TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

My take on this controversy ni hii:-
1. Jeshi la Polisi(JLP) baada ya kuwa wameaibishwa mara kadhaa na Jerry Muro(JM) walipanga kumnyamazisha/kulipa kisasi kwa mbinu yeyote.
2. Kapama na Mgasa (matapeli sugu) wametumika na JLP kumtumbukiza Jerry katika mchezo wa kutafuta rushwa kwa Wage. Kwanini nafikiri hivi? Polisi inawataja Kapama na Mgasa kama matapeli sugu na waliona kesi nyingine ghafla baada ya JM kukamatwa na matangazo yote kwenye media zote nchini, jamaa wamekamatwa ''kirahisi'' kinondoni (JIULIZE). Polisi walikuwa wapi siku zote kukamata matapeli hawa sugu?
3.Kapama na Mgassa wamekataliwa dhamana kwa kuwa wana kesi nyingine. Hawa hawataachiwa kwani wanaweza kuropoka wakiwa uraiani.Kwa kuwa hawa ni watuhumiwa na JLP inawajua kama matapeli sugu huenda hapa kuna dili, tusaidieni kumdhalilisha JM tuwape ''ulinzi wa kipolisi'' kama vile kuacha kufuatilia kesi zenu za nyuma n.k
4.Ziko taarifa kuwa JM was on the verge of revealling a shocking corruption scandal. Nani angetajwa? Wage alikuwa nahusika? pamoja na kina nani wengine? Hawa hawawezi ku conspire na JLP (wanayo motive, JM amewaumbua), Kapama na Mgassa (wametishwa na JLP, wanataka kujinasua) Wage (pengine ni mtajwa katika kashfa aliyokuwa anifuatilia JM pamoja na kina nani) duh...ngumu...hii kesi ni ngumu.

Upande wa pili wa shillingi:
1. JM alikuwa mzoefu kweneye huu mchezo(kutisha na kujipatia rushwa)
2. Akaunda urafiki na Mgassa na kapama(matapeli sugu) pengine na baadhi ya polisi ambao wamemgeuka na kumchoma.

Maswali machache.
1. Hivi JLP wamefanya upekuzi wowote nyumbani kwa JM?Au ndio kusema wameridhika ushahidi wote wanaoutaka ulikuwa kwenye gari and that is it? Sijasikia lolote kuhusu JLP kwenda nyumbani kwa JM.
2.Kwanini JLP hawakusubiri JM akutane na WAGE ,pengine hela zitolewe ndipo wafanye arrest?
3. Kama tayari walikuwa na ushahidi wa CCTV na wanaonekana walikuwa na UHAKIKA kuwa vidhibiti vyote vilivyotajwa na mlalamikaji viko kwenye gari kwanini walimuita City Garden aje kufanya nini??????? si wangenkamata mahali popote tu barabarani, AU wangeenda tu ofisini kwake TBC kwani Wage alikuwa najua mtuhumiwa wake ni JM.
4. Hivi kwa mtu kama Wage ni kweli alikuwa hamjui JM kiasi aamini kuwa JM ni mtu wa usalama wa Taifa/mwanajeshi/PCCB kwanini asingemtaarifu tu Tido Mhando kuwa JM aamekuja kwangu na kuiita Polisi??????

Maswali ni mengi...Polisi watahitaji nguvu lubwa sana kushinda hii kesi, wasidhani RISITI YA PINGU PEKEE NDIO ITAWAPA USHINDI, baadhi ya maswali haya yatauliwzwa na DPP, mawakili, Wazee wa baraza n.k!!!!
 
hivi huyo muhasibu baada kufuzwa kazi inamaana anaenda ku-enjoy hizo hela alizopata kwa udanganyifu au uchunguzi unafanywa hili achukuliwe hatua pamoja na kufilisiwa?
 
Mimi ninafikiri pa kuanzia ni ku-trace ile namba alopigiwa Jerry Muro kwamba kuna story ya ku-cover pale City Garden. Hili mbona liko wazi ati! We should not sweep it under the carpet! Atafutwe alopiga simu then picha linaendelea...........
 
