TCRA: Usikubali kuingiza Alama za Vidole mara mbili wakati wa kusajili Line

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeeleza wahalifu wa mitandao ya simu maarufu kama 'Tuma kwa namba hii' wanavyosajili laini kinyemela kwa kutumia vitambulisho na alama za vidole vya watu, bila wahusika kugundua.

Imesema uhalifu huo hufanywa na mawakala wanaosajili laini za simu mteja anapokwenda kujisajili akiwa na kitambulisho kwa kumtaka kuweka alama za vidole kwenye mashine zaidi ya mara moja kwa kisingizio alama haijasoma.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Bidhaa za Mawasiliano TCRA, Thadayo Ringo, alibainisha udanganyifu huo juzi wakati akitoa mafunzo ya kuzijengea uwezo wa kukabiliana na makosa ya mitandaoni Kamati za Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano za mikoa kupitia Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA- CCC).

"Ukienda kusajili laini ukiona umechukuliwa alama za vidole, akaendelea kuingiza taarifa akarudi kukuambia tena alama hazijakubali rudia tena usikubali, anatumia taarifa zako kusajili laini zaidi ya moja na kuwapatia wahalifu," alisema Thadayo.

Alisema wahalifu wa mitandao wamekuwa wakiibuka na mbinu mpya kila mara na TCRA huchunguza na kuzibaini kuhakikisha wanadhibiti uhalifu.
 
Ni swala la programming
Mtu asiruhusiwe sajili laini zaidi ya moja ndani ya miezi 6, wakifanya hivi hata hao wasajili watashindwa.

Renew iwe na taratibu nyingi

Namba ya mtu iwe yake maisha yote kama TIN.
Akitaka namba mpya airejeshe ile ambapo itafuatiliwa kwa muda kabla hajapewa nyingine
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Sasa utaachaje kuweka kidole tena wakati umeambiwa mtandao umefeli au ukiambiwa badili kidole kingine hicho kimegoma.
TCRA hapo mmefeli mngetengenezatu utaratibu kwamba haiwezekani laini za mtandao mmoja zikasajiliwa ndani ya siku moja. Hilo lingemaliza tatizo hilo
 
Back
Top Bottom