TBC,Star TV wamefutika katika sattelite?

TBC,Star TV wamefutika katika sattelite?

Pia napenda kuwakumbusha kuwa kuna kupatwa kwa satellite mara mbili kila mwaka, na wakati wa tukio hilo channel zote zinazotumia Satellite ya Intelsat906 ya nyuzi 64 ambayo huonyesha channel nilizozitaja katika post iliyotangulia hukatika kabisa, pia hata radio nazo kukatika kabisa,

Kilelle cha matukio haya ni wiki moja au zaidi kabla na baada ya tarehe 21 March na 23 September. Na mara nyingi hutokea kati ya saa 3:30 na saa 5:00 asubuhi. Kwa wale tunaokumbuka Jiografia kwa shule za msingi au Geography kwa shule za sekondari tarehe hizo jua la utosi huwa katika mstari wa Ikweta. Tukio hili hutokea wakati ambapo Dunia, Satellite na Jua vinakuwa katika mstari mmoja. Kwa uthibitisho majira ya saa 4:00 asubuhi ukiangalia dish lako utakuta limeelekezwa kwenye jua ambapo kwa wakati huo satellite inakuwa katikati. Kuelekea mwishoni mwa wiki hii tutaanza kushuhudia tukio.
 
Back
Top Bottom