Leo nimefuatilia katika matangazo yenu kuhusu ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma. Kwa asilimia kubwa mnajitahidi sana kutomtaja John Pombe Magufuli katika ujenzi huo wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma. Sijajua kama ni maelekezo au ni matatizo yenu tu ya kutaka kujikomba kwa wenye mamlaka.
Mtanzania yeyote mwenye kichwa kizuri kabisa hawezi kuzungumzia ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma bila kumtaja John Pombe Magufuli.
Ukiachana na Mwl. Nyerere, JPM ni Rais pekee aliyeshupalia ujenzi huo wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma. Ndio maana Watanzania wengi si wapenzi wa kusikiliza TBC, kwa sababu kama hizo.
Badilikeni, hizi ni nyakati nyingine. Hilo hata mtoto mdogo kabisa wa darasa la kwanza anajua.