TBC, mnawatia aibu Watanzania

TBC, mnawatia aibu Watanzania

TBC ni kama bomba tu, mwenye kulimiliki (serikali iliyopo madarakani) ndio huamua maji gani yatoke, ama masafi au machafu. Kipindi cha utawala wa Magufuli, TBC ilikuwa busy kuhubiri kila ugoro wake na sasa Magufuli akiwa hayupo tena madarakani TBC hiyo hiyo imeamua kupotezea kila chema cha Magufuli. Hivyo hakuna cha ajabu, hiyo ndio TBC tunayoijua siku zote.
Kwa mchango huu, uzi ufungwe rasmi.
Kongole ndugu Zanzibar-ASP .
 
Mwendazake alikosea pale alipouliza umma"SIJUI NIKIFA MIMI NANI ATAWEZA KUFANYA MIRADI HII?"sasa nawenzake acha wauonyeshe umma kwamba wanaweza.
 
Ha ha ha uchawa umeanza tangu kipindi cha baba wa Taifa
 
Usivimbe mkuu bwawa aliliacha 32 na kujitapa kuwa yeye akiondoka madarakani miradi haitaendelezwa. Mungu alivyo fundi, kaamua kamletea mwanamama tu na anaendeleza fresh kabisa.
Acha chuki na mfu hakuwahi jitapa ila alihofia muendelezo kutokana na upinzani juu ya miradi hiyo.
 
Leo nimefuatilia katika matangazo yenu kuhusu ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma. Kwa asilimia kubwa mnajitahidi sana kutomtaja John Pombe Magufuli katika ujenzi huo wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma. Sijajua kama ni maelekezo au ni matatizo yenu tu ya kutaka kujikomba kwa wenye mamlaka.

Mtanzania yeyote mwenye kichwa kizuri kabisa hawezi kuzungumzia ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma bila kumtaja John Pombe Magufuli.

Ukiachana na Mwl. Nyerere, JPM ni Rais pekee aliyeshupalia ujenzi huo wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma. Ndio maana Watanzania wengi si wapenzi wa kusikiliza TBC, kwa sababu kama hizo.

Badilikeni, hizi ni nyakati nyingine. Hilo hata mtoto mdogo kabisa wa darasa la kwanza anajua.
Kila zama na kitabu chake... kila masika yana mbu wake.

Hata enzi za JIWE alishainjoi coverage ya peke ake mwacheni Samia nae ainjoi
 
Huyo kikwete wako alikuwa na kitu gani kizuri, zaidi ya ufisadi, uzembe, kuchekeana na lousy presidency?
Bila Kikwete kubuni mradi wa REA na kuutafuta pesa kwa wafadhili ili ukamilike huyo bibi yako aliyeko manyoni vijijini angekuwa anajua hata barubu ya umeme inafananaje?
Au hizo barabara ndefu za rami zinazo unganisha mikoa alizijenga baba yako?

Au hizo Shule za kata ambazo ndo zilifanya mpaka na nyinyi mnao jiita wanyonge mpate elimu zilijegwa na babu yako?
 
Acha chuki na mfu hakuwahi jitapa ila alihofia muendelezo kutokana na upinzani juu ya miradi hiyo.
Ali hofia kama nani? Yakuwa yeye alikuwa mungu hivyo angekufa ndo ungekuwa mwisho wa dunia?
 
Anawasumbua misukule yake mpk mnataka kutulazimisha na sie eti tuwe tunamtajataja
Ukimaliza kudonoa keyboard unapita kwenye miradi aliyoisimamia... na hakuna ndani ya hii nchi hutaona kazi zake. Utaishia kutukuna ila ukweli unao moyoni.
 
Nashukuru sana mtoa post ulichokieleza ni kweli kabisa mm ni shuhuda nimeangalia TBC hiyo hiyo Kwa kweli wanajitajidi kulikwepa sana jina la JPM naona kwa lengo la kujaribu kupoteza legacy yake ambayo haifutiki ingependeza Sana kama angepewa sifa zake stahiki maana bila JPM serikali ingekuwa bado iko Dar na kila mtu kimoyomoyo anajua hilo.

Japo samia kajitajidi kidogo kusema ukweli lakini historia imejaa kubeba awamu zote ili kupoteza nguvu kubwa iliyofanya awamu ya tano ambayo Kwa hakika bila juhudi hizo kusingekuwa na Ikulu na zingeendelea tu kuwa ndoto.

Nina hakika na ujenzi usingekuwa umefikia asilimia 70 kuna ambao walitamani hilo wazo lake lingekufa nae kuna watu walitamani wangesikia serikali inarudi Dar Ila ashukuriwe Mungu ambae ndie mpanga wa vyote.

Nimejikuta natokwa na machozi Mama Janeth na mwanae walipokwenda kupokea tuzo.

Tunamshukuru Mungu Kwa zawadi ya maisha ya JPM.

Mungu aendelee kumpumzisha shujaa JPM mahali pema peponi.

Amen.
 
Umesahau kabla ya mwaka 2005 Kijijini kwenu kulikuwa hakuna umeme!
Bahati hiyo hatukuwa nayo umeme ulifika kijijini mwaka 1984 nadhani hata bi mkubwa wako hakuwa na ndoto za kukuleta kwenye huu uwanja wa fujo... vumilia ndio uanaume.
Kiswahili kuandika pia shida tu... "kulikuwa hakuna".. sio sanifu tumia ukanushi kwa neno moja.. ungeandika hapakuwa na umeme
 
Leo nimefuatilia katika matangazo yenu kuhusu ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma. Kwa asilimia kubwa mnajitahidi sana kutomtaja John Pombe Magufuli katika ujenzi huo wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma. Sijajua kama ni maelekezo au ni matatizo yenu tu ya kutaka kujikomba kwa wenye mamlaka.

Mtanzania yeyote mwenye kichwa kizuri kabisa hawezi kuzungumzia ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma bila kumtaja John Pombe Magufuli.

Ukiachana na Mwl. Nyerere, JPM ni Rais pekee aliyeshupalia ujenzi huo wa Ikulu ya Chamwino, Dodoma. Ndio maana Watanzania wengi si wapenzi wa kusikiliza TBC, kwa sababu kama hizo.

Badilikeni, hizi ni nyakati nyingine. Hilo hata mtoto mdogo kabisa wa darasa la kwanza anajua.
Wewe si umeshamtaja INATOSHA!! Ila sisi TBC hatutaki kuhusisha mafanikio yetu na mtu alikuwa anaharibu nchi yetu.

Tunataka kabisa afutike yeye kwanza kwa sababu yeye ndiye alikuwa anataka kufuta watu kwa kuwaua kama akina Ben Saanane, Azory na mashambulizi ya Lissu
 
Mbona JPM alikuwa hamtaji JK ? halafu JPM alikuwa ana ujuaji mwingi mno alikuwa anafanya mambo kwa utashi wake na sio vile inavyotakiwa. Hivi unajua ile fly over ya pale Ubungo haikutakiwa iwe vile? Na michoro iliandaliwa utawala wa JK. Yule JPM alikuwa anapenda sana Macamera na kuwahadaa Wananchi wa kawaida na kuwatisha wenye nazo.
Mradi gani mkubwa aliouzindua Ambao umeanzishwa na mtangulizi wake na hakuwataja. Uwanja wa mpira wa taifa kwa heshima ya Mkapa akauita uwanja wa mpira wa Mkapa
 
Back
Top Bottom