Uchu wa Urais umewatoa macho na staha Tundu Lissu na Zitto Kabwe

Dec 13, 2018
30
140
UCHU WA URAIS, UMEWATOA MACHO NA STAHA TUNDU LISSU NA ZITTO KABWE.

Leo 13:15pm,10/02/2019.

Kadri afya ya Tundu Lissu inavyoimarika na kuonesha dalili ya kurejea Tanzania ndivyo Zitto Kabwe anavyozidi kuibua matukio ya kulazimisha azungumzwe na kubaki kwenye kurasa za mbele za magazeti.

Zitto Kabwe alifanya siasa za kiungwana sana miaka ya 2005-2010 akijaribu kujenga hoja na ushawishi wa aina mbalimbali ndani na nje ya bunge,pengine kwa kuwa alipata chochote kitu kwa wakati ule lakini si sasa katika utawala wa Mh Rais Magufuli, Utawala ambao hauna rushwa, Zitto Kabwe alijijenga Sana akijifunza toka kwa Dr Wilbroad Slaa aliyegombea Urais 2010 kupitia Chadema na Zitto Kabwe aliishia kuendelea kujifunza toka kwa Mkongwe wa Upinzani Dr Wilbroad Slaa kwa kuwa umri wake ulikuwa hautoshi kikatiba kugombea Urais.

Bahati mbaya sana mwaka 2015 umri wa Zitto Kabwe ulipotosha kugombea urais akakuta soko la siasa za upinzani bidhaa inayouzwa sana katika nafasi ya Mgombea wa kiti cha Urais Upinzani ni Edward Lowassa aliyehamia Upinzani akitokea CCM,Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti na Mgombea Urais wa 2005 na chipukizi Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu.

Bahati ya mtende aliyoipata Zitto Kabwe kwa sasa tunapoelekea uchaguzi Mkuu wa 2020 ni kwamba chipukizi Tundu Lissu hayupo Tanzania.Kwa mazingira hayo Zitto Kabwe amepata fursa ya kujitengeneza ili kuishinda bidhaa inayoitwa Lissu kwenye siasa za upinzani,na hapa ndipo kitako cha andiko langu la leo.

Kimkokotenge Upinzani umekosa hoja kwa sasa baada ya Mh Rais Magufuli kutekeleza kwa vitendo yale yote yaliyokuwa yakipigiwa kelele na Upinzani wa Tanzania, Kwa sasa Upinzani umebadili strategy na kuanza kupinga maendeleo na kubadili kwa maneno kila chaupe kukiita cheusi kitu ambacho kimeshindwa kutamalaki katikati ya ukweli, Mviringo huu wa ulongo ulongo umewaleta kwetu Tundu Lissu na Zitto Kabwe kama wagombea Urais wa Upinzani mwaka 2020,Kwa ufupi kilichomuweka juu Tundu Lissu ni siasa zake za kiharakati na siasa hizi za kiharakati kumemlazimu Zitto abadili aina ya siasa zake na kuanza kufanya vuguvugu ya si siasa wala si harakati.

Mwanafalsafa wa kiajemi Murtadha Mutahhari anasema harakati huanzishwa na wanyongea kielezea nadharia hii katika mojawapo ya matoleo yake anasema, harakati zisizojikita kwenye mahusiani na jamii zimekosa sifa ya kuitwa harakati.

Mwanaharakati hunyooka kama kamba au ruler,ila Mwanasiasa hutembea katika fursa za kisiasa,wote awa Mwanasiasa na Mwanaharakati si waumini wa Uzalendo bali ni adui wa Uzalendo na ndipo tunapata mfano wa Tundu Lissu.

Zitto Zuberi Kabwe hatoshi kwenye hata moja kati ya mwanasiasa na mwanaharakati.Vijana wangesema hayupo duniani wala mbinguni.Kwa kutafuta mtoko hivi sasa Zitto Kabwe amechanganya siasa na harakati,kwa ufupi mchanyato huo tuuite "Vuguvugu" kwa hiyo Zitto Kabwe anafanya Vuguvugu na ndani ya vuguvugu kuna udini na ukabila. Ni rai yangu kumwangalia kwa umakini huyu Zitto Kabwe.

Kuanzia mwaka wa 2014 Zitto Kabwe alivyofukuzwa na Freeman Mbowe uko Chadema na kwenda kuiteka ACT WAZALENDO ndipo alipoanza kufanya vuguvugu, Miaka 2015 kurudi nyuma tafuta lini Zitto alikamatwa na polisi na mara ngapi katika kipindi chote umri wake hauku tosha kugombea urais linganisha na anavyokamatwa kamatwa wakati huu .

Zitto yule asiyekua anawaza urais alikua mjenzi hasa wa hoja kwa nini akamatwe? Japo hoja nyingi alipewa kwenda kuzisema bungeni na kuibua kashfa nzito nzito, lakini tofauti na miaka ya 2015 kurudi nyuma, Zitto huyu wa sasa ameonekana kutaka kufanana na Tundu Lissu ambao wote nia yao ni kugombea urais 2020.

Kama ambavyo Tundu Lissu anakamatwa kwa kutukana mamlaka na mihimili ya nchi vivyo hivyo tunamuona Zitto Kabwe akikamatwa Oktoba 31 2017 kwa kutamka maneno ya uchochezi kwenye kampeni,akakamatwa tena Jumatano Oktoba 31 2018 kwa kusema zaidi ya watu 100 wameuawawa mkoani Kigoma kabla yaFebruary 18,2018 mkoani Morogoro,kukamatwa tena kwa kukusanyika bila kibali mkoani Morogoro.Huyu ndiyo Zitto Kabwe wa sasa tofauti na yule aliyekuwa akijenga hoja za ukweli miaka ile ya 2005 hadi 2010.

-Ugomvi wa Zitto Kabwe na Tundu Lissu.

Zitto anasema,"Wakili Tundu Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari moja mbili, freelnder ninayotumia Dar Es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni. Tuhuma hii haimo katika tuhuma nilizotuhumiwa nazo na kuandikiwa na chama ili kujibu.

Kama Tundu lissu anadhani tuhuma hii ana ushahidi nayo wa kutosha aiongeze kwenye tuhuma walizoniandikia ili niweze kujitetea kwenye vikao, vinginevyo ni mipasho tu. Nawapa changamoto Tundu lissu na wenzake kama wana tuhuma Mpya dhidi yangu waniandikie kwa mujibu wa taratibu. Tuhuma nilizo nazo hivi sasa na ambazo nimezikatia rufaa katika Baraza Kuu zinahusu mkakati wa kugombea uenyekiti Taifa na kutaka mahesabu ya chama yakaguliwe na CAG."

"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. NaaminiMkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini.

Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.

Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?

Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda. Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.

They must know I am not a push over. Chacha died, I won't. Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili."

-Siasa za kujilinda za Zitto Kabwe.

Mh. Zitto hakutegemea kuwa siri zao na Mh. Mbowe walizozifanya wakati wa ujenzi wa CHADEMA wanaweza kuzitoa. Hii ni sawa sawa na kusema "mimi na fulani" tulishirikiana kumuua fulani kitu ambacho kinawaingiza wote hatiani na hasa kama hakuna a plea bargain. Kwenye siasa kufanya hivyo ni kujiua wote.

Baada ya kutolewa tuhuma. Mh. Zitto alipatwa na shock kwa sababu hakutegemea siri zao kutolewa, hii ilikuwa kama ni political scud la kumuua kisiasa, na kwa kufanya hivyo, na yeye akaamua kurusha scud kwa mtu ambaye anafahamu ndiye kichocheo cha bomu. Ndiyo maana hata utetezi wake na Mh. Mkono una mashimo mengi tu.

Mh. Mbowe pia hakutegemea kuwa Mh. Zitto anaweza kuyasema aliyoyasema, na yeye pia utetezi wake na Rostam una mashimo mengi tu.

Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa hawa wanasiasa wetu (Zitto na Mbowe) walichukua hizi pesa za mafisadi na kwa sasa wanataka kujenga hoja za kisiasa kwa faida yao kisiasa.

-Huu ni upepo na utapita kuhusiana na siasa za Tanzania.

Katika Hotuba ya kuaga bungeni, Zitto Kabwe,Alhamisi, tarehe 19 Machi 2015.Alisema na namnukuu,

Mheshimiwa Spika, katika hali ya kawaida na kwa mujibu wa katiba ya chama chetu, ilitarajiwa kwamba baada ya maamuzi ya Mahakama Kuu, Kamati Kuu ingekaa na kunipa rasmi mashtaka yangu yanayohusu uanachama wangu, mimi kuitwa kujieleza na hatimaye Kamati Kuu kutoa uamuzi wake. Hata hivyo, mara baada ya hukumu ya Mahakama Kuu dunia nzima ilitangaziwa na Mwanasheria wetu Mkuu, kwa niaba ya chama, kwamba mimi nimeshafukuzwa na sio mwanachama tena wa CHADEMA. Baada ya hapo viongozi wangu wametoa matamko mbalimbali yote yakionyesha kwamba sitakiwi tena katika chama hiki, pamoja na kwamba hadi ninapoongea hapa leo sijawahi kukabidhiwa barua yoyote inayonitaarifu kufukuzwa kwangu katika chama.

-Sheria za Vyama vya Siasa zinajibu tatizo alilopata Zitto Kabwe.

Katika hotuba ya Kisha bungeni, Zitto Kabwe analalamikia sheria dhaifu za vyama vya Siasa, namnukuu "Mheshimiwa Spika, vyama vya siasa ni jukwaa muhimu katika ujenzi wa demokrasia lakini havipaswi kamwe kuwa juu ya wananchi. Kwa hiyo ni maoni yangu kwamba wakati sasa umefika wa kukomesha udola na ufalme wa vyama vya siasa hapa nchini. Mfumo wa siasa ambao unavipa vyama vya siasa mamlaka ya kisheria ya kukanyaga mamlaka ya wananchi haupaswi kuendelea katika Karne ya 21 na katika nchi ambayo inaendeshwa kwa misingi ya demokrasia ya kuheshimu wananchi. Mimi ninaondoka bungeni sio kwa sababu wananchi wangu wa Kigoma Kaskazini walionichagua wametaka niondoke."

"Siondoki kwa sababu nimeshindwa kufanya kazi zangu za ubunge. Na kwa kweli siondoki kwa sababu wanachama wenzangu katika CHADEMA wametaka niondoke. Ninaondoka kwa sababu mfumo wetu wa kisheria unavipa vyama vya siasa mamlaka juu ya wananchi na wapiga kura. Ni matumaini yangu kwamba Bunge lako tukufu halitaruhusu mfumo huu unaoruhusu vyama vya siasa kupora mamlaka ya wananchi uendelee. Ni Bunge lako pekee lenye uwezo wa kukomesha mfumo ambao unatukuza Parties' Power, badala ya People's Power."

Nimalizie kwa kusema,Only Genuine will be called to do the job, Wenye Wito pekee ndio wataitwa kufanya Siasa kwa maana Siasa si Biashara tena bali ni kuwa Mtumishi wa Watu.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
 
CCM ni zaidi ndio maaana Tume ya Uchaguzi Polisi wote ni wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa najiuliza wapinzani wanaitwa Wana uchu wa madaraka, ivi wale wanaotumia jeshi la polisi, time, Ded, kuiba kura wanaitwaje?
 
Hivi kwanini tusiamini anayepiga watu risasi ndio ana uchu wa Urais?
 
Kuwajadili Tundu Lissu ama Zito Kabwe kwa kujaribu kuwa - portray negatively ku - suit interests zako na waliokutuma, it's a wastage of your time and resources....

Honestly, nimesoma heading then paragraph ya kwanza nikajua where exactly you are heading to....

Pole sana kwa maumivu. Lakini ndivyo ilivyo and it's time to go
 
kama magufuli hana uchu wa madaraka, kwanini anatumia wapambe kina juma nkamia ili aongezewe muda wa kutawala
 
Back
Top Bottom