Hii inawezekana kabisa kutrace nadhani calls zote. kisheria
 
Sawa tutapata namba ya simu, lakini Police kwa nini wanaifanya hii ni issure kuuuuubwa!! jamani kwani Jerry ni nani? Mbona Kova ukitaka kumuweka kwenye umaarufu ni maarufu kuliko Jerry!!! Sasa kwa kumsumbua huyu Jerry kiasi hiki police wanashusha umaarufu wao.

Kwanza mtu mmoja wao polisi walienda kumi sita kwenye Defender na wanne askali kanzu hii ni dhihaka ya mwaka.

Kuhusu simu ni rahisi kuipata kwanza utachukua namba ya Jerry na kwenda kwenye kampuni ya simu anayoitumia kama vile Tigo, voda au Zain kisha utafeed Data kwenye mkanda ukiomba simu namba furani imepigiwa simu gani siku tano kabla na siku tano baada na je mazungumzo ni yapi kila kitu kitatoka.

Na kama namba ile iliyomuita kama itatokea mala nyingi huko nyuma basi Jerry mtu huyo alikuwa anamfahamu lau kama haijatokea basi mtu huyo ni tapeli na utakuwa mchezo wa kuigiza. ila Kova asiombe waende mahakamani police watashindwa vibaya.
 
Sawa tutapata namba ya simu, lakini Police kwa nini wanaifanya hii ni issure kuuuuubwa!! jamani kwani Jerry ni nani? Mbona Kova ukitaka kumuweka kwenye umaarufu ni maarufu kuliko Jerry!!! Sasa kwa kumsumbua huyu Jerry kiasi hiki police wanashusha umaarufu wao.

Kwanza mtu mmoja wao polisi walienda kumi sita kwenye Defender na wanne askali kanzu hii ni dhihaka ya mwaka.

Kuhusu simu ni rahisi kuipata kwanza utachukua namba ya Jerry na kwenda kwenye kampuni ya simu anayoitumia kama vile Tigo, voda au Zain kisha utafeed Data kwenye mkanda ukiomba simu namba furani imepigiwa simu gani siku tano kabla na siku tano baada na je mazungumzo ni yapi kila kitu kitatoka.

Na kama namba ile iliyomuita kama itatokea mala nyingi huko nyuma basi Jerry mtu huyo alikuwa anamfahamu lau kama haijatokea basi mtu huyo ni tapeli na utakuwa mchezo wa kuigiza. ila Kova asiombe waende mahakamani police watashindwa vibaya.

Mazungumzo ngumu mzee labda meseji!
 
nadhani inabidi kweli kucheki kama ile namba ilikuwa inampigia jerry mara nyingi kabla ya hapo? kila details zipo wazi .
 
nadhani inabidi kweli kucheki kama ile namba ilikuwa inampigia jerry mara nyingi kabla ya hapo? kila details zipo wazi .

Hii namba ndipo pa kuanzia. Na siku hizi namba zote si zimeandikishwa kwa hiyo mwenye namba hiyo atakuwa anajulikana (kama kaiandikisha namba hiyo).
 
hivi nyie vipi? Kuna cctv imemnasa Jerry wenu akiwa na jamaa hotelini na Jerry wenu alivyo mjinga kamkana jamaa . Tulieni Jerry ni mlla rushwa.
 
Mimi ninafikiri pa kuanzia ni ku-trace ile namba alopigiwa Jerry Muro kwamba kuna story ya ku-cover pale City Garden. Hili mbona liko wazi ati! We should not sweep it under the carpet! Atafutwe alopiga simu then picha linaendelea...........
hii sio issue kabisa bandugu;
mtu afanye uharamia halafu awe traceable kifala hivyo?
mjanja ananunua handset ya tsh 35,000 na anakuwa na unregistered simcard, akishamaliza kuitumia anatupa vyote?
hapo vipi?
 
PRESS RELEASE
02.02.2010
MATAPELI SUGU WAWILI WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM NI WALE
WALIOSHIRIKIANA NA JERRY MURO.

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limewashikilia na kuwahoji watuhumiwa wawili kwa kosa la kutumia vitisho katika kudai fedha Tsh.10,000,000/= kutoka kwa mlalamikaji Michael Wage Karoli. Watuhumiwa hao ni: ...

1.Edmund S/O Kapama (52) maarufu kama Dr. au Jiji Kazi, mkazi wa Mwananyamala
2.Deogratius S/O Mgasa umri wa miaka 35 hana kazi anaishi Mbezi Beach.

Katika kuendelea na upelelezi wa kesi ambayo Michael Karoli anadai alipata vitisho na kutakiwa atoe Tshs. 10,000,000/= na watuhumiwa watatu. Polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao eneo la Kinondoni baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia mwema. Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa wote tarehe 1/2/2010 katika mgahawa maarufu wa PR. Camp Kinondoni.

Kabla ya kukamatwa watuhumiwa hawa polisi wapelelezi walifanikiwa kupata kumbukumbu za watuhumiwa hao walioshirikiana na mtuhumiwa Jerry Muro. Picha hizo zimeonekana katika kifaa cha ELEKTRONIKI (CCTV) chenye uwezo wa kurekodi na kutunza kumbukumbu. Katika tukio hilo watuhumiwa watatu walionekana wakiwa katika meza ya mazungumzo pamoja na mlalamikaji. Aidha kumbukumbu zingine zinaendelea kufuatiliwa kwa mtindo huu kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa ili kuondoa ubishi na utata kwa lengo la kupata ufanisi na uwazi. Watu hao wawili walifanyiwa gwaride la utambulisho na tayari mlalamikaji Michael Wage Karoli amewatambua. Aidha Edmund Kapama na Deo Mgassa ni matapeli sugu wenye kesi katika mahakama mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakingojea hatma yao.

Upelelezi wa shauri hili unaendelea kwa kasi na kwa umakini kwa kuzingatia sheria na taratibu.

S.H.Kova-SACP
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUM YA POLISI
DAR ES SALAAM.
 
Hapa naona Polisi hawana ushahidi hata kwa hao matapeli zaidi naona ni Blackmailing, kwanza kwa kumbukumbu yangu wanasema walikuwa wakimtafuta kwa Siku tatu, hiyo inaonyesha ni kitu cha kupanga, pilli wameshindwa kuwashika wote kwa tukio hilo la kupokea Rushwa hivyo kuna alama ya kujiuliza kuhusu kuwepo kwa njama hizo, Sasa ukija Suala la Mazungumzo au CCTV kwa mfano miim na X kuhusu tukio lolote Baya, haimaanishi mimi kushiriki, labda na mimi ni gather information ili niwapatie wa husika, na zaidi inaonyesha Polisi kwa sababu walikuwa nae Mtu wao Huyo Wage ndio wakamtumia kama Chambo ili kuwa leta watu hao pamoja kwa minajili ya kuwa rekodi sauti na hiyo CCTV na kuongezea huo ushaidi wao uwe strong walimfundisha Wage chakuonge ili ionekane Muro na Wenzake wametaka Rushwa.
Jambo jingine sasa kama Rushwa walikuwa wapoke Nuro na hao wengine wawili mbona hawakuwepo siku alioshikwa Muro.

Kova mbona unadhalilisha fani yako, au ndio tuseme ndivyo Polisi walivyo? Au CCP hawafundishi vizuri? nako mitihani inavujaa?
Jee leo hii niseme nataka nimshikishe Mtu X kwa Rushwa hivyo nimchukue nimpeleke Bar wakati huo niwe nimetoa taarifa Polisi kwamba X anataka Rushwa wakati ukweli ni mimi nataka nimkamatishe huyo Jamaa na Rushwa, si nitatengeneza hayo mazingira kama kuacha Koti kwenye gari lake Pili kumpeleka sehemu na kupigwa picha nae na kuzumgmzia aise Vipi nikupe ule Mzigo wako? upi ah hii ni zawadi tu 10m si unajua tena maisha bongo ni kusaidiana, na Jamaa zake Kova wana rekodi tukio mwisho wa siku fulani bin fulani umeshikwa kwa kupokea/kuomba rushwa na ushaidi wa ki-elctroniki tunao mwenyewe Kova anasema wana kitengo cha Cyber crime Geshi letu kweli lime kwenda Mbele
 
Back
Top Bottom