TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

Jana usiku niliangalia vipande vyote vilivyorekodiwa vye maelezo ya Jerry Muro na yale ya Kamanda Kova. Kwa kuangalia lugha ya mwili, nilimwonea huruma sana Jerry Muro. Yuko katika wakati mgumu, maana, katika yote mazuri aliyoifanyia jamii, kwa sasa yuko katika mtihani mgumu . Swa ni kwa namna gani ataibakisha imani na heshima ya jamii kwake?

Niandikayo hapa hayamhusu Kamanda Kova na Jerry Muro tu, huenda yana manufaa kwa jamii pana. Katika ulimwengu huu kuna waliotembea katika nchi nyingi. Na hufika wakati ukamsikia binadamu mwenzako akitamka kwa kujisifu: " Mimi nimezunguka karibu dunia nzima!". Asichokijua binadamu huyo ni ukweli kuwa huko kote alikokwenda ni kipande kidogo sana cha dunia hii. Ukiunganisha sehemu zote alizokanyaga mguu wake na kujionea kwa macho yake yaweza kuwa sawa na kipande ambacho Baba Gile wa kijijini Kalenga , Iringa amekanyaga na kujionea kwa macho yake. Naye atakwambia ametembea kwa miguu au kusafiri kwa baiskeli kwenda vijiji vya mbali sana na Kalenga anakoishi.

Ndivyo maisha yalivyo. Hapa duniani tunayoyajua ni machache sana kuliko tusiyoyajua. Kila mtu ana kipande chake anachokijua. Tukiunganishanganisha vipande hivi, vinakua, tunapata maarifa zaidi. La Jerry Muro limegeuka. Sasa lLinahusianishwa na tuhuma za utapeli, ni tuhuma nzito, ni kashfa. Jana niliandika juu ya kiu ya kutaka kufahamu ukweli. Ukweli mzima.

Na siku zote, ukweli udhihiri, huwa ni suala la wakati tu. Ukweli hauhitaji shahidi, husimama wenyewe. Mapinduzi ya teknolojia nayo yamepelekea wanajamii wengi kufuatilia yanayofanyika Dar na kwengineko. Pale kijijini Kalenga, katika kila wanakijiji kumi, wanne wana simu za mkononi. Katika kila kaya kumi, moja ina televisheni. Kasi hii ya mapinduzi ya upatikanaji wa taarifa inaendelea.

Vivyo hivyo, na hamu pia ya wanajamii kuutafuta na kuupata ukweli imeongezeka. Na maishani, jambo baya linalokuhusu wewe, liseme mwenyewe. Mfano, una mkeo nyumbani. Kazini unatembea na Katibu wako Muhtasi. Kuna siku mfanyakazi mwenzako atamwambia ukweli mkeo juu ya mahusiano yako na Katibu wako. Mkeo atakuweka kikaangoni na ushahidi. Utakiri kosa, utaomba msamaha. Nafasi ya mkeo kukusamehe ni 20/80. Ndio, una nafasi ya asilimia 20 tu ya kusamehewa.

Kinyume chake, kama ungeenda mwenyewe ukamwambia mkeo juu ya dhambi uliyofanya, dhambi ya kuisaliti ndoa yenu. Kisha ukamwomba radhi akusamehe kwa kutoka nje ya reli, nafasi ya mkeo kukusamehe ni 80/20. Ndio, una nafasi ya asilimia 80 ya mkeo kukusamehe.

Macho ya wanajamii yanaliangalia na kulifuatilia kwa karibu sakata hili la Jerry Muro na Jeshi la Polisi. Jerry Muro hapa anawakilisha pia tasnia ya habari na mawasiliano. Kwa wanajamii inahusu imani yao kwa Jeshi la Polisi na Wanahabari. Ikumbukwe, huu ni mwaka wa uchaguzi. Polisi na Wanahabari wana mchango mkubwa katika kufanikisha mchakato huo. Vyombo hivyo viwili havipaswi kugubikwa na wingu kubwa la mashaka. Ya wanajamii juu ya utendaji wao na hususan suala zima la maadili.

Kama sakata zima ni kazi ya ' kisanii' inayofanywa na baadhi ndani ya jeshi la polisi, basi, busara hapa si kusubiri mahakama. Ni kwa polisi kuikabili jamii na kusema ukweli mzima, kukiri mapungufu, maana sote ni binadamu. Polisi iwaombe radhi Jerry Muro na wanajamii. Nafasi ya kusamehewa na kubakisha imani ya jamii kwa jeshi hilo ni 80/20. Ni kubwa. Na kwa Jerry Muro, hivyo hivyo. Ukweli wa jambo zima anaujua, na jamii itakuja kufahamu. Kama amehusika kwa namna moja au nyingine na tuhuma hizi za utapeli, basi, aikabili jamii. Akiri mapungufu, naye ni binadamu. Aliombe radhi jeshi la polisi na wanajamii. Na saa ya kufanya hivyo ni hii.

Maggid

Iringa, Februari, 3, 2010.
 
Hii ni kiini macho. Inavyoonekana Kova amekula dili na hawa watu watimize mission fulani against Jerry kwa kumtumia huyo ex-mhasibu wa bagamoyo. Baada ya mtego kushindikana kutokana sasa watakua wamekubaliana awatose kiaina na tuhuma za utapeli lakini ajenge mazingira ya kushindwa kesi.

Nasema hivyo kwa sababu naamini Kova sio mjinga kiasi cha kuwaleta watuhumiwa anaotarajia kuwafikisha mahakamani kwenye press conference na kuwahukumu kuwa ni matapeli wakubwa ilihali akijua kabisa kwa kufanya hivyo ameipa mahaka kibali cha kuwaachia kwa kutotendewa haki na polisi. Pili anajua kabisa kuwa watuhumiwa wanaweza kumshitaki yeye na jeshi la polisi kwa kuwadhalilisha. Mbona hakumleta Jerry kwenye hiyo press confrerence????

Angalia jinsi anavyojiuma uma na anavyotumia lugha kali dhidi yao as if tayari wamedhihirika kuwa ni wahalifu. Kama walijua ni matapeli mbona hawakuwakamata siku zote na leo walipowahitaji tu wakawachukua hapo kinondoni??

Inonekana hawa ni washirika wa polisi kwenye michezo yao michafu na hapa wanafanya usanii tu. Kalakabaho.
National inteligence, please do your part!!!!!!!!
 
Kibao chamgeukia Kova http://majira.co.tz/index.php?view=...-kova&format=pdf&option=com_content&Itemid=57 http://majira.co.tz/index.php?view=...nt&print=1&page=&option=com_content&Itemid=57 http://majira.co.tz/index.php?optio...vdmEmb3B0aW9uPWNvbV9jb250ZW50Jkl0ZW1pZD01Nw== Wednesday, 03 February 2010 05:51 Na Edmund Mihale

SAKATA la kukamatwa kwa tuhuma za kutaka kupokea rushwa kwa mwandishi habari wa TBC, Bw. Jerry Muro, limeanza kumgeuka Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova kuwa amevunja Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.

Kwa mujibu wa wanasheria mbalimbali, Bw. Kova amevunja sheria hiyo kwa kumtaja mtoa taarifa, Bw. Michael Wage, ambaye alidai kuombwa rushwa ya sh. milioni 10 na Bw. Muro.

Bw. Wage alikuwa Mhasibu wa Hamashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kabla ya kutimuliwa kazi na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda.

Sheria hiyo kifungu cha 51 (1) (a) inazuia kutajwa kwa jina, makazi na anuani ya mtu aliyetoa taarifa kuhusu vitendo vya rushwa au aliyesaidia mamlaka inayohusika kufanikisha kukamatwa kwa mhusika.

Sehemu (b) ya kifungu hicho inazuia shahidi kujibu swali ambalo jibu lake linaweza kusababisha kujulikana kwa mtu aliyetoa taarifa juu ya vitendo vya rushwa.

Chanzo chetu kutoka ndani ya TAKUKURU kililimbia Majira kuwa kitendo kilichofanywa na Bw. Kova ni uvunjifu wa sheria hiyo.

Kamanda Kova hakupatikana jana jioni kuzungumzia suala hilo kwani simu yake ilikuwa ikiita bila kupokewa.

Wakati huo huo, mapema jana, Bw. Kova aliwataja watu wawili aliodai ni matapeli sugu kuwa ndio walishirikiana na Bw. Muro kumtishia Bw. Wage kwa lengo la kujipatia rushwa.

Watu hao ni Bw. Edmund Kapama Mkazi wa Mwananyamala na Bw. Deogratius Mgassa, Mkazi Mbezi Beach ambao walikamatwa jana katika Mgahawa wa PR Camp, Kinondoni Dar es Salaam.

Source:Majira
 
Maggid;

Hard Facts:
1. Jerry ameonekana kwenye camera ya hotel akiwa na huyo mhasibu na wale matapeli wa Dar wanaojulikana.

2. Jerry alikutwa na pingu aliyothibitisha kuwa ni yake. pingu na mwandishi wa habari wapi na wapi?

3. Kwenye Camera ya Jerry kulikuwa na picha ya ghorofa za huyu mhasibu wa bagamoyo9Nyumba anazojenga Morogoro)

4. Jerry hakutaka kushuka kwenye gari bali alitaka kukutana na jamaa kwenye gari badala ya sehemu public.

5. Jerry anadai Kamanda Kova (kamishna wa polisi) ni mtu mdogo sana hapa Tanzania.

Madai:

1. Ni tabia ya Jerry kula rushwa
2. Jerry siku hiyo aliwazunguka wenzie.
3. Wale jamaa waliokamatwa na kuonekana na jerry ni matapeli makubwa.


Machache tu hayo

FP
 
Maggid,
Kwa Tanzania yetu hii hakuna mwenye ujasiri wa kukiri kosa, mapungufu, kasoro zake na wakati mwingine hata kwa mtutu. Polisi wetu wamekosea sana tangu walipoanza kulifuatilia hili hadi ukamataji wa Muro na wenzake. Mzee Kova yeye anadhani TV ni kila kitu katika kuonekana anachapa kazi.
Muro ameyatumia makosa ya polisi wetu vizuri tu. Alikosea kidogo alipoanza kutafuta huruma ya Watanzania kupitia kwenye vyombo vya habari. Amesahau kuwa wapo wanaomjua vizuri na waliokwishamhonga kwa masuala mengine.
Hili litamalizika kisiasa tu.
 
aina ya pistol/bastola ya jerry

i1606_CZ97.JPG.jpeg
 
Ukiangalia press conference hiyo ya Kova unatoka na maswali mengi kuliko majibu.
1.Kwa nini Kova kawaleta hao anaowaita matapeli sugu ktk conference yake huku akijua wana kesi mahakamani na kawaita matapeli sugu hadharani?
2. Kama anauhakika wanashirikiana na Muro, mbona Muro hajamsimamisha hapo pamoja na hao.
3. Hizo pesa M.10 alizotegeshewa Muro ziko wapi?
4. Kwa nini? kwa nini? kwa nini? ni nyingi mno.
Polisi sasa inakwenda harijojo, nakumbuka kuna mbunge mmoja aliwahi kusema jeshi hili livunjwe ili kuliunda upya enzi za Mahita ila aliambulia majibu ya kebehi kutoka kwa mbabe yule. Wazo lile lingefanyiwa kazi sasa maana Polisi wa sasa wanaanza kuwa tishio kuliko majambazi,maharamia na matapeli.
 
Cn this be a conspiracy by ..jerry;s previous employer? hmmmmmmm................
Lately many are leaving ITV..Jerry was a anchor of ITV..Let us give this a thought..
 
Maggid;

Hard Facts:
1. Jerry ameonekana kwenye camera ya hotel akiwa na huyo mhasibu na wale matapeli wa Dar wanaojulikana.

2. Jerry alikutwa na pingu aliyothibitisha kuwa ni yake. pingu na mwandishi wa habari wapi na wapi?

3. Kwenye Camera ya Jerry kulikuwa na picha ya ghorofa za huyu mhasibu wa bagamoyo9Nyumba anazojenga Morogoro)

4. Jerry hakutaka kushuka kwenye gari bali alitaka kukutana na jamaa kwenye gari badala ya sehemu public.

5. Jerry anadai Kamanda Kova (kamishna wa polisi) ni mtu mdogo sana hapa Tanzania.

Madai:

1. Ni tabia ya Jerry kula rushwa
2. Jerry siku hiyo aliwazunguka wenzie.
3. Wale jamaa waliokamatwa na kuonekana na jerry ni matapeli makubwa.


Machache tu hayo

FP

Hebu tujaribu kupitia habari hii toka gazeti la Mwananchi tuone wataalamu wa sheria wanasemaje kuhusu Jerry kukutwa na Pingu

SAKATA LA JERRY MURO: Wanasheria wasema pingu ni kama ndizi

SAKATA la mwandishi wa habari za uchunguzi, Jerry Muro, limeingia katika hatua mpya baada ya wanasheria kusema kitendo chake cha kukutwa na pingu si kosa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Muro, mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji (TBC) na ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kufichua aina tofauti za rushwa, Jumapili iliyopita alikutwa na pingu katika gari alilokuwa akilitumia mara baada ya kukamatwa kwa kudaiwa kutaka fedha kwa njia ya vitisho kwa aliyekuwa mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Wage.

Wage alisimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali za serikali pamoja na viongozi wengine wa halmashauri hiyo.

Kamanda wa polisi Kanda ya Dar es salaam, Suleiman Kova alisema kuwa baada ya kulifanyia upekuzi gari la Muro walikuta pingu na bastola na hivyo wakamuagiza mwandishi huyo awapelekee risiti zinazoonyesha kuwa alinunua pingu hizo kihalali.

Kamanda huyo akadokeza kuwa pamoja na kumwambia awapelekee risiti, wanajua kuwa hangefanikiwa kuzipata kwa kuwa pingu haziuzwi ovyo na kwa kuwa mwenye mamlaka ya kumuweka nguvuni mtu ni polisi pekee.

Hadi jana, Muro alikuwa hajawasilisha risiti hiyo na Kova alisema jeshi lake linaendelea kumpa muda wa kutafuta kidhibiti hicho.

Lakini wanasheria waliozungumza na Mwananchi wanapingana na maelezo hayo ya Kamanda Kova.

Wakizungumza jana jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti, mawakili wa jijini Dar es salaam, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando walisema kwa mujibu wa sheria za nchini, hakuna kosa kwa mtu kukutwa na pingu.

"Kwa mujibu wa sheria za nchi, kukutwa na pingu si kosa ila utakuwa na kosa tena la jinai endapo ukikutwa na government stores (mavazi ya kijeshi na polisi ikiwemo kofia na mabuti) pamoja na kumiliki isivyo halali bunduki, bastola na hata risasi," alisema Profesa Safari.

Profesa Safari alifafanua kwamba katika mwenendo wa makosa ya jinai, hakuna kipengele kinachoonyesha kuwa ni kosa mtu kukutwa na pingu.

Naye Marando alisema hakuna kosa kukutwa na pingu kwa kuwa kifaa hicho ni kama bidhaa nyingine.

Alisema ndio maana duka la silaha huu vitu hivyo kwa hiyo kisheria si kosa kukutwa na pingu.

"Hakuna tatizo kukutwa na pingu kwa kuwa ni bidhaa na ndo maana inauzwa kwenye duka la silaha," alisema Marando.

Kova alidai polisi walikuta bastola aina ya CZ97B yenye namba A6466 iliyokuwa na risasi 10 iliyotengenezwa Jamhuri ya Check na pingu. Polisi pia walikuta miwani ambayo inadaiwa kuwa ya Wage pamoja na karatasi nyepesi (tissue) ambazo mhasibu huyo anadai alizisahau kwenye gari hilo.

Katika kanda ya video ilivyo mtandaoni, Muro anaonekana akieleza kuwa amekuwa na bastola na pingu hizo kwa takriban miaka minne na kwamba Kova anajua hilo, lakini anashangaa kwamba hataki kueleza ukweli wote.

Hata hivyo, Kova alikana kuwa na uhusiano na Jerry na tuhuma za kumpa pingu hizo huku akikanusha kuwepo na tukio la kutishiwa kwa mwandishi huyo wa zamani wa ITV na mtangazaji wa kipindi kinachoanza kupata umaarufu cha Usiku wa Habari kinachorushwa na TBC1.

Katika hatua nyingine watu mawili wamekamatwa juzi jioni katika mgahawa wa PR Camp Kinondoni jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kushirikiana na Muro kufanya vitisho na kudai kiasi cha Sh10 milioni kwa Michael Karoli.

Polisi imedai iliwakamata watu hao juzi jioni wakiwa pamoja katika mgahawa huo na kwamba hawatawekewa dhamana kutokana na kutoaminika.

Walidai kuwa watu hao wataendelea kushikiliwa na polisi tofauti na Muro ambaye bado yupo nje kwa dhamana.

Kamanda Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa watu hao walikamatwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema jana jioni.

Alisema kabla ya kukamatwa kwao, wapelelezi waliziona picha za kumbukumbu za watuhumiwa hao kwenye kamera maalum za CCTV ambazo hurekodi na kutunza kumbukumbu za matukio.

Kamanda Kova alisema watu hao wanaonekana kwenye mkanda wa kamera hizo wakiwa watatu na wanafanya mazungumzo kwenye meza pamoja na mlalamikaji.

Kova pia alisema kumbukumbu nyingine za CCTV zinaendelea kufuatiliwa katika mtindo huo kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa ili kuondoa utata wa tukio hilo linalomkabili Jerry Muro.

"Tunaendelea kufuatilia tukio zima lilivyofanyika... kwa kutumia teknolojia za kisasa tutaweza kutambua ukweli wote na kuondoa ubishi au utata uliopo kwa lengo la kuweka mambo wazi,’’ alisema Kova.

Aliongeza kuwa baada ya kuonekana kwa watu hao kwenye mkanda wa CCTV, mlalamikaji Wage aliwatambua kuwa hao ndiyo waliotaka rushwa na kumtishia kwa kumtaka awape Sh10milioni.

"Hawa jamaa walitambuliwa katika gwaride maalum la kutambua wahalifu. Baada ya mlalamikji kuja aliwatambua lakini pia hawa jamaa katika kumbukumbu zetu tumegundua kuwa ni matapeli ambao tuliwahi kuwakamata wakihusika katika matukio mbalimbali na walifikishwa mahakamani ambako hadi sasa wana kesi,"alisema Kova.

Kova alidai kuwa upelelezi wa tukio hilo unaendelea kwa kasi na kwa umakini kwa kuzingatia sheria na taratibu.

 
350__1_pvc_animal_print_set__38179.jpg
aayq1.jpg
51ANgPKx6AL.jpg


unajua inawezekana Jerry akawa na pingu as a SEX TOY...you know he's probably into S & M kama hizo hapo juu

lakini kama ina references za polisi then thats a different case...hivyo kama ana akali he can get away with this argument kuwa he is into WILD sex GAMES

then tutamove on kwente issue ya bastola
 
Cn this be a conspiracy by ..jerry;s previous employer? hmmmmmmm................
Lately many are leaving ITV..Jerry was a anchor of ITV..Let us give this a thought..
No thank you! ITV mbona haijashabikia hii na inaonyesha pande zote vizuri? Mbona pia guardian limeandika objectively? Hapa hakuna kitu kama hicho. It is possible JM aliandaliwa mtego na ukawa haujateguka vizuri lakini pia inawezekana pia ikawa ni tabia yake. Pia hizo camer lazima zionyesha kuwa ni kweli ni JM na isije ikiwa imetengenezwa kwa fix za komputa, maana kwa jinsi Kova anavyopende sifa angeweza hata kuonyesha hiyo picha. Lakini hayo yote yatajulikana kama uchunguzi wa kina utafanyika na tasnia ya habari nayo ikawa inatoa taarifa za uchunguzi zaidi kuwa inasikiliza tu kuandika Kova kasema nini.
Ile la ITV kuondokewa na wanahabari wanakuwa porched and they are looking for greener pastures same as you if you get a lucrative offer somewhere else. Wafanyakazi waliopitia Radio one and ITV na kuondoka na wengi wapo hata katika vyombo vikubwa zaidi na wengi pia wana umaarufu mkubwa kuliko wa JM na hawajawahi kufanyiwa mizengwe otherwise wangesema. Lets focus on the real issue: Kuomba rushwa ya shs10million na JM toka kwa Wage!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Polisi wetu hawaaminiki. Na hii kesi ina maruweruwe kibao, yanayosababisha wazidi kutoaminika. Hata kama kweli Jerry alikuwa anaitaka hiyo rushwa, inakuwa rahisi zaidi hapa kuwatia hao polisi hatiani kuliko Jerry. Yani pumba na mchele zimefanana, unfortunately.
 
Maggid;

Hard Facts:
1. Jerry ameonekana kwenye camera ya hotel akiwa na huyo mhasibu na wale matapeli wa Dar wanaojulikana.

2. Jerry alikutwa na pingu aliyothibitisha kuwa ni yake. pingu na mwandishi wa habari wapi na wapi?

3. Kwenye Camera ya Jerry kulikuwa na picha ya ghorofa za huyu mhasibu wa bagamoyo9Nyumba anazojenga Morogoro)

4. Jerry hakutaka kushuka kwenye gari bali alitaka kukutana na jamaa kwenye gari badala ya sehemu public.

5. Jerry anadai Kamanda Kova (kamishna wa polisi) ni mtu mdogo sana hapa Tanzania.

Madai:

1. Ni tabia ya Jerry kula rushwa
2. Jerry siku hiyo aliwazunguka wenzie.
3. Wale jamaa waliokamatwa na kuonekana na jerry ni matapeli makubwa.


Machache tu hayo

FP

Shida ni kwamba hizo unazoita 'hard facts' - zote zinafikirika. Hakuna evidence yoyote. Mwandishi wa habari kukutwa na picha sio hoja, na sio lazima aeleze undani wa picha hizo hasa kama kazi yake ni investigative journalist. Mbona polisi wanashinda vijiweni na majambazi sugu tena wanakula nao mgao - achilia mbali matapeli. Mbona hatutangaziwi watu ambao hatutakiwi kuonekana nao hadharani?

Hili swala limekaa kiubabaishaji zaidi - kuna kitu kimefichwa au kinatafutwa. Kwa nini hawakusubiri wapate red handed exhibit? Simtetei Jerry ila nasema, kwa jinsi mazingira yalivyo tunalazimika kuuliza integrity ya jeshi la polisi hasa ukizingatia reputation waliyo nayo.
 
Maggid;

Hard Facts:
1. Jerry ameonekana kwenye camera ya hotel akiwa na huyo mhasibu na wale matapeli wa Dar wanaojulikana.

2. Jerry alikutwa na pingu aliyothibitisha kuwa ni yake. pingu na mwandishi wa habari wapi na wapi?

3. Kwenye Camera ya Jerry kulikuwa na picha ya ghorofa za huyu mhasibu wa bagamoyo9Nyumba anazojenga Morogoro)

4. Jerry hakutaka kushuka kwenye gari bali alitaka kukutana na jamaa kwenye gari badala ya sehemu public.

5. Jerry anadai Kamanda Kova (kamishna wa polisi) ni mtu mdogo sana hapa Tanzania.

Madai:

1. Ni tabia ya Jerry kula rushwa
2. Jerry siku hiyo aliwazunguka wenzie.
3. Wale jamaa waliokamatwa na kuonekana na jerry ni matapeli makubwa.


Machache tu hayo

FairPlayer tuongelee zaidi sheria inasemaje kuhusu jambo hili na tuache mazoea!

Kwanza;tuhuma za Muro ilikuwa kupokea rushwa ya milion 10 lkn sasa afande Kova haiongelei tena tuhuma hizo nzito za rushwa na sasa anaongelea zaidi mambo ya kukutwa na pingu;kifaa ambacho HAKIHESABIKI kama ni sare ya majeshi ya tz kwa hiyo sio kosa kuwa na pingu!

Pili,kwa sababu ilikuwa ni suala la rushwa wanaopaswa kuweka mtego hasa ni TAKUKURU ingawaje Polisi wanaruhisiwa kufanya hivyo pia;lkn polisi ama TAKUKURU wanapaswa kisheria wasitoe majina ya waliowapasha kuhusu kuombwa rushwa ili wasiharibu ushahidi badala yake kamanda Kova kataja ni nani alitaka kuombwa rushwa na Muro

Tatu,kukutwa kwenye mitambo ya ving'amuzi akiwa na jamaa aliyeombwa rushwa au kukataa kushuka kwenye gari lake au hata kutambuliwa miwani ya mtuhumu kwenye gari la Muro hakumfanyi mtuhumiwa ndiyo ashatakiwe kwa rushwa

Mwisho shitaka la rushwa inabidi waendesha mshtaka wathibitishe mahakamani "without any reasonable doubt"kama mtuhumiwa ama aliomba au alipokea rushwa,lkn badala yake upande wa jamhuri umeshindwa sio tu kumkamatisha Muro na kidhibiti cha rushwa bali pia hamna taarifa zozote hata kama kweli hizo milion 10 zilikuwepo eneo la tukio wakati Muro anakamatwa!

Muro asibugudhiwe na nina imani kwa asilimia zote kitendo cha ujasiri cha Muro kutangaza rushwa miongoni mwa polisi-trafic ndiyo kunamtokea sasa puani!
 
Muro asibugudhiwe na nina imani kwa asilimia zote kitendo cha ujasiri cha Muro kutangaza rushwa miongoni mwa polisi-trafic ndiyo kunamtokea sasa puani!

Well nadhani kuna zaidi ya hii; wale polisi kule hawana uwezo wa kuendesha racket nzuri namna hii na isitoshe wengi wao wapo hatiani tayari; kuna real story hapa inafunikwa; lakini tutajua tu ; ndio uzuri wa dhambi; dhambi bwana hata uwe peke yako; iko siku inakuadhiri inajifunua mbele ya kadamnasi na kila mtu ndipo anpogundua kuwa mfalme yuko uchi!
 
My take on this controversy ni hii:-
1. Jeshi la Polisi(JLP) baada ya kuwa wameaibishwa mara kadhaa na Jerry Muro(JM) walipanga kumnyamazisha/kulipa kisasi kwa mbinu yeyote.
2. Kapama na Mgasa (matapeli sugu) wametumika na JLP kumtumbukiza Jerry katika mchezo wa kutafuta rushwa kwa Wage. Kwanini nafikiri hivi? Polisi inawataja Kapama na Mgasa kama matapeli sugu na waliona kesi nyingine ghafla baada ya JM kukamatwa na matangazo yote kwenye media zote nchini, jamaa wamekamatwa ''kirahisi'' kinondoni (JIULIZE). Polisi walikuwa wapi siku zote kukamata matapeli hawa sugu?
3.Kapama na Mgassa wamekataliwa dhamana kwa kuwa wana kesi nyingine. Hawa hawataachiwa kwani wanaweza kuropoka wakiwa uraiani.Kwa kuwa hawa ni watuhumiwa na JLP inawajua kama matapeli sugu huenda hapa kuna dili, tusaidieni kumdhalilisha JM tuwape ''ulinzi wa kipolisi'' kama vile kuacha kufuatilia kesi zenu za nyuma n.k
4.Ziko taarifa kuwa JM was on the verge of revealling a shocking corruption scandal. Nani angetajwa? Wage alikuwa nahusika? pamoja na kina nani wengine? Hawa hawawezi ku conspire na JLP (wanayo motive, JM amewaumbua), Kapama na Mgassa (wametishwa na JLP, wanataka kujinasua) Wage (pengine ni mtajwa katika kashfa aliyokuwa anifuatilia JM pamoja na kina nani) duh...ngumu...hii kesi ni ngumu.

Upande wa pili wa shillingi:
1. JM alikuwa mzoefu kweneye huu mchezo(kutisha na kujipatia rushwa)
2. Akaunda urafiki na Mgassa na kapama(matapeli sugu) pengine na baadhi ya polisi ambao wamemgeuka na kumchoma.

Maswali machache.
1. Hivi JLP wamefanya upekuzi wowote nyumbani kwa JM?Au ndio kusema wameridhika ushahidi wote wanaoutaka ulikuwa kwenye gari and that is it? Sijasikia lolote kuhusu JLP kwenda nyumbani kwa JM.
2.Kwanini JLP hawakusubiri JM akutane na WAGE ,pengine hela zitolewe ndipo wafanye arrest?
3. Kama tayari walikuwa na ushahidi wa CCTV na wanaonekana walikuwa na UHAKIKA kuwa vidhibiti vyote vilivyotajwa na mlalamikaji viko kwenye gari kwanini walimuita City Garden aje kufanya nini??????? si wangenkamata mahali popote tu barabarani, AU wangeenda tu ofisini kwake TBC kwani Wage alikuwa najua mtuhumiwa wake ni JM.
4. Hivi kwa mtu kama Wage ni kweli alikuwa hamjui JM kiasi aamini kuwa JM ni mtu wa usalama wa Taifa/mwanajeshi/PCCB kwanini asingemtaarifu tu Tido Mhando kuwa JM aamekuja kwangu na kuiita Polisi??????

Maswali ni mengi...Polisi watahitaji nguvu lubwa sana kushinda hii kesi, wasidhani RISITI YA PINGU PEKEE NDIO ITAWAPA USHINDI, baadhi ya maswali haya yatauliwzwa na DPP, mawakili, Wazee wa baraza n.k!!!!

nadhani kesi ikianzia hapam ,bivu na mbichi zitajulikana. hongera scofield
 
Polisi wa nchi hii wakikutaka hawakukosi. Huenda woote tukaona kuwa Jerry Muro ametabambikiwa (kwa kujumuishwa) kwenye hii kesi ya kudai rushwa, hali iliyopelekea kupekuliwa na polisi na kukamatwa kwa silaha (bastola anayodai kumiliki kihalali), na pingu (anazohojiwa za nini kwake, ingawa sheria haimkatazi mtu kumiliki). Jamii nzima imejua kuwa JM anamiliki silaha, na pia ana pingu, ambazo pamoja na kuwa hazihitaji kibali kumiliki, bado hajaweza kusema alikuwa nazo garini kwa ajili gani (maana huenda zingekuwa nyumbani angeweza kusema hua anafunga watoto wake wanapoleta vurugu).

Polisi wa nchi wakikutaka hawakukosi. Polisi wa kanda maalumu ya Dar sasa wanayo bastola ya Jerry Muro na pingu. wanaweza kusema uchunguzi wao na ushauri wa kisheria wa mawakili wao umekosa nguvu ya kumpeleka JM mahakamani, lakini jamii itakuwa at least imepata hisia kuwa huenda alikuwemo, na itakuwa imejua kuwa anamiliki silaha (ambayo polisi wameishikilia kwa muda) na pingu. Baada ya hayo kutokea, polisi watamuachia Jerry Muro kwa kumwambia hawana ushahidi wakutosha, lakini watakuwa wamepata wanachokitaka. wanaweza kuweka vitu fulani, mfano maganda ya risasi toka silaha ya jerry muro, halafu wanamrudishia silaha yake. Halafu akiendelea na fumua fumua yake kwa askari wala rushwa, utasikia siku moja kuwa kuna majambazi yameua na kupora, na katika uchunguzi wa kipolisi, moja ya silaha zilizotumika inahisiwa ni ile ya JM, kwakuangalia maganda ya risasi. Hapa atakuwa amepatikana tu

ushauri wangu....kuwa makini sana ukishakuwa unalengwa na polisi, Polisi ipo chini ya serilkali, na hiyo hiyo serikali ambayo mpaka leo inalia na ishu ya zombe, kwani inaamini alifanya uhalifu lakini mahakama haijaona

Don't trust them
 
Back
Top Bottom