TCRA naomba msaada wenu, nimetapeliwa mchana huu

TCRA naomba msaada wenu, nimetapeliwa mchana huu

Daaah!! kuna kauvivu wa kufikiri kidogo mixer haraka iliyokosa baraka hadi ukagawa hela kwa wasiojulikana.
 
Mkuu, pana zile jumbe za kutumiwa pesa hizo nimezizowea lakini hii kwangu ndo imekuwa ya kwanza na sijapata isikia.
Pole sana sikiliza hiyo audio utajifunza kitu nimekutumia
 
Pole sana ndugu yangu, sasa mwenzenu kaibiwa bado tena mna mporomoshea matusi na kashfa, hii sio sawa. Ijue 60 usawa huu lazima kichwa kikuume
 
Tena huyo mwalimu mkuu ilitakiwa baada kukupa pole ya kutapeliwa akuongezee na tusi zito sana la nguoni
 
Swaga zingine mnaoonewa wanawajua.. hivi mtu aje aniambie upuuzi huoo halafu natuma hela tu hata kama namapenzi mazito kwa mwanangu. Haijawahi tokea kwa kweli kutuma hela bila kupata uthibitisho kwa mwl mkuu. Nina namba za mwl wake wa darasa na patron na pia mkuu wa shule.. lolote likitokea hao huwa wananipigia na sio new number from pasipojulikana.. halafu hao watu jaman kwa nn wasikamatweeeeee....
NB:
Kuna siku niliwahi ambiwa nitume hela kwani nilotumiwa imekosewa nilikuwa nimetumiwa hela na mtu wangu wa karibu muda si mrefuu. Nilichofanya nilichukua ile meseeji na kuongeza masifur kibao ikawa kama milioni kadhaa nimamforwadia akagie nayo mbele..
Jifunze kupunguza jazba na kucontrol hari.
 
Daaah!! kuna kauvivu wa kufikiri kidogo mixer haraka iliyokosa baraka hadi ukagawa hela kwa wasiojulikana.
Mkuu, sio kauvivu. Hebu fikiria kama mzazi mwisho wa mwezi uliopita bweni la Mihayo sec kwa 'form one' liliungua na vitu vyote viliteketea ikiwa na vya mwanangu.
 
Mkuu, sio kauvivu. Hebu fikiria kama mzazi mwisho wa mwezi uliopita bweni la Mihayo sec kwa 'form one' liliungua na vitu vyote viliteketea ikiwa na vya mwanangu.
Ni Mara ngapi huwa unawasiliana na walimu/wasimamizi wa mwanao akiwa shule ?. Je, huwa wanatumia the same style na iliyotumiwa hapo na hao watu?.

Kumbukumbu zangu zinasema kuna clip iliwahi sambaa ya mama mmoja aliyenusurika kudhurumiwa na Matapeli with exactly same style of yours. Sina 7bu ya kusema pole katika hili.

Ni sawa Waafrika wavivu, ila ume advance kidogo.
 
Ni Mara ngapi huwa unawasiliana na walimu/wasimamizi wa mwanao akiwa shule ?. Je, huwa wanatumia the same style na iliyotumiwa hapo na hao watu?.

Kumbukumbu zangu zinasema kuna clip iliwahi sambaa ya mama mmoja aliyenusurika kudhurumiwa na Matapela with exactly same style of yours. Sina 7bu ya kusema pole katika hili.

Ni sawa Waafrika wavivu, ila ume advance kidogo.
Mkuu, sio rahisi kwangu kwani huwa napokea mpaka e-mail za kitapeli kama toka FIFA, Toyota na kadha wa kadha ila hii ya leo KIBOKO.
 
Wakuu, mchana huu kama saa sita hivi nimepokea ujumbe huu 'HABARI YAKO MZAZI MIMI MWALIMU HAPA SHULENI MWANAO AMEANGUKA GAFLA NAOMBA NIPIGIE HARAKA', ujumbe huu unatoka 0746136380.

Nikachanganyikiwa mno kwani mwanangu kweli yupo skuli Arusha 'boarding', nikampigia huyo jamaa na kuzidi niambia kuwa eti ana malaria ya muda mrefu na kwamba kadi yake ya Bima ya afya hawajaiona halafu akaniunganisha na daktari. Daktari kaniambia panatakiwa chupa ya maji haraka na nitume sh 57,500/=, sikuwa na ajizi nikatuma sh 60,000/= kupitia M-Pesa ndipo nikafahamu jina la huyo mwalimu tapeli kuwa ni Beatus Lyandungwe.

Alipopata hiyo pesa akanipigia na kuniambia kuwa pana majibu ya vipimo vya damu na harakaharaka akanipa tena huyo daktari (tapeli) na kuniambia damu ya mtoto haina tatizo (kumbuka hapo mwanzo aliniambia mtoto ana malaria) ila kwa kuwa kavuja damu nyingi baada ya kuanguka hivo chupa mbili za damu zinatakiwa na kwambi kila chupa ni sh 60,000/=.

Hapo nikasituka na kuamua kumpigia mwalimu mkuu, yeye akasangaa na kunipa pole ya kutapeliwa.

Voda nilipowapigia wakanitaarifu jamaa kesha toa hiyo sitini.
Ila wewe inaonekana ni mzazi boya. Kweli kweli.ulishindwaje kumpigia kwaza mkuu wa shule?
 
Back
Top Bottom