TBC FM tafuteni maudhui ya vipindi vyenu, mnakera masikio yetu

Rogart Ngaillo

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
899
1,887
Hapo mwanzo nilikuwa mfuatiliaji sana wa vipindi vya radio...ila niliacha kutokana na kuwa bize na harakati za maisha,nilipenda kufuatilia kutokana na mpangilio mzuri wa vipindi na maudhui yake.

Huku kwetu hakuna radio yoyote isikilizwayo zaidi ya TBC Taifa na TBC Fm kwahiyo haina namna,ukifungulia radio tu lazima upambane nazo.

Kinachokera kwenye TBC Fm ni kwamba kwenye vipindi vyao inaonesha hawaandai MAUDHUI yoyote ambayo wasikilzaji wangetarajia kuyapata,tofauti yake ni kusheheni kwa MATANGAZO YA "CHEZA PESA" (kamari) kila baada ya dakika tano....yaani ukisikiliza radio hii utadhani iko mahsusi kutangaza kamari!

Hata watangazaji nao wamebweteka...hawatafuti habari mpya, wao kila dakika ni "INGIZA NAMBA YA KAMPUNI 551551"..Hopeless!

Hiyo radio hata nikikabidhiwa mimi naweza kumudu kuendesha vipindi vyote maana mtangazaji hana haja ya kuumiza kichwa kuandaa maudhui ya kipindi husika zaidi ya kuongelea NAMBA YA KAMPUNI na KUMBUKUMBU NAMBA...

MNAKERA MASIKIO!!
 
Back
Top Bottom