Manyara: Mshauri wa Wafanyabiashara TCCIA ahukumiwa kwa kughushi nyaraka za malipo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,537
9,348
Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara imemhukumu Bw. RAMADHANI RASHID MSANGI ambaye ni Mshauri wa Wafanyabiashara mwajiriwa wa Chama cha wenye viwanda na kilimo Mkoa wa Manyara (Bussines consultant -TCCIA Manyara).

Mshtakiwa ameamriwa kulipa faini kiasi cha shilingi 900,000/= au kwenda jela miaka mitatu, kwa kosa la kughushi nyaraka za malipo.

Hukumu hiyo dhidi ya Ramadhani Rashid Msangi katika shauri la uhujumu uchumi Na. 05/2023, imetolewa chini ya Mhe. Martin Massao, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Manyara Machi 22, 2024.

Mshtakiwa alighushi nyaraka mbali mbali katika marejesho yake kuonesha kuwa alihudhuria na kuendesha mafunzo ya wajasiriamali yaliyofanyika wilayani Hana'ng kwa kipindi cha Mwezi Februari na Juni Mwaka 2018 na kwamba alitumia kiasi cha shilingi 6,695,000/= kugharamia posho ya chakula , ukumbi na nauli kwa waliodaiwa kushiriki mafunzo hayo - huku akijua taarifa hizo hazikuwa sahihi.

Mshitakiwa amelipa faini na kuachiwa huru na mahakama.
 
Huko manyara kaingia chaka wanapenda sana kesi watu wa huko..
Hiyo michezo inafanywa sana mikoa ya pwani na usukumani huko.
 
Hivi mahakimu hawajui hesabu au Ni rushwa nje nje wanachukua?
Au labda Mimi Nina akili kuliko mahakimu?
Si ajabu Cde msangi anaendelea na kazi Kama kawaida.
Hii inamfundisha Nini mwizi mtarajiwa????
 
Na chenji iliyobaki ameipeleka kwa nani? au ameirudisha TCCIA? au shauri limeshia hapo.kama ni hivyo kuna walakini na interpretation ya sheria iliyotumika

-KUMBUKA Aliyetenda Kosa ni MSHAURI WA WAFANYABIASHARA-
 
Hivi mahakimu hawajui hesabu au Ni rushwa nje nje wanachukua?
Au labda Mimi Nina akili kuliko mahakimu?
Si ajabu Cde msangi anaendelea na kazi Kama kawaida.
Hii inamfundisha Nini mwizi mtarajiwa????
Hakimu anasema adhabu hatoi kichwani bali zimeshaandikwa, kosa hili adhabu yake hii
 
Ishu hapo no risiti kama za taxi, caterer n.k but mafunzo yakifanyika sema risiti ndo tatizo
 
Back
Top Bottom