TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

Hiyo call detail haitasaidia unless iwe na content ya hayo mazungumzo, ambayo sidhani kama kampuni ya simu inayo. Inawezekana huyo bw. mawenge akawa kweli ndiye aliyempigia na wakazungumza. Hiyo sio ishu maana hata mimi nikikupigia sasa hivi japo huijui namba yangu utapokea na tutaongea. Nikidai baadaye kwamba ulinidai rushwa?

Labda watoe call details za mwezi mzima waangalie kama hizo namba zao zimekuwa zikiwasiliana frequently - implying kwamba likely walikuwa wanajuana kwa muda. Maana huwezi kupiga mara moja na kuomba rushwa hapohapo.

Unafikiri tuna jeshi lenye akili ya kufanya investigation kama hizi basi? We acha tu.
Si hapo sasa! Hebu kwa mara ya kwanza katika mahakama zetu Tanzania tuone ushahidi wa simu unavyoweza kutumika kutoa tafsiri isiyoleta mashaka kwa umma!
 
Ah hapo mheshimiwa tulipitiwa kidogo ila hata hivyo mheshimiwa tulifanya vizuri kwenda kwani tulimkamata mshtakiwa akiwa na pingu garini
Hakimu: Je pingu hizo zinahusika vipi na mashtaka?
Mashtaka: Mpaka sasa hatujawezakuilink kisawa sawa bwana hakimu lakini mshtakiwa haruhusiwi kumiliki pingu
Hakimu: Sheria inasemaje juu ya hilo?
Mashtaka: Ah........... hebu ngoja kidogo Bwana hakimu tuconsult sheria zetu ila inaonekana kuwa hakuna sheria inayokataza ila tu huwa hatuuzii pingu kwa raia
Hakimu: Jibu swali bwana mashtaka, sheria inaruhusu au hairuhusu?
bado masaa tu, naona mwisho wa Kova kuwa mkuu wa Police kanda maalumu ya Dar es salaam ukikaribia, naiona aibu yake haiko mbali....shitaka jepeesi.......
 
Ushaidi wa kimazingira ni kama ifuatavyo:

1. Kamera yake ilikuwa na nyumba za jamaa mhasibu anazojenga Morogoro so Jerry alikuwa anamchunguza

2. Walionekana wote na CCTV hotelini ambako Jerry alikana kwenye maelezo yake kuwa hamjui jamaa

3. Mhasibu alisema wazi kuwa ndani ya gari la Jerry kuna nini (pingu, bastola)

4. Miwani ya mhasibu ilikutwa ndani ya gari la Jerry inaonyesha kimazingira walishakutana jambo ambalo jerry alikana.

Jerry alikurupuka, laiti angesema alishamuona mahali au jana yake huyu mhasibu na wakakaa meza mmoja, maana unaweza hotelini kukaa meza moja na mtu usiemjua hasa kama CCTV kamera ikionyesha kulikuwa kumejaa..ANGEKUWA HANA KESI YA KUJIBU KABISA.

Yeye Jerry ndo amekaribisha ushahidi wa kimazingira.

Tatizo alishavimba sana bichwa....linaelekea kupasuka sasa.
 
lets hope mahakama itatenda haki juu ya tukio hili la aina yake 2010
 
Shishye
Ni kweli hakuna uwezo wa kustore information za mazungumzo but kama Jerry anakumbuka muda aliopigiwa kuitwa kwenye tukio ni rahisi kujua simu iliyoingia muda huo kwa Jerry na mmiliki then akamatwe awe shahidi kwani ni wazi Jerry aliitiwa tukio 'hewa' ambalo alipoitikia wito kwenda akajikuta yeye ndo amekuwa tukio la kutolewa magazetini.

Akipatikana huyo mtu aulizwe motive ya kuita mwandishi wa habari kwa tukio hewa pale City Garden.

Pili frequency za mawasiliano ya Muro na bwana Mawenge zitajulikana pamoja na hao kina Kapanini sijui!
 
Je ni kwanini police wamelivalia njuga kiivyo?sipati picha kamili

Hii nchi inatawaliwa na itikadi ya kijambazi, kifisadi. Yeyote atayekwenda kinyume na itikadi hii lazima ashughulikiwe - anapingana na dola. Ndio maana kiongozi kama wa kanda maalum haogopi kutamka mbele ya umma maneno ya uongo wa wazi anayojua fika hayana uthibitisho na asiogope wakuu wake wanaweza kumchukulia hatua za kinidhamu. Katika hali ya kawaida, jeshi lingewajibishwa kwa kuwafanyia wananchi vitendo viovu pale inapothibitika lakini hapa kwetu ni kinyume. Ukifanya madudu unalindwa. Ukitetea haki siku unatishiwa usalama hata kuuawa. Fuatilia historia. Tujitokeze wengi kama Jerry kusimamia ukweli ili kugeuza mambo.

Inatakiwa watu tuandamane, wanasiasa wapinzani wapaze sauti kukemea pindi vitu kama hivi vinapotokea.
 
Ushaidi wa kimazingira ni kama ifuatavyo:

1. Kamera yake ilikuwa na nyumba za jamaa mhasibu anazojenga Morogoro so Jerry alikuwa anamchunguza

2. Walionekana wote na CCTV hotelini ambako Jerry alikana kwenye maelezo yake kuwa hamjui jamaa

3. Mhasibu alisema wazi kuwa ndani ya gari la Jerry kuna nini (pingu, bastola)

4. Miwani ya mhasibu ilikutwa ndani ya gari la Jerry inaonyesha kimazingira walishakutana jambo ambalo jerry alikana.

Jerry alikurupuka, laiti angesema alishamuona mahali au jana yake huyu mhasibu na wakakaa meza mmoja, maana unaweza hotelini kukaa meza moja na mtu usiemjua hasa kama CCTV kamera ikionyesha kulikuwa kumejaa..ANGEKUWA HANA KESI YA KUJIBU KABISA.

Yeye Jerry ndo amekaribisha ushahidi wa kimazingira.

Tatizo alishavimba sana bichwa....linaelekea kupasuka sasa.

Umejibu vema FP na nimeelewa maana ya ushahidi wa mazingira.
Hata mimi sikumuelewa Jerry aliposema hamfahamu kabisa bwana Mawenge and yet wanadai camera ya CCTV iliwaonyesha wakiwa pamoja.

Hilo la miwani angewezasema kawekewa na polisi. Asipoangalia itakula kwake!
 
Mheshimiwa Hakimu: Ndugu Mawenge ukiwa kama shahidi wa kesi hii je unasema kuwa mshitakiwa alikulazimisha umpatie kiasi cha pesa
Mawenge: Ndiyo Mheshimiwa
Hakimu: Je mshitakiwa alitaka kiasi gani? na alijitambulisha kama nani?
Mawenge: Milioni 10 na alisema yeye ni afisa wa Takukuru
Hakimu: je rushwa hiyo ilitakiwa kwa ajili ya nini? Kwa sababu inafahamika kuwa mtu huwa anatoa rushwa pale anapohitaji kupewa huduma flani, je wewe ni huduma gani uliyoitaka kutoka kwa mshtakiwa hadi akuombe rushwa?
Mawenge: Alisema ili asinitoe kwenye vyombo vya habari kama fisadi
Hakimu: Je wewe ni fisadi?
Mawenge: Hapana mimi si fisadi, mwulize hata mke wangu mimi si fisadi kabisa bwana hakimu
Hakimu: Sasa kama wewe si fisadi kwa nini ulikubali kutoa rushwa? kwa nini usimpuuze tu kwa sababu hata akikutoa kwenye vyombo vya habari wewe si fisadi.
Mawenge: Ndio maana mheshimiwa hakimu nikaenda kumripoti polisi
Hakimu: Wewe ulikuwa mtumishi wa uma, je masuala ya rushwa huwa yanaripotiwa polisi au TAKUKURU? na je uliporipoti polisi, walikupatia pesa za moto ambazo ulitakiwa kumpa mshitakiwa?
Mawenge: Ah bwana Hakimu, unajua, kule kwetu Bagamoyo huwa hatujui tofauti kati ya polisi na TAKUKURU tunachojua wote ni polisi tu!! ...................


Ah kumbe naota mchana.!!
Senior Officer wa serikali anayefanyakazi bagamoyo mkoa wa pwani [siyo biharamulo]eti haju tofauti kati ya polisi na takukuru tehe tehe tehe.
Kwa vile jamaa ameondolewa hapo ofisini kutokana na ubadhirifu isije ikawa anajihami fulani ili asichunguzwe kwa vile amesaidia******
Lakini mwisho wa siku tutajua chuya ni ipi na mchele ni upi
 
JF kwa kutetea wahalifu ambao huko nyuma walijifanya wapiganaji ndiyo yenyewe. Ukifanya kosa jua mahakama inakusubiri. Watanzania wengi ni wala rushwa tu ila wengi hawajapata nafasi tu. Muro ni mwakilishi wetu, ambaye baada ya kupata umaarufu kazini, akaamua kutumia nafasi hiyo kujitajirisha.

Tupige kelele kwamba wahalifu wengine kama akina Chenge mbona hawafikishwi mahakamani? Lakini ambacho tunafanya makosa ni kuwatetea wale wapenzi wetu hata pale wanapofanya makosa.

Ukiwa unapigana na makosa lazima wewe ndio uwe wa kwanza kuhakikisha huna kosa.

Tulaani matendo mabaya bila kujali yamefanywa na nani.

Kwenye hili wacha vyombo vya sheria viamue kama jamaa ana makosa au la.

Ila mwandishi wa habari kukutwa na pingu, hapo mimi nimebaki hoi. Bastola sawa, labda alitaka kujilinda, lakini pingu? Mmmm!!! Mungu ibariki Tanzania.
 
lets hope mahakama itatenda haki juu ya tukio hili la aina yake 2010

Hivi ni mahakama ileile iliyomwachia huru yule polisi aliyeamuru wafanya biashara wa madini kuuawa kwa jina la majambazi? Au ni ileile ambayo kwa miaka mitano sasa haijamhukumu hata mmoja wa wale waliokula mabilioni ya EPA? Nikumbushe pliz.
 
Hivi ni mahakama ileile iliyomwachia huru yule polisi aliyeamuru wafanya biashara wa madini kuuawa kwa jina la majambazi? Au ni ileile ambayo kwa miaka mitano sasa haijamhukumu hata mmoja wa wale waliokula mabilioni ya EPA? Nikumbushe pliz.

Ni hiyohiyo mahakama inayokumu maskini waliosutana kila kukicha!!! Nani alisema kuna haki katika nchi maskini??

Na hao mahakimu ndio badae wankua majaji
 
safari ya kutafuta utawala wa haki ni ndefu lazima wapo watakaotolewa kafara lakini iko siku moja damu zao ndio itakuwa chachu ya ushindi kwa waliobaki" by tryphone 2010
 
.......Serikali ya Tanzania ni zaidi ya unavyoijua, sasa hivi hali inatisha kwa sisi vijana maana kuna wazee waliokalia nchi ambao wamekalia uozo na hawataki kuuondoa.
Mtoto mdogo ukitaka ufuate haki itendeke utastukia unabebeshwa kesi isiyokuwa na mbele wala nyuma........kwa mtindo huu sijui tutaishia wapi.
 

Muro+akitoka+mahakamani+baada+ya+kupata+dhamana.JPG

Jerry Muro akipoza koo baada ya kuachiwa kwa dhamana leo
Jerry Muro na Edmund Kapama
walitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa.
Mwenza Ngassa amepelekwa rumande.
 
Anaenuna anune anaecheka acheke bwana Muro kwa namna moja ama nyingine lazima atakua anajihusisha na makundi ya kihalifu.Hata kama inaruhusiwa kisheria mtu yeyote kumiliki pingu mwanahabari na pingu wapi na wapi?alizinunua kwa ajili gani?self defence or what?haiingii akilini,hata panga,kisu,shoka n.k mtu yeyote anaruhusiwa kumiliki lakini nadhani kila mtu atakushangaa ukionekana unatembea na shoka mitaani wakati huonekani kuwa na shughuli yeyote inayohitaji uwe na shoka!!

Pole sana, Just simple logic unafikiri pingu inamsaidia mtu kufanya uharifu gani.
Ukiwauliza waharifu wa list zana wanazotumia , unategemea watalist pingu.
Jamani, mbona watu hamna hata aibu. Kama mtu una personal problem na Muro, tafuta jinsi ya kuziendeleza kama ni mihimu otherwise, mara nyingi ubaya na kinyongo juu ya mtu humrudia mtu mwenyewe.
 
Senior Officer wa serikali anayefanyakazi bagamoyo mkoa wa pwani [siyo biharamulo]eti haju tofauti kati ya polisi na takukuru tehe tehe tehe.
Kwa vile jamaa ameondolewa hapo ofisini kutokana na ubadhirifu isije ikawa anajihami fulani ili asichunguzwe kwa vile amesaidia******
Lakini mwisho wa siku tutajua chuya ni ipi na mchele ni upi

Anajua tofauti kati ya PCCB na Police, ila PCCB ndio ambao walimwondosha ofisini na jamaa akatake advantage ya kummaliza kabisa! So he can't go back to PCCB they will just conclude their case on him.
 
Ametoa dhamana ya sh Milioni 5 na Wadhamini wawili.Kesi yake itatajwa tena tarehe 12 Mwezi huu.Cha kushangaza Amefunguliwa mashtaka mawili tu kwa sasa la rushwa lakini la pingu halijatajwa wanadai wanafanya uchunguzi kwa kuwa ameshakabidhi risiti.
 
Back
Top Bottom