Hii mbona ilikua wazi ilitakiwa umpigie mwalim mkuu kwanza kabla ya yoteWakuu, mchana huu kama saa sita hivi nimepokea ujumbe huu 'HABARI YAKO MZAZI MIMI MWALIMU HAPA SHULENI MWANAO AMEANGUKA GAFLA NAOMBA NIPIGIE HARAKA', ujumbe huu unatoka 0746136380.
Nikachanganyikiwa mno kwani mwanangu kweli yupo skuli Arusha 'boarding', nikampigia huyo jamaa na kuzidi niambia kuwa eti ana malaria ya muda mrefu na kwamba kadi yake ya Bima ya afya hawajaiona halafu akaniunganisha na daktari. Daktari kaniambia panatakiwa chupa ya maji haraka na nitume sh 57,500/=, sikuwa na ajizi nikatuma sh 60,000/= kupitia M-Pesa ndipo nikafahamu jina la huyo mwalimu tapeli kuwa ni Beatus Lyandungwe.
Alipopata hiyo pesa akanipigia na kuniambia kuwa pana majibu ya vipimo vya damu na harakaharaka akanipa tena huyo daktari (tapeli) na kuniambia damu ya mtoto haina tatizo (kumbuka hapo mwanzo aliniambia mtoto ana malaria) ila kwa kuwa kavuja damu nyingi baada ya kuanguka hivo chupa mbili za damu zinatakiwa na kwambi kila chupa ni sh 60,000/=.
Hapo nikasituka na kuamua kumpigia mwalimu mkuu, yeye akasangaa na kunipa pole ya kutapeliwa.
Voda nilipowapigia wakanitaarifu jamaa kesha toa hiyo sitini.
tafuta uzi upo humu andika mobistock utaelewaHiyo mobistock ndiyo mdudu gani tena jamani?
Aksante sana mkuu, mtu hukosea mara ya kwanza. Na kama ulivosema ujumbe huo kama una mtoto shule ya bweni tena mkoa tofauti hali ya kupanic utakuwa nayo tu.Pole sana na hongera kwa kumjali mwanao kuhakikisha unaokoa maisha yake ambayo ni furaha yako. Hali kama hiyo ya kupanic inatokea na baadae hurudi ghafla na kujua kuwa umetapeliwa. Wachache watakuelewa. Ungekuwa hauna mtoto shule ndo ungejua mapema hao ni matapeli.
Wakuu, mchana huu kama saa sita hivi nimepokea ujumbe huu 'HABARI YAKO MZAZI MIMI MWALIMU HAPA SHULENI MWANAO AMEANGUKA GAFLA NAOMBA NIPIGIE HARAKA', ujumbe huu unatoka 0746136380.
Nikachanganyikiwa mno kwani mwanangu kweli yupo skuli Arusha 'boarding', nikampigia huyo jamaa na kuzidi niambia kuwa eti ana malaria ya muda mrefu na kwamba kadi yake ya Bima ya afya hawajaiona halafu akaniunganisha na daktari. Daktari kaniambia panatakiwa chupa ya maji haraka na nitume sh 57,500/=, sikuwa na ajizi nikatuma sh 60,000/= kupitia M-Pesa ndipo nikafahamu jina la huyo mwalimu tapeli kuwa ni Beatus Lyandungwe.
Alipopata hiyo pesa akanipigia na kuniambia kuwa pana majibu ya vipimo vya damu na harakaharaka akanipa tena huyo daktari (tapeli) na kuniambia damu ya mtoto haina tatizo (kumbuka hapo mwanzo aliniambia mtoto ana malaria) ila kwa kuwa kavuja damu nyingi baada ya kuanguka hivo chupa mbili za damu zinatakiwa na kwambi kila chupa ni sh 60,000/=.
Hapo nikasituka na kuamua kumpigia mwalimu mkuu, yeye akasangaa na kunipa pole ya kutapeliwa.
Voda nilipowapigia wakanitaarifu jamaa kesha toa hiyo sitini.
jaman had nimepaliwa!dah nimecheka wakt nakula..eti nimewaza neno ng'ombe!dahh tisherrrrNg'ombe wanazaliwa kila siku.
Na watanzania mnapenda kutapeliwa sana. Kwa nini usinunue vocha kawaida unaamua ku-complicate mambo!tafuta uzi upo humu andika mobistock utaelewa