TCRA: Laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa namba za NIDA zitafungwa kufikia Desemba 31, 2019

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
1576823620806.png
Mamlaka hiyo imesema kwamba hakuna laini ya simu itakayofungwa kabla ya tarehe hiyo.

Aidha, imesema wananchi wanatakiwa kwenda kusajili laini zao kwa kutumia vitambulisho vya uraia, na kuthibitisha usajili huo kabla ya muda uliowekwa kwa kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya kuzifunga.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakanjala, alisema hadi sasa laini za simu milioni 20 zimesajiliwa.

“Hakuna mabadiliko yaliyotolewa ikifika Disemba 31, mwaka huu, laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa namba ya Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa) na kuthibitisha kwenye mifumo zitafungwa, tunawakata wananchi wasajili haraka,” alisema.

Aidha, alisema hakuna mtoa huduma atakayeruhusiwa kufunga au kukatisha mawasiliano ya mtumiaji yeyote kabla ya muda uliopangwa.

Jana kwenye baadhi ya makundi songezi (WhatsApp) baadhi ya watumiaji wa laini za simu walilalamika kukosa mawasiliano kwenye baadhi ya laini kwa kile kilichoelezwa kuwa zimezimwa kwa kuwa hawajasajili.

Mei mwaka jana, serikali ilitangaza ulazima wa usajili wa laini za simu, na kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka huu zitafungwa.

IPP Media
 
Wafunge haina shida... Mimi nazani ikifika tarehe 29 nitakuwa tayari nimetoa pesa zangu zote kwa laini zao kama njia ya kujiandaa na zoezi hilo ufungaji...

Watu wana zimia ktk mafoleni NIDA wamekaa hawana mawazo mbadala kutatua changamoto ya upatikanaji wa vitambulisho...

Wafunge tu... Tutaanza upya wakiwa wamesha jizatiti kutoa huduma bora sio bora huduma...

Nazani ukusanyaji wa mapato ya serikali kuanzia January yatashuka kwa speed kubwa ktk hii nyanja...

SMS na simu za kheri ya mwaka mpya tuta zisikia na kusomewa ktk TV....
 
Umeongea maneno kuntu kabisa aisee!
Wafunge tu japo tutaumia

NIDA, foleni hazipungui kila siku na bado hata walio fanikiwa kukamilisha, bado wanazungushwa!

Na unaweza kuwa umemaliza kila kitu siku ya kufuata namba ndipo wanakwambia anza upya! Taarifa zako zilikosewa! Zinakosewaje na wakati ziko kwenye Database yenu mliiweka kwa ufasaha!?

Maafisa wa NIDA nao siku hizi wanataka waitwe na kuonekana miungu watu! Utadhani wamekuwa watu special kutoka sayari ya Jupiter! Hii nchi bhaana! Kila kitu ni fursa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom