Wanabidii: Mamuruki wa chadema/fanatics wa Zitto
Na, <bongotz.com>
Kwa muda mrefu, vyombo vya habari Duniani kote (Televisheni, Magazeti, Majarida, redio, Tovuti) vimekuwa ndio chanzo kikubwa cha kufichua watenda makosa wa Idara nyingine za serikali na kuhakikisha kuwa hazifanyi mambo ambayo hazitakiwi kufanya. Hili tumelishudia sana katika nchi zilizoendelea. Kadhia ya miaka ya sabini (70s) ya
Watergate iliyomlazimisha Rais Richard Nixon kujiuzuru ni mfano mzuri wa kutizamwa.
Ingawa kumekuwepo na ongezeko la Vyombo vya habari nchini, kinachosikitisha ni kwamba, vyombo hivyo (aidha kwa kutokujua wajibu wao) vimeshindwa kabisa kukidhi maridhio yao na badala yake vinatumia vitisho/matusi kuhakikisha kwamba wale wote wasiokubalina na mitizamo yao (walio na mawazo tofauti), hawatoi maoni yao kupitia vyombo hivyo. Kundi la Wanabidii ni mfano mzuri wa kutizamwa.
Hivi karibuni kulizuka mjadala kwenye forum ya Wanabidii kuhusu hoja ya kutenganisha uchaguzi wa urais na wabunge. Maada ambayo ilichangiwa na watu wengi akiwemo mbuge wa Kigoma-kaskazini, Zitto Zuberi Kawe, mhariri wa gazeti la Tanzania Daima (Absalom Kibanda), Managing Editor,
The Gurdian on suday (Richard Mgamba); na Excecutive Editor,
Tanzania Media Women's Association (TAMWA)-- Ananilea Nkya. Katika kuchangia mada hiyo, Zitto alikurupuka (a rookie mistake), na kutoa mifano mbalimbali (basically, mifano ya kitoto) ikiwemo Rwanda ambapo rais anakaa madarakani miaka 7 na wabunge miaka 5. Akaenda mbali kidogo na kutoa mifano ya nchi za dunia ya kwanza kama vile marekani ambapo rais anakaa madarakani miaka 4, maseneta miaka 6, na members of congress (wabunge) miaka 2. Kwenye hitimisho la mjadala, Zitto akesema (kwa ki-inglish), nami namnukuu, " I would go for 6 years Urais and 4 years Ubunge.
Siku iliyofuata, gazeti la Tanzania Daima likaandika habari kulingano na alichokisema Zitto kichwa cha habari kikisomeka, "Zitto: JK aongezewe Muda". Baada ya hapo, Zitto na wafuasi wake (Wanabidii); Richard Mgamba, pamoja na Ananilea Nkya wakaanza kumshambulia mhariri wa Tanzania Daima ndugu Absalom Kibanda huku wakidai gazeti lake (Tanzania Daima) limuombe radhi Zitto. Kwa ushujaa wa pekee, ndugu Kibanda akajbu na kusema, "hatutarajii kufanya hivyo!" Baadhi ya wanabidii wachache (foward-thinking people), wakaandika maoni yao wakimuunga mkono ndugu Kibanda kitu ambacho kiliwakera mamuruki wa Chadema na mafanatics wa Zitto wanaoendesha forum ya Wanabidii na kuanza kumshambulia kila mtu aliyeonekana kutofautiana nao kiitikadi. Wengi wakakasirika na kutaka mjadala huu ufungwe eti kwasababu tu sisi tulio wachache hatukukubaliana na matakwa ya walio wengi (wafuasi wa Zitto). Maoni yetu yakawa blocked/deleted, na wakaanza kututukana na kuturushia vijembe.
Penginepo tu labda niwakumbushe Wanabidii kuwa, uhuni na vitisho vinavyoendeshwa na forum yao, ni kinyume kabisa na katiba ya nchi yetu: Ibara ya kumi na nane (18) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inaeleza waziwazi kwamba: [1] Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati. [2] Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbali mbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.
Chini, nimeambatanisha maoni ya mwanabidii mmoja [Kevin Makyao] ambaye aliandika na kufafanua kwa kina kuhusu nilichoandika/sema:
"Wanabidii naona baadhi yenu mnakuwa wakali kiasi cha kutia wasiwasi ikiwa hapa ni jukwaa lililo tofauti na wale tunaowaeleza kwamba wameshindwa. Linageuka kuwa jukwaa la kuzuia kisima cha fikra. Linakuwa jukwaa la kushindwa kuvumiliana lakini baya zaiidi linakuwa jukwaa la kutaka vikwazo dhidi ya uhuru wa kutoa maoni. Hoja ya kutaka kuombwa radhi kwa kutumia maelezo ya humu ndani ni potofu kwa sababu chache rahisi kabisa.
[1]. Ili iwe umetumia maelezo ya mtu bila halali unatakiwa kuwa umechukua maelezo fulani na kudai ni ya kwako.
[2]. Sheria mama ni katiba. Kama kanuni ya Wanabidii inazuia watu kutumia uhuru wa kikatiba wa kukusanya na kusambaza habari au maoni ni kukiuka katiba. Nitashangaa sana kama wanabidii mnakubaliana na hilo.
[3]. Kama kwa namna yoyote ile kuna ukiukwaji wa haki miliki anayepaswa kulalamika ni yule anayeweza kuthibitisha kwamba haki miliki yake imetumiwa isivyo. Katika hili Wanabidii hatuna haki miliki ya chochote kilichopo jukwaani. sana sana aliyeandika ahangaike kututhibitishia kwamba ana haki miliki ya alichokiandika.
[4]. Habari inayolalamikiwa haijaonyeshwa popote ambapo ilinukuu kwa makosa chochote kilichopo ndani ya jukwaa. kama kuna makosa (jambo ambalo ni la mjadala) basi hayawezi kwa namna yoyote kuwa yamekuwa dhidi ya wanabidii.
[5]. Nani annafungwa na kanuni za Wanabidii? Gazeti ni "legal person". Je gazeti kama gazeti ni mwanachama wa Wanabidii? kama sio, unawezaje kulibana kwa kanuni ambazo kama kweli zipo zinawabana wanachama tu? Tutofautishe gazeti na Kibanda. Kibanda anaweza akaondoka Tanzania Daima muda wowote lakini uwajibikaji wa habari ile hautahama naye. Utabaki kwa gazeti, mwandishi na mhariri atakayechukua dawati. Tufikirie nje ya boksi.
[6]. Wanabidii wanapoteza nini kama Zitto asipoombwa radhi au wanabidii wasipoombwa radhi?
[7]. Tunawezaje kujidai tunataka kuwasaidia watanzania ikiwa tunataka yanayojadiliwa humu yabaki "siri" ya wanachama? Tuna wanachama wangapi na taifa hili lina watu wangapi? (Milioni 40). Ni vigumu kufikiria eti mnaweza kujadili mambo yatakayoleta mabadiliko kwa taifa mkiwa kikundi cha watu wasiofika mia na hamtaki manachojadili kisambazwe kwa wengine. kama kuna upotoshaji katika kusambaza, basi suluhisho ni kutoa habari sahihi. nani kati yenu amejaribu kutoa kwa umma kukweli wa kile anachokifikiri kuwa kimepotoshwa?
[8]. Hivi ni kweli kwamba kila ukijadili watu una makosa? Unaweza kuzungumzia mauaji ya wayahudi bila kumjadili Hitala? Unaweza kuzungumzia mauaji ya halaiki ya Rwanda bila kumjadili Juvenal Habyarima na viongozi waandamizi wa Interahamwe kama akina Chezinga? Unaweza kuajdili ukristo bila Yesu? Unaweza kujadili uislam bila Mohamed? Unaweza kujadili historia ya Tanzania bila Nyerere? Lazima tukubali wakati mwingine ili kupata maana halisi ya jambo lazima kujadili pia watu. Tusipumbazwe na huo msemo wa simple minds discuss personalities. Lazima tuupe maana huo msemo. Kuna wakati hutapata maana ya tukio bila kumjadili aliyefanya tukio.
[9]. hata wale wanaosema mjadala ufungwe wanatumia lugha ambayo inaita watu kutoa maelezo. huwezi kusema mjadala ufungwe kisha ukasema eti hata katika ujinga kuna cha kujifunza. Waswahili wanasema fumbo mfumbe mjinga, mwerevu atalielewa. Bila shaka kama mjadala ni wa kufungwa lazima ufungwe kwa kauli ambazo haziiti maelezo ya ziada.
[10]. Kwa kuandika habari hii ni maslahi ya nani yanaweza kusemwa kiukweli na kwa kumuogopa Mola wako yamekiukwa? Sio kila kosa linahitaji kubebewa bango. Wakati mwingine lazima kuangalia gravity of the harm.
Jambo moja la msingi ni kwamba nimeshangaa sana kuona watu ambao hawako tayari kujeruhiwa kwa namana yoyote. Lazima tukumbuke siku zote kwamba hakuna utukufu bila mateso. yeyote anayetaka kweli kuleta ukweli lazima awe tayari kwa michubuko. Hata fizikia inatufundisha kwamba bila ukinzani hakuna mjongeo (no movement without friction.) kama tunataka kuayamaliza haya mambo basi tuyamalize bila vijembe..."
Mungu ibariki Tanzania!!