nguvumali
JF-Expert Member
- Sep 3, 2009
- 4,927
- 1,342
ukitaka kujua Police hawatimizi wajibu wao ni pale nilipposafiri kwa gari la ofisi lenye namba za kibalozi toka Dar es salaam mpaka Kigoma, kweli hakuna polisi alienisimamisha wala nini, unafika mahala polisi anakupungia usimame ukipunguza mwendo akisoma namba za kijani anakuashiria uondoke, mimi nauliza wavunja sheria ni watu wenye magari binafsi tu ama ?Tanzania sio kuna miujiza au vituko ila ni kichaa, nimesafiri kutoka Mwanza kwenda shinyanga kwa gari njiani kuna Check Points za Jeshi Tukufu la Polisi zaidi ya Sita na zote zina polisi wenye SMG waliovaa ki Raia(Wasio na Vazi Rasmi) Wanaonekana kama Vibaka, Je utaweza kutambua Check Point ya Polisi au Majambazi.
Tena Wanakagua kuanzia Wasafiri mpaka kazi za Traffic.
mimi naamini Rushwa iliostukiwa na Muro ndio chanzo cha yote yanayompata.