Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 45,931
- 102,001
Wanabodi,
Kwa watu wasiojua mambo ya utangazaji na haswa live programs mnaweza msielewe msingi wa pongezi zangu, kwa vile mimi ni Mtangazaji na nilifanyia kazi, TBC, I know what it takes kumualika mpinzani Vocal kama Zitto Kabwe kwenye a live program ya TV, hivyo hizi hongera zangu kwa TBC na kwa Dr. Ayub Rioba Chacha ni hongera bonafide genuine,
Kitendo cha wapinzani kualikwa TBC kwenye live program, chataka moyo. Kwa msiomjua ni moyo gani, naomba tembelea bandiko hili,uone kilitokea nini kwenye live ya chama hiki
Hivyo kitendo cha mpinzani Zitto Kabwe kualikwa kwenye a Live Program ya TBC, TBC unastahili hongera za that, hongera sana TBC, ila pia hongera sana kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dr. Ayub Rioba, huu ni uthibitisho kuwa sasa TBC ni TV ya Taifa kiukweli ukweli sio TV ya serikali tuu, au TV ya CCM, ni TV ya Wote!. Kwa bandiko hili, lile jina la utani la TBCCM sasa life!.
Kwa maoni yangu, hili limewezekana kufuatia mwelekeo wa the Editor in Chief wa TBC, Rais Samia kuhusu mwelekeo na mustakabali mwema wa taifa letu, umeanza kuzaa matunda, Baada ya Rais Samia, kukubali kuzungumza na wapinzani Dodