TBC1 inapotumika vibaya: Nani alaumiwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBC1 inapotumika vibaya: Nani alaumiwe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Asha Abdala, May 3, 2009.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  TBC wanaoendeshwa kwa kodi yako wewe na mimi. Hawa ndio waliotumiwa na Rostam Aziz kuihusisha kwa nguvu zote CHADEMA na Kifo cha Wangwe.

  Mnaweza kukumbuka mtiririko wa mambo waliyoyafanya. Hawa ndio waliokatisha hotuba ya Dr Slaa kuhusu ufisadi aliyotoa bungeni watanzania wasiione. Ndio hao hao, wiki iliyopita walikatisha hotuba ya Zitto Kabwe iliyohusu ufisadi. Hawa ndio ambao leo wamerusha maelezo ya fisadi Rostam Aziz (wenyewe wanasema kwa kulipia).

  Kwa hiyo natoa hoja, Dr Slaa peleka TBC ule mkanda wako wa hotuba yako ya Mwembe Yanga. Ule ambao TBC hata kwenye habari yao hawakurusha majina ya mafisadi badala yake walisema tu 'wapinzani wataja watuhumiwa wa ufisadi'. Sasa peleka mkanda mzima, wewe ni mbunge kama Rostam Aziz. Rusha hewani hotuba yako yote ya mafisadi 11. Kama walivyoirusha hotuba ya leo ya Fisadi Mshenzi (Uncivilized) Rostam Aziz. Hiyo ndio Tanzania Broadcasting Corruption (TBC).

  Halafu wakaulizwe Sophia Simba na Mkuchika, kuhusu utawala bora na matumizi ya vyombo vya habari.

  Asha
   
 2. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Well said Asha!! Double standards of our leaders, if I can pay and insult anyone in any News Channel, I am ready to pay and give a go at the Party and the government itself!! Zaidi ya yote wanatumia kodi zetu kutetea ufisadi?

  Nimeamini sisi ndio wenye tatizo, why do we have to keep these thugs in power anyway?
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hilo ndo tunalisubili kwa mikono miwili! Kama si mtu mzima aibu!
   
 4. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  when the fight stands between political parties, its member are left with no choice more than defending their political parties members and not necessary the issues. Let get out of party politics.
   
 5. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapana, suala sio vyama hapa. Ni kuhusu Mwanamtandao Mshenzi(Uncivilized) Tido Mhando ambaye anakubali kuwa kuwadi wa mafisadi kwa kutumia television ya umma!

  Asha
   
 6. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kabisa nia ya maandiko yako ni kuonyesha Ukuwadi wa TIDO, lakini kwangu haisomeki hivyo. Ingawaji hujaandika nene chadema, cuf lakini munkari na ushahidi wako unaongelea hilo.

  Tofauti ni nini kati ya mtandao na ccm? Kwanini uwateje Zitto na Slaa peke yao, ama ndio kusema wao wenyewe ndio wamenyanyasika na TBC?

  Nia yangu si kulumbana ila nilikuwa natoa tahadhari maana mijadala mingi inapoteza hamasa pale ambapo uchangiaji wake unajikita kwenye siasa zaidi, hasa hoja inapojaribu kuongelea maslahi ya wapinzani. Ni vyema, tusome hisia hizi, ili kuhakikisha hoja zetu zinabebwa na wengi - nje ya siasa za vyama!
   
 7. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu mbona maelezo ya Asha yapo clear kabisa. Hujaona hoja yake yamsingi hapo mkuu?
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,549
  Trophy Points: 280
  Huu mjadala watu wanakuwa so emotional for nothing, Dada Asha, kwa sisi tunaoijua TBC ilivyokuwa na ilivyo sasa, please, please, please, leave Tido na timu yake alone!

  kipindi cha Fisadi Papa kuhusu fisadi Nyangumi sio TBC production. ni kipindi cha nje, by production house, jamaa kalipia, kosa la Tido lipi.

  Hata Mbowe na Chadema akilipia kipindi kinarushwa.

  Kile cha Mwembeyanga hata ningekuwa mimi ningekirusha bila majina kwa sababu ni tuhuma. Fisadi Nyangumi alimwaga tuhuma za fisadi papa bila kutoa ushahidi, fisadi papa kamwaga za Fisadi nyangumi na nondo juu. siye dagaa ni kuangalia movie tuu, kosa la TBC lipi?

  Hivi kelele zote hizi kuhusu fisadi papa, anayelelewa na JK, halafu fisadi nyangumu anataka kumsaidia JK kumtokomeza fisadi papa, kweli inakuja hii?.

  Mzee wetu ana agenda yake, ilidhamiria kulamba dume, tatizo kazichanga vibaya karata zake akalamba magarasa huku mshindani akichezesha mizungu na dume JK yuko mkononi.

  Tuendeleeni kudebate ila TBC iacheni kando.

  Ukiwa na pesa nchi hii unaabudiwa, mwenye CNN ni Ted Turner, ushawahi kumuona kwenye CNN?. Mwenye Sky ni Rupert Murdoch, ushawahi kumuona kwenye TV?. Mzee wako ni kila kukicha, unataka kumlinganisha na Tido?

  Hata ukiwaweka wakae kimya kwa kuwatazama machoni tuu, kama una macho, utaona tofauti, leo unataka kuzielekeza hasira za kipenzi cha watu kuitwa papa nyangumi, kwa kuigeuzia kibao TBC?

  Tudadilianeni, tulumbane, tubishane na tukubaliane au tusikubaliane, leave TBC alone.
   
