TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

Wakuu kijana anatinga mahakamani leo, ni kisutu au ilala. Wenye nguvu mkamuwekee dhamana
 
Jamani tukubali kuwa hapa ndio tunazidi kuielewa Tanzania yetu. Kwani vitu vingi katika nji vimekaa vibaya. Sheria nyingi hazijakamilika. Ignorance ni kubwa sana katika nji hii.

Kuna watu wamefaidika sana na hii mianya ya watu kutokujua mambo.
 
Pingu zinatumika hasa kwa wazungu na wengineo katika kufanya mapenzi, kuna wanawake mpaka watiwe pingu ndiyo wanasikia raha, hali kadhalika wanaume wengine pia hivyo hivyo. Kwa hiyo pingu zina matumizi ya kila namna.

Lakini pia Jerry kazi aliyoifanya dhidi ya polisi ni ya hatari sanaaa, kuwa na pingu ni kitu kizuri tuu.
And who knows my be Jerry ni mtu wa USALAMA WA TAIFA!!!! Yoteee yawezekana.
Nadhani kuna namna ya kuwasaidia watu hawa wa Usalama pindi wanapokamatwa na police wakiwa kazini- either mkuu wao anawasiliana na police na mhusika kuachiwa kitu ambacho hakijafanyika kwa Jerry otherwise sioni mantiki ya kuhojiwa juu ya pingu kama anafahamika kuwa ni Usalama.

Hii kesi bwan aina vificho vingi tu- Kova naye amechukua jukumu la PCCCB na bado amevunja sheria ya PCCCB ya kuwatangaza hadharani majina ya watoa rushwa jamani huu kweli ni usiku wa giza
 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameagiza uchunguzi kuhusu sakata la mwandishi wa habari, Jerry Muro, anayetuhumiwa kwa rushwa na kukutwa na pingu, ufanyike kwa kina na haraka ili ukweli ubainike, badala ya suala hilo kuendelea kuibua hisia mbaya miongoni mwa wananchi
Asee yani mpaka sasa sielewi kama kuwa na pingu ni kosa au la!!
 
Kweli Tanzania ni nchi ya amani...au watu mnataka kuwafunga mapingu wakezenu ana watoto wenu wanapowakosea?


Mkuu hata mimi nilitaka kuuliza swali kama hilo,kwa nini unataka kumiliki pingu ili watoto wakikukorofisha uwafunge na kuwapatia kibano wakiwa hawawezi kufurukuta au? Nini hasa lengo la kutaka kumiliki pingu? Hata kwa Jerry Muro nimejiuliza sana hiyo pingu kwake ni ya nini?
 
Mbona kwenye "Citizen" ya leo Imememnukuu afisa wa duka la Mzinga lilopo Ppanga kwamba wao huwa hawamuuzii mtu binafsi pingu ispokuwa polisi na magereza tu? Hii inakuwaje mbona mnatuchanganya?
 
Pamoja na kuwa sheria haimkatazi raia kuwa na pingu, jamani tujiulize hasa pingu hizi Jerry alikuwa anamiliki kwa sababu gani hasa kiundani, na zaidi ya yote kwa nini alitembea nazo kwenye gari siku hiyo? je katika kazi yake ya uandishi wa habari huwa wanakutana na purukushani ambazo huwenda zingehitaji matumizi ya pingu hizo?

Tusikimbilie kusema sheria haikatazi yeye kama raia kuwa na pingu but tukumbuke kuwa pingu si sawa na maji ya kunywa kuwa ni muhimu kuwa nazo (unless alikuwa na specific matumizi nazo) na atueleze matumizi hayo, na kwa nini siku hiyo zilikuwa garini?

Kuna mijadala mingine huwa tunairefusha pasipo hata sababu za msingi! Thibitisheni kwanza kama muro si usalama wa taifa halafu ndiyo muendelee na mjadala wa yeye kutembea na pingu. Kama raia wa kawaida, kwa nini auziwe pinu kihalali na awe anatembea nazo? Usalama wa taifa wao wenyewe kwa wenyewe hawajuani, uje iwe wewe raia? Ni evident kwamba huyu bwana ni usalama wa taifa, wapo mpaka wafagiaji wanapita kufagia maofisini kwetu. KALAGABAHO!
 
