Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
TCCIA Manyara imedai imedai licha ya tuhuma zinazomkabili Ramadhani Rashid Msangi, kwa sasa sio mwajiriwa wa Chama hicho kwani aliondolewa kazini tangu Aprili 2019.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari imetolewa na Uongozi wa Chama hicho ikieleza kuwa Mfanyakazi hahusiki na shughuli zozote za Chama hicho.
Taarifa hiyo imesema "Tunajitahidi kufuata miongozo na mifumo iliyoainishwa katika katiba yetu, pamoja na kuzingatia sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunathamini uwazi na uwajibikaji katika kazi zetu, na tunajitahidi kuhakikisha kwamba tunazingatia viwango vya juu vya maadili na utawala bora katika kila hatua tunayochukua."