TCCIA Manyara yasema Ramadhani Rashid Msangi aliyehukumiwa kughushi nyaraka sio muajiriwa wao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
WhatsApp Image 2024-03-28 at 11.02.45_1e86670c.jpg
Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Mkoa wa Manyara (TCCIA Manyara) kimeeleza kuwa taarifa zilizosambaa mitandaoni zikimtaja mshauri wa biashara na mwajiriwa wa TCCIA Manyara, Ramadhani Rashid Msangi aliyehukumiwa kwenda jela miaka 3 au kulipa faini ya shilingi 900,000 kwa kosa la kughushi nyaraka za mafunzo kwa wajasiriamali Mwaka 2018 hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Manyara (Machi 23, 2024) kuwa hausiki na chama hicho.

TCCIA Manyara imedai imedai licha ya tuhuma zinazomkabili Ramadhani Rashid Msangi, kwa sasa sio mwajiriwa wa Chama hicho kwani aliondolewa kazini tangu Aprili 2019.

Taarifa kwa Vyombo vya Habari imetolewa na Uongozi wa Chama hicho ikieleza kuwa Mfanyakazi hahusiki na shughuli zozote za Chama hicho.

Taarifa hiyo imesema "Tunajitahidi kufuata miongozo na mifumo iliyoainishwa katika katiba yetu, pamoja na kuzingatia sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunathamini uwazi na uwajibikaji katika kazi zetu, na tunajitahidi kuhakikisha kwamba tunazingatia viwango vya juu vya maadili na utawala bora katika kila hatua tunayochukua."
 
Na hao TCCIA waache porojo. Tukio la kughushi lilitokea 2018 huyo Msangi alipokuwa ni mwajiriwa wao! Walimfukuza kazi mwaka 2019! Na hukumu imetoka 2024!
 
Na hao TCCIA waache porojo. Tukio la kughushi lilitokea 2018 huyo Msangi alipokuwa ni mwajiriwa wao! Walimfukuza kazi mwaka 2019! Na hukumu imetoka 2024!
Mshtakiwa alighushi nyaraka mbali mbali katika marejesho yake kuonesha kuwa alihudhuria na kuendesha mafunzo ya wajasiriamali yaliyofanyika wilayani Hana'ng kwa kipindi cha Mwezi Februari na Juni Mwaka 2018 na kwamba alitumia kiasi cha shilingi 6,695,000/= kugharamia posho ya chakula , ukumbi na nauli kwa waliodaiwa kushiriki mafunzo hayo - huku akijua taarifa hizo hazikuwa sahihi.
 
Back
Top Bottom