Mwanakijiji hakuna aliyesema ni kosa tumeelewa kuwa si kosa. Lakini mtu yeyote akiwa na kitu chake atakwambia kuwa anacho kwa sababu flani, silaha mtu anamiliki kwa kuwa anajilinda kwa usalama wake na pingu ni kwa ajili ya kufanyia nini? Sawa umesema kuna matumizi mengine ambayo pingu zinatumika huwenda sababu za Jerry zinaangukia ndani ya kundi hilo la sababu nyinginezo but why zilikuwa garini siku ile ya tukio? Sisemi kuwa Jerry ana makosa la hasha but najaribu kuwaza zaidi why atembee nazo siku hiyo? au huwa zinakaa ndani ya gari lake daima? Yeye mwenyewe anasemaje?

Mi bado haijaniingia akilini huwenda ni kwa sababu ya upeo wangu mfupi wa haya mambo lakini ninaamini kama ambavyo mmenijuza mengi hata hili mtanisaidia tu.

Muro is under no obligation whatsoever to explain to anybody kwanini alikuwa na pingu. Kama kuna kosa la kuwa na pingu wampeleke mahakamani na wathibitishe kuwa ni kosa.
 
Kuna mijadala mingine huwa tunairefusha pasipo hata sababu za msingi! Thibitisheni kwanza kama muro si usalama wa taifa halafu ndiyo muendelee na mjadala wa yeye kutembea na pingu. Kama raia wa kawaida, kwa nini auziwe pinu kihalali na awe anatembea nazo? Usalama wa taifa wao wenyewe kwa wenyewe hawajuani, uje iwe wewe raia? Ni evident kwamba huyu bwana ni usalama wa taifa, wapo mpaka wafagiaji wanapita kufagia maofisini kwetu. KALAGABAHO!

Usalama wa Taifa wa Tanzania hawatakiwi hata kuwa na pingu wala bunduki!
 
unaniangusha mkuu.. tatizo ni wale ambao waliamini maneno ya serikali! Tulisema mapema siyo kosa kumiliki pingu watu hawataki ati kwa vile Polisei wamesema.

Nadhani hawakusoma shairi la pingu ya mapenzi. Mimi binafsi nina pingu milioni moja na nimetengeneza mwenyewe na zina ubora kuliko wanazotumia polisi, zangu ni digito, unafungua kwa passcode, unafunga kwa kumrushia mtu mikononi, miguuni au begani. Polisi wakitaka waje nyumbani kwangu wanikamate.
 
Usalama wa Taifa wa Tanzania hawatakiwi hata kuwa na pingu wala bunduki!
MM,
Big NO na wala usijidanganye. Wewe mwenyewe hapo ulipo uko eligible kuwa navyo, usalama wa taifa yuko entitled, ungesema usalama wa taifa hawatakiwi kuonekana navyo hadharani kama ilivyo kwa polisi na jwtz, n.k. Ndiyo maana hata Muro alikuwa hajawahi kuonekana na pingu mpaka siku alipokuja kupekuliwa na polisi, hata polisi wenyewe walikuwa hawajui kama alikuwa akimiliki pingu. Hiki ktu kiko so obvious to the extent hakihitaji hata kuendelea kukijadili. Tuletee mada nyingine hot, hasa za uchaguzi tujadili hizo!
 
02/04/2010

Kadhia anayoendesha kwa mbwembwe Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuhusu mwandishi wa habari za uchunguzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Jerry Muro, imezidi kumweka pagumu baada ya risiti ya pingu anayotuhumiwa nayo mwandishi huyo kupatikana.

2909552.jpg
nakala ya stakabathi ya malipo ya pingu alokutwa nayo Jerry Muro​


Hali hiyo inajitokeza baada ya kile alichoapa Kova kwamba hakuna raia anayeweza kumiliki pingu, na kwamba alikuwa na hakika kwamba Muro asingeweza kupeleka risiti hiyo. Juzi akiendelea na juhudi zake za kuwakamata watuhumiwa na kuwahukumu huku akisema wengine ni "matapeli sugu", Kova alisema kwamba Muro aliyekamatwa Jumapili iliyopita na kuachiwa kwa dhamana, alikuwa hajawasilisha risiti hiyo.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kwamba Muro alinunua pingu hiyo kihalali kutoka duka la kuuza silaha la Shirika la Mzinga. Shirika hili ni mali ya serikali. Nipashe imefanikiwa pia kuona risiti aliyopewa Muro kama ushahidi wa ununuzi wa pingu hiyo, ikiwa na namba 34357310. Stakabadhi hiyo ni mali ya serikali pia. Risiti hiyo iliyotolewa Mei 20, mwaka 2008, inaonyesha kuwa Muro alinunua pingu kwa Sh, 25,000. Muro ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kufichua aina tofauti za rushwa, Jumapili iliyopita alikutwa na pingu katika gari alilokuwa akilitumia mara baada ya kukamatwa kwa kudaiwa kutaka fedha kwa njia ya vitisho kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Wage.

Wage pamoja na maofisa wa juu wa Halmashauri hiyo mwezi uliopita walifutwa kazi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa tuhuma za ufisadi wa kutisha. Bado wanachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Miongoni mwa rushwa ambazo Muro alizifichua ni zile zilizohusu askari wa usalama barabarani kupokea rushwa.



8772229.png
Jerry Muro​


Kwa mara ya kwanza Muro alifanya kipindi maalum akiwa mfanyakazi wa ITV na kuwanasa askari hao katika barabara kuu ya Morogoro, kati ya Dar es Salaam na Morogoro. Mara ya pili alifanya kipindi cha usiku wa habari katika barabara kuu mkoani Iringa na kilionyeshwa na TBC1 anakofanya kazi Muro kwa sasa.

Mwaka jana Muro alishinda tuzo ya mwandishi bora wa mwaka na kipindi cha ITV ambacho kilisababisha askari kadhaa walioonekana wakipokea rushwa kufukuzwa, ndicho kilimpandisha ngazi.

Kadhalika kipindi cha TBC1 nacho kimepeleka kilio kwa askari waliomulikwa, na sasa wanachunguzwa kabla ya kufukuzwa kazi kwa kula rushwa.

Kamanda Kova tangu kuibuka kwa kadhia ya Muro ambayo imeacha maswali mengi kutokana na kuendeshwa mno kwa mizengwe, amekuwa akikanyaga sheria ambazo kama kiongozi wa juu wa Jeshi la Polisi anapaswa kuzisimamia. Kwa mfano Jumatatu Kova alionyesha hadharani bastola anayomiliki Muro kama ambavyo polisi wengi wamekuwa wakionyesha silaha walizokamata kwa watu wanatuhumiwa kwa ujambazi. Ingawa Kova alikiri kwamba Muro alikuwa anamiliki bastola hiyo kihalali, hakueleza umma ilikuwa na umuhimu gani basi kiutaalam na kiusalama kutoa taarifa za kina za silaha ya raia, ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa kubeba risasi na ilikotengenezwa. Kadhalika, Kova alionekana akijenga hoja kwamba pingu aliyokuwa anamiliki Muro ilikuwa inatiliwa shaka na kukiwa hakuna sheria yoyote Tanzania inayomzuia mtu kumiliki pingu, kifaa hicho si silaha wala hakina ukiritimba wowote wa kukimiliki. Kova pia anadaiwa kuvunja sheria ya Takukuru ya mwaka 2007 kwa kuwataja watu waliotoa taarifa za rushwa, hivyo kuweka suala zima katika mtihani mkubwa wa kisheria. Kifungu cha 51(1) (a) cha sheria hiyo, kinazuia kutajwa kwa jina, makazi na anuani ya mtu aliyetoa taarifa kuhusu vitendo vya rushwa au aliyesaidia mamlaka inayohusika kufanikisha kukamatwa kwa mhusika.