 9. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Pasco

  Pale Mwembe Yanga Dr Slaa na Tundu Lissu walilitoa tuhuma na ushahidi tena kwa kunukuu nyaka za serikali yenyewe. Kwanini TBC hawakurusha?

  Halafu tofautisha TV ya umma na ya binafsi, ya umma si suala la fedha tu na kurusha. Inatizama pia maslahi ya taifa. Sasa kama hao TBC wameona maslahi ya Taifa ni kipindi maalum cha Rostam wakaacha Orodha ya Mafisadi na wakakwepa kurusha session contraversial za Bunge tena kwa kuzikatisha kati kati then hatupaswi kuwaacha hao Tanzania Broadcasting Corruption(TBC). Tido anatumiwa!

  Asha
   
 10. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pasco nadhani hii issue imekugusa kwenye rizki..tbc was wrong for this and you know it..bbc hata sikumoja haiwezi rusha malumbano ya watu binafsi kwa kipindi maalamu..nadhani huelewi kazi ya public body. CNN and Sky ni Private wamiliki wakijisikia kujitangaza they can do so, uamuzi tuu!! Kama ulivyosema mwenye Tido na Mengi huwezi linganisha kwasababu Tido ni Mfanyakazi wa SERIKALI!!
   
 11. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Asha amekuwa mshabiki zaidi wa vyama kuliko issue iliyopo.tizama mchango wake kwenye press ya RA.

  inasemwa sana kuwa Mengi anaisaidia Chadema na kweli hili wapenzi wote wa Chadema wamejiweka wazi kuwa wako pamoja na Mengi.
  Asha naomba uelewe siku bunge lilipomtoa lowassa wadhifa wa ubunge kupitia ripoti ya Mwakyembe ni TBC iliyorusha habari ile LIVE!.

  Lakini Lowassa baadaye alikwenda kununua airtime na kuanza kujibu tuhuma zote alizopewa na Bunge ambalo ni serikali inayoimiliki TBC.kama TBC walimpa nafasi Lowassa kusema anachokitaka dhidi ya serikali sioni Tatizo kwa Rostam kupata fursa hiyo.

  Sophia Simba alifanyiwa maandamano alipochukuwa Uenyekiti wa UWT na yalirushwa na TBC kwa gharama ya milioni sita,kama Slaa,Zitto,Mengi au Mbowe wanataka kurushwa kwa kulipia hakuna tatizo.
   
 12. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Pasco, Asante kwa uchambuzi wako katika suala hili. Lakini toka lini mbwa akamuuma master wake anayemlisha mabaki ya chakula?
   
 13. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hayawi hayawi sasa yamekuwa,Vile vita vya mafisadi papa na nyangumi vimetinga hata kwenye vyombo vya umma,Ni usiku wa jana tu RA alikuwa akitumia TBC1 kulumbana na RM nani zaidi.Swali langu kwa jamii ya Tanzania kama tumefikia hatua hii ya kutumia vyombo vya umma kuvunjiana na kujibishana tuhuma dhidi ya mbaya fulani hatima yake ni nini?Je chombo cha umma kama TBC1 kinapofikia kuvunja maadili na kukubali kutumiwa na wachache nani alaumiwe?Awajibishwe?
   
 14. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #14
  May 4, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Maslahi ya taifa kwa TBC ni kumlinda Rais na viongozi wa CCM.muda mrefu tumekua tukiumiza vichwa vyetu kuhusu maslahi ya taifa.Kwa nchi yetu maslahi ya taifa ni hayo niliyoyataja hapo juu.Kitu kingine ambacho tunajaribu kijifanya kukielewa ni kuhusu nani Rais wetu kikatiba ni JK kiukweli ROSTAM AZIZ.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 15. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Mambo hadharani badala ya kujadili fisadi papa na nyangumi sasa wanairukia TBC.kwani kwani RAM naye unamuonaje si huyo huyo kama hao anaowatuhumu.

  Naye analipa sana payroll, kwani fedha anazozipata za bure anazifanyia kazi gani kama si hiyo ya kununua umaarufu. Kama mfanyibiashara wa kweli kwa jinsi nchi hii inavyotoza kodi asingepata fedha za kujiingiza kwenye kwenye kutaka umaarufu katika kila sekta ya maisha.

  Hapa suala RAM anatakiwa kujibu hizo account alizochukua pesa ni yake au laa .
   
 16. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Duh we need to restructure the all media personel and also the government needs to change from being under politician influence, what I mean is to stop working as a part of a political part
   
 17. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Sheria ya vyombo vya habari VS umiliki unatakiwa kutazamwa upya sio \Kwa TBC hata IPP
   
 18. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kimatire,
  Hebu tupe taarifa kamili ya yaliyojiri maana TBC kuripoti sio vibaya kama iko hiyo habari iko balanced.

  Lakini kama wanampamba RA then itabidi Tido atueleze ni vipi mbona hakuyafanya hayo alipokuwa BBC?
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Asha, i support you 100%. Huyu Tido sio civilized bali ni syphilized!

  Hata kama yeye ni pro-FISADIs asitumie TV ya taifa kunajisi kodi zetu for

  whatever price of airtime. So they have shown to us which side they are

  biased to!

  Washindiliwe na walegee!!
   
  Last edited: May 7, 2009
 20. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2009
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ni kweli,kinachoendelea kaika hiinchi ni ujinga mtupu, kuanzia tbc1 hadi serikalini kuhusu suala zima la mafisadi..
  its non sense,mawaziri wale wawili aotetea ufisadi hawana akili..
  kuna mengi ya kurekebisha katika nchi hii..
   
Loading...