TBS watoa ufafanuzi kuhusu bidhaa ya Majani ya Chai ya "Safari Premium Tea"

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
TAARIFA KUTOKA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS)

Ufafanuzi kuhusu bidhaa ya Majani ya Chai ya "SAFARI PRIMIUM TEA"

@TBS_Tanzania

IMG-20230221-WA0634(1).jpg

====
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonesha utata unaotokana na taarifa iliyopo kwenye kifungashio kuhusu uasili wa bidhaa ya majani ya chai aina ya Safari Premium Tea na matumizi ya alama ya ubora ya TBS kwa chai inayoingizwa kutoka Kenya na kufungashwa hapa nchini.

TBS inapenda kuujulisha umma kuwa bidhaa hiyo inazalishwa na kiwanda cha Afri Tea and Coffee Blenders (1986) Ltd cha jijini Dar es Salaam, Tanzania na kimepewa leseni namba 1595 ya kutumia alama ya ubora ya TBS kwenye bidhaa za Blended Black Tea (Green Label Tea, Kilimanjaro, African Pride, Simba Chai, Simba Chai Tangawizi, Safari Premium Tea) tangu mwaka 2014 na bidhaa zote hizi zinazalishwa Tanzania na kwa kutumia malighafi kutoka ndani ya nchi.

Kutokana na taratibu za utoaji leseni, kiwanda hiki kimekuwa kikikaguliwa kwa vipindi tofauti ambapo ukaguzi wa mwisho ulifanyika tarehe 2022-08-11 ambapo hakukuwa na mabadiliko yoyote kuhusu utaratibu wa uzalishaji na malighafi. Hivyo, kufuatia taarifa hiyo, TBS ilifanya ukaguzi wa dharura kiwandani tarehe 2023-02-20 na kujiridhisha kwamba mzalishaji aliingiza chai kama malighafi kutoka Kenya mwezi Oktoba, 2022 bila kutoa taarifa kwa TBS kama mkataba (Scheme of Inspection and Test) unavyotaka. Hivyo. suala hili linashughulikiwa na hatua stahiki zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.

TBS inawashukuru wananchi wote ambao wanaendelea kutoa ushirikiano kwani suala la udhibiti wa usalama na ubora wa bidhaa ni mtambuka.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja kwa namba 0800 110 827.
Imetolewa na:
Gladness H. Kaseka​
 
Attachments

  • IMG-20230226-WA1084.jpg
    IMG-20230226-WA1084.jpg
    116.8 KB · Views: 5
hahahahahaha TRA bana, hapo kuna officers kadhaa wa TRA wanahusika moja kwa moja, but kama mwenye mamlaka anaishia kusema STUPID huku jicho linarembua unadhani hawa WAHAFIDHINA wa nchi watafanyaje. Ngoja tuone kiwanda kitalipa mabilion mangapi kama faini
 
Umeandika Nini hii wewe mtu,unadhani bila taasisi za serikali kuna nchi!? Sasa unataka kutulaumu wewe au!?
Hujanielewa, hapa nazungumzia waleta bidhaa kimagendo na wale wanaowasidia vusha magendo hayo.Kuna watu hawajali kabisa afya za ndugu zao wao wanaangalia pesa tu ndiyo naowaongelea.Ndiyo maana nikasema tutaishia laumu taasisi kumbe vitu vimepita njia ya panya huko. Maana nijuavyo mimi bandarini kuna tbs,tmda,tra,polisi,bandari wenyewe,mkemia mkuu wa serikali,usalama sasa unataka niambia hawa wote hawakuona au waliacha? isitoshe mzigo hauwezi toka kama tbs au tmda au mkemia mkuu hajapasisha na pia kama hujalipa garama za bandari na pia kodi za tra hujamalizana nao.
 
Sasa wewe majambazi yakivamia kila uchwao na kupola na kuu a raia ,kwa uelewa wako unataka tuyalaumu majambazi na sio polisi!!?
 
Sasa wewe majambazi yakivamia kila uchwao na kupola na kuu a raia ,kwa uelewa wako unataka tuyalaumu majambazi na sio polisi!!?
kama yanasaidiwa na wananchi kuyaficha je? kila mtu akichukua jukumu haya mambo yatakuwa hamna sasa wewe kama raia unaona kabisa kitu kinapita njia ya panya unasaidia badala ya kutoa taarifa mwisho wa siku unakuja laumu. niwapongeze hao waliotoa taarifa TBS maana wamesaidi kizazi na kizazi kupata madhara.wengi tunaona ni jukumu la taasisi husika kumbe hata sisi raia tunajukumu tunapoona kitu hakiko sawa kutoa taarifa
 
Back
Top Bottom