TBC aibu tupu kwa taifa

sasa wamegoma kutuletea bunge live??manake sasa naona wale wachina wao wanaoongea kiswahili!
 
TBC ilipoteza ueledi Alipoondoka tu Tido kwa siasa za chuki za CCM.

Kama waliweza kuendelea kupiga ndombolo siku nzima bila kuwajibishwa wakati tunaomboleza Msiba wa spice islander, usitegemee ufanisi wowote!
 
Kodi yetu inalipia shughuli zote za kipuuzi zinaofanywa na baadhi ya taasisi za serikali hii ziwe za utangazaji mbaya,ulinzi na usalama mbaya,kudidimiza taifa n.k.Chukua sekunde 15,tafakari kuhusu hili kisha jiulize:''Kwa nini tunaendeleza madubwana yasiyotuletea faida?''
 
Tanzania watu wanafanya kila njia kuuondoa utamaduni wa kanzu na kofia na khanga kuwa ndio vazi la asili na linalotumiwa na watu wengi kwa ufinyu tu wa mawazo kuwa ni la Kiislaam. Ndio maana unaona kuhangaika kote huku.
Kuna siku imepita bila ya kutaja dini yako? Wewe nadhani hata mada kama inazungumzia mpira lazima utataja dini
 
Yana hayo mambo ya vazi la taifa yananiudhi sana,wakikupigia hesabu ya hizo gharama unaweza kuzimia

Nahisi harufu ya watu kulazimisha ajenda ili wapate tenda... Yale yale ya Mariedo Bout. na wizara ya afya.:A S embarassed:
 
Ni aibu kubwa sana kwa Taifa au jamii kukosa vazi la taifa ambao ndio unakuwa utambulisho wenu mnapokuwa ndani au nje ya mipaka ya nchi yenu.

Hebu nitazameni mimi hapo kwenye avatar yangu nikiwa na vazi letu la taifa. Je kwa vazi hilo si unaweza kujua natoka nchi gani.

Fungukeni na mtafute utambulisho wenu kitaifa na kimataifa.

Utamaduni wetu watanzania unaeleweka kila kabila lina utamaduni wake hii ikijumuisha mavazi ya asili, vitatumika vigezo kuhahakisha kila kila kabila linawakilisha mawazo yake? Hii ni kupoteza muda, mavazi ya taifa tayari tunayo la zaidi vazi la taifa linaongeza tija gani kwa taifa? Hicho ulichovaa hakimaanishi umetoka nchi gani, inawezekana ni mtumwa wa akili kavishwa vazi na bwana wake! Hivi umetoka nchi gani naona unajichanganya sana.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
hawa tbc mbona hamna ki2 ss ivi kilchobaki ni kula mishahara na posho ze2 bila kufanya kazi ambayo wananchi wote tunataka wafanye na sio CCM. kama wanavyofanya sasa kuwabeba CCM
 
Unajua unapokea cheo ambacho mwenzio kanyang'anywa kama un akili lazima upeleleze kwa nini mwenzio kaondolewa,mkurugenzi alikuwa TIDO tu wengine hawa waganga njaa.
 
Kitengo cha propaganda na uenezi cha ccm, sio tv ya taifa hiyo

KWA MAWAZO YANGU KWA KUWA CHAMA CHA MAGAMBA KINAFIKISHA 35YRS THIS YEAR, NI MUDA MUAFAKA KWA TBC1 NAO KUBADILI JINA NA KUITWA CBC i.e CCM BROADCASTING COOPERATION,
 
i see. .
Vazi la taifa?
Sijui 'ishu' ya nani hii!

Inaogopesha mkuu. shame on us all. just imagine wenzetu wa Kenya na Uganda wanavyo pambana na maendeleo ya Taifa sisi tunafocus na madudu.
Hilo vazi la Taifa apewe taifa avae, sisi halituhusu
 
hivi kuna watu bado wanamawazo ya kua tbc ni ya taifa.labda tu kwa mwenye mawazo hayo anifafanulie.ni ya taifa lipi hapa duniani!!!
nasema hivyo kw sbb,angalia hiyo tbc kipindi cha uchaguzi.kisha utapata jibu ni tv ya taifa gani..
 
ni kweli kabisa tangu tido aondolewe TBC imeshuka sana tarifa za habari ni aibu tupu, watangazaji wanapata aibu pale mchanganya picha za matukio anaposhindwa kuunganisha picha za matukio yanayofuata.

Kiukweli Tiod na Suzan Mungi waliipaisha sana TBC. tokea tido ameondolewa TBC imezikwa
 
La kuvunda halina ubani, ndiyo tbc japo jina lake zuri lakini vitendo sifuri.
 
Bado wanaendeleza siasa zao za kifisadi na kuficha mambo muhimu kwa wananchi. Ukiona hivyo ujue kuna move inafanyika pale Bungeni ya ambayo hawataki watu waione live kwa sababu ni aibu kwa serikali. Lakini wamefanya hivyo purpose kabisa. Mtasikia baadae moto uliowaka huko.

Nimepata tetesi kuwa kuna karatasi imepitishwa mle Bungeni na imesainiwa na wabunge zaidi ya 2/3 kuwa hawana imani na PM. Sasa hivyo move ni kali kwelikweli haiwezi ikawekwa LIVE. Tusubiri.

Mdau hebu funguka vizuri hiyo paragrafu ya mwisho! Naona umetupia uzi halafu umepotea au ni hisia zako tu
 
Siku ambayo watanzania wenyewe, sisi ambao kila kukicha tunalalamika thru threads hizi na zile tukiwaonyesha kwa vitendo hao wapuuzi kwamba tumechoka, coz in the first place sisi ndio watanzania wenyewe na tukisema kwa VITENDO vazi hatulitaki nina imani wataelewa, i just think muda wa kulalamika kwa maandishi na midomo umetosha!!!!
 
Back
Top Bottom