Juzi Kova aliwaanika watu wengine wawili aliodai kuwa ni washirika wa Muro katika kutenda uhalifu, na aliwatangaza kwamba ni "mapateli sugu wasiostahili kupewa dhamana". Kova aligeuka kuwa Polisi na Hakimu wa kuhukumu papo hapo. Kadhia ya Muro imekuwa ikibadili mwelekeo kila uchao, awali polisi walikuwa wanamtuhumu kwamba alidai rushwa ya Sh. milioni 10, lakini wameshindwa kueleza ni kwa nini hawakuweka mtego ili kumshikisha na pia ni kwa nini suala hilo halikupelekwa Takukuru ambao kisheria ndio mahali hasa pa kushughulikia makosa ya rushwa.


Jana nipashe iliwasiliana na uongozi wa Shirika la Mzinga ambalo linauza pingu hapa nchini, na ulisema upo tayari kumuuzia hata mwandishi kama anazo fedha. "Wewe kama una hela njoo tutakuuzia pingu, haina shida tatizo lipo katika silaha," alisema Mary Peter, mfanyakazi wa shirika hilo alipoulizwa na Nipashe, jana jioni. Mary alipoulizwa kama anakumbuka Muro aliwahi kununua pingu kwao, alijibu kwa kifupi kuwa yeye sio msemaji wa shirika hilo.

Habari kwa mujibu wa gazeti Nipashe na Picha ni kwa mujibu wa wavuti.com na blogu ya Mroki

What was the real motive from Kova?
Alionyesha silaha ya Murro hasarani na kiasi cha risasi inayoweza kuchukuwa, je kesho mtu akitokea tu na kusema Jerry kanitishia na silaha, kisa tu anajua anamiliki silaha Jeshi la Polisi (JLP) watasemaje?
Kama silaha inamilikiwa kihalali kwanini iwe "displayed" kwa umma? Je hii haileti wasiwasi kuwa hata zile silaha wanazoonyesha kila siku ni zile za miaka nenda rudi na wanaonyesha tu ili "ku-justify" killing waliokwisha fanya?
Hizi silaha wanazonyang'anywa majambazi ziko wapi? Mbona hatujawahi kusikia yameteketezwa?
Umma tukiamini kuwa JLP ndiyo wanaokodishia raia au majambazi silaha, je haiyamkiniki?
Sasa receipt ya pingu imepatikana na imenunuliwa kihalali wakati Kova kesha sema ni kinyume cha sheria. Alaumiwe nani?
Nani kadanganya na kupotosha umma? Kama Kova amedanganya na kupotosha umma wakati yeye ni kiongozi mwandamizi wa JLP, nini kitaisafisha JLP?
Hii ni kama tamthilia, tusubiri "episode" nyingine.
 
Kuna mijadala mingine huwa tunairefusha pasipo hata sababu za msingi! Thibitisheni kwanza kama muro si usalama wa taifa halafu ndiyo muendelee na mjadala wa yeye kutembea na pingu. Kama raia wa kawaida, kwa nini auziwe pinu kihalali na awe anatembea nazo? Usalama wa taifa wao wenyewe kwa wenyewe hawajuani, uje iwe wewe raia? Ni evident kwamba huyu bwana ni usalama wa taifa, wapo mpaka wafagiaji wanapita kufagia maofisini kwetu. KALAGABAHO!
makanyaga aksante kwa post yako kali. Ni kweli usemayo na hakuna anayebisha kama ulivyosema hapo kwenye post yako kuwa si rahisi sisi kama raia wa kawaida kuwajua usalama wa taifa so tunaombwa kujulishwa kama inawezekana kama Jerry ni usalama au la. Kama haiwezekani kwa sisi kujulishwa basi usalama wenyewe wawasiliane na police kwa siri ili hili suala la kumiliki pingu liondolewe kwenye masikio yetu maana likiachwa hivi ndilo linalopelekea sisi kuhoji pasipo kuwa na hoja za msingi kama unavyosema.

Hapo kwenye blue: Aksante
 
Muro is under no obligation whatsoever to explain to anybody kwanini alikuwa na pingu. Kama kuna kosa la kuwa na pingu wampeleke mahakamani na wathibitishe kuwa ni kosa.
Mwanakijiji uko right Muro hana obligation yoyote kuexplain matumizi ya pingu zake but under special circumstance kama hiinadhani anatakiwa unless kuna siri (mf. ni usalama wa taifa na hairuhusiwi kujitangaza) but kama suala la kipolisi police wanatakiwa wajulishwe hilo la Jerry kuwa usalama ili waondoe suala hilo na kuclear the air ama sivyo basi tusingekuwa na obligations za kupekuliwa majumbani kwetu wala kuexplain any umbiguous situations tunazokutwa nazo. Nadhani inapotokea kitu ambacho kina utata tuna obligation ya kutoa explaination.

Umesema na inasemekana si kosa kwa raia kumiliki pingu yet wanadai huwa hawaziuzi kwa raia -so ni kwa nini hawauzii raia wakati haikatazwi kumiliki pingu? does it come into their heads?
 
Huyu Kanali angetutajia basi kifungu cha sheria kinachosema ivyo.....

Angekwambia kifungu X (1) na YRP # $ (7) Ni marufuku kunifukuzia vijana/mawakala wangu wanaonikusanyia pesa barabarani ndani ya Tanzania hii kwa wakati wowote kwani kufanya hivyo ni kuua familia yangu na mke wangu na kifungu PF kinaongeza kuwa

Hivi watanzania mnajua kuwa ni utaratibu wa kawaida matrafiki hulipa kiwango fulani kila mwezi kwa hawa wakubwa ili wabaki hapo walipo? hii vita si ndogo kwani Jerry kawagusa wakubwa bila kujijua
icon5.gif
 
makanyaga aksante kwa post yako kali. Ni kweli usemayo na hakuna anayebisha kama ulivyosema hapo kwenye post yako kuwa si rahisi sisi kama raia wa kawaida kuwajua usalama wa taifa so tunaombwa kujulishwa kama inawezekana kama Jerry ni usalama au la. Kama haiwezekani kwa sisi kujulishwa basi usalama wenyewe wawasiliane na police kwa siri ili hili suala la kumiliki pingu liondolewe kwenye masikio yetu maana likiachwa hivi ndilo linalopelekea sisi kuhoji pasipo kuwa na hoja za msingi kama unavyosema.

Hapo kwenye blue: Aksante


Wakuu ni vigumu na kamwe haitakuja kuellezwa kazi ya Ndugu yetu Muro zaidi Ya uandishi wa Habari.Hata wewe mwanajamii unaweza kuwa usalama wa Taifa baba yako na mama yako wa kukuza wasiweze kujua chochote.Sema alichokifanya kova alikosea kumhukumu mtu bila kujua kazi yake na kama alikuwa anajuwa kuwa si rahisi raia yeyote kumiliki pingu basi alitakiwa kujiridhisha kabla ya kuwasiliana na waandishi wa habari.Haya Muro kawasilisha receipt halali huoni kwamba amejiharibia kutoa matamshi ambayo hajayafanyia uchunguzi na kuyatoa kwa waandishi wa habari?Je anafaa kuwa kiongozi?

Kiongozi wa ngazi ile anatakiwa kuwa Confidentiality na awe Trustworth sasa yeye haoni kuwa anaanza kupublisize vitu ambavyo havikutakiwa kutolewa njee ya pazia??

Na kama ikilazimika kumuanika Muro basi itabidi wamvua hiyo hidden nyazifa ili awe raia ambaye haruhusiwi kumili pingu.

NOTE:Kuna mtu anayejua tabaka za kazi za usalama wa raia?Katika tabaka hizo ni nani anatakiwa kumili nini na mwingine hatakiwi?mfano waandishi wa habari wanaoambatana na Rais, waziri mkuu kwenye ziara mbalimbali ni usalama wa taifa au ni waandishi wa TSJ?

haya yote yamekuja kuvuja kipindi hiki enzi za mwalimu hata mwanao alikuwa anaweza kuwa anafanya kazi bila hata wewe ukiwa hujui.

Mwenye wasiwasi aniPM nimpe habari ili tuendelee na sredi zingine na kuiacha hii ya Muro ili vyombo husika viendelee kufanya kazi.
 
Back
Top Bottom