TCRA wanajua IP address yako, uko wapi and a precise location..

4: Simu unazopiga, kuingia, sms, data usage, etc etc wanazo, hata utumie line mpya lakini haina jina still watapata details zote hizo..

Swali rahisi kabisa, je alama ya vidole ndio security sign kubwa zaidi kuliko hizo correct digital details kama ni security mnahitaji? The answer is BIG NO definitely..

Je, alama ya vidole nchi nzima, let's say only 40% wenye line wamejiweza wakaenda, 60% hawajaweza, na mkawafungia tuseme, serikali hawaoni watapoteza matrilioni ya shilingi kwa kuwapoteza hawa ambao hawajaenda kutoa alama ya vidole..?

Swali la mwisho na kubwa kabisa lenye kikwazo haswa, ukisema mwananchi aende na IDs za NIDA wengi hawana, IDs za Mpiga kura wengi hawana na wenye umri wa 18 and below hawana, ID za shule labda sekondari hapo wanazo ila akimaliza tu shule wanaacha so hizo hazifai, hili tu la IDs watapoteza wateja mamilioni, hii ina maana serikali itapoteza matrilioni ya shilingi kwa kupoteza wateja wengi mnooooo

Kama issue ni security, finger print sio realible these days, njia za kisasa za kidigitali nilizotaja hapo juu ndio very correct one and world wide are using..!!

Sijaelewa TCRA wamekaa na kujadili hasara kubwa itakayojitokeza sbb tu ya kutafuta finger prints za watu... Nimeshangaa sana. Siku hizi kumkamata mhalifu finger prints is nothing, just unatakiwa kujua line yake tu, basii. TCRA, msaidieni mh Rais wetu, apate mapato ya kutosha, hizi ideas zenu za kuja kuleta hasara kubwa unreasonably acheni.
M
 
Watanzania kwa kulalamika, tunaongoza duniani. Hata wangesema, kuanzia sasa hakuna kusajili line, unanunua na kutumia hapo hapo, tungelalamika. Kwa taarifa yako, kusajili line kwa finger print hakujaanza Leo, huu mwaka wa pili sasa na wananchi washaelewa. Makampuni ya simu wanao mawakala walioanza kusajili line kwa mfumo huo toka kitambo. Unga mkono juhudi, tusonge mbele. Tengeneza makala kuonesha faida za finger print badala ya kulalamika, Huu ni ujenzi was Tanzania mpya, utapata stress bure kupinga pinga maendeleo
M
:(:(:(:oops::oops::oops::oops::oops::oops::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes:
 
Siyo kila mwenye SIM card ana hicho kitambulisho cha taifa. Really makes no sense
 
Hili zoezi liwe jepesi kwa nini wasingekuja na technology ambayo mtumiaji wa simu ..anatumia website or apps kumaliza mambo yote

Kama finger print za simu imewezekana wao kwa nini washindwe..maana kuna watu simu zao hazi support fingerprint but unakuta ka download apps inayo support, kitu ingekuwa easy before ata may1

If it isn’t perfect ,it’s not good enough
 
Fikiria kama TCRA pia.

Hili zoezi ni endelevu na hawajatangaza ukomo bali mwanzo.

Hakuna kampuni itakayopoteza wateja maadam ukamilishapo vigezo ikiwa ni pamoja na kupatiwa kitambulisho cha TAIFA nenda kakamilishe usajili.

Kwa wenye vitambulisho hivyo waanze kusajili upya laini zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshangaa Sana Tunatia Aibu kuwa nyuma kwa Technology😁😁😁yaani miaka hi ya kupoteza Muda kukaa foleni eti usubiri kuchukuliwa fingerprint
Wakati tulisha poteza Muda wakati wa vitambulisho vya NIDA,😁😁 Na Tunajua ID hizo ndizo zenye taarifa zote Hadi fingerprint😊😊😊😊 dah Kweli TCRA Mambo yenu yajayo Yanasikitisha 😎
TCRA kama wameshindwa kufanya kazi na taasisi zingine kama NIDA wakamtafute yule jamaa wa SAUZI aliyehack akaunti ye serikali nakujilipa mshahara kwa mwaka mzima. TCRA mnakwama wapi hadi mnatia aibu
 
Kinachotokea kila kampuni ya simu itakuwa na database ya fingerprints zake maana wengine tuna line karibu tano kila moja na kazi zake inamaana itakulazimu kupita maduka yote kuchukua fingerprints jambo linaloonyesha hii mifumo wala itakuwa haifanyi integration na TCRA ilihali wangeweza tumia data base ya finger prints ambazo NIDA wanazo sema ambacho wananchi tungepaswa ni kwenda kufanya uthibitisho kwa kuonyesha namba au ID ya NIDA ambapo kwa kutumia portal iliyounganishwa NIDA wangeweza kupata taarifa zote za mmiliki wa simu hapo ingekuwa more secure kuliko hii kila kampuni ukachukuliwe finger prints.

Mfano line ya TTCL me ntaipotezea tu hata wakiifunga ikwende tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom