Mimi sipati TBC1 na Star Tv wiki moja sasa huku Mbeya. Hata ATN inataka inikoseshe Champions League kesho
Kuna mambo kadhaa twapasa kuyajua au kuyafahamu, hata mimi ilinitokea halafu nikadhani wana mpango wa kuziondoa kabisa kutokana na kuingia kwa hii STAR TIMES.
1. Huu ni msimu wa upepo mkali kuna wakati unaweza kuyumbisha dish na hivyo kuanza kupotea kwa baadhi ya channel.
2. Kila baada ya muda fulani unatakiwa kukagua dish lako hasa viunganishio namaanisha F-connectors/M-connectors kwenye Receiver na LNB,
3. Hakikisha LNB yako ni CLEAN yaani haina uchafu au kitu chochote ndani. Hii ilinitokea siku moja au siku kadhaa nilikuwa napata channel mbili tu kwenye dish na zenyewe kwa low signal, nikajaribu kuangalia kwa majirani nikaona wenyewe baadhi yao wanapata channel karibu zote zinazotakiwa kuonekana. Nikatoa TV nje na kuanza kuset vizuri dish na matokeo yake ni channel zile zile mbili. Nikatulia, baada ya takribani mwezi mzima nikaondoa kabisa LNB na nikakuta kuna udongo fulani unasababishwa na wadudu waitwao nyigu. Nikauondoa kabisa kisha nikarudishia, amini usiamini channel zote zilizokuwa hazionekani zikaanza kuonekana tena kwa good signal.
Mimi niko maeneo ya Iyunga Mbeya natumia dish la futi 8, channel ambazo nazipata mpaka sasa kupitia satellite ya Lyngsat degree 64 ni:- ITV, EATV Capital, Star tv, TBC, Channel 10, ATN, TVM, TBN Namibia na Channel moja mpya ya Kiislam.
Au tembelea link ifuatayo kupata parameters za channel hizo.
http://www.lyngsat.com/intel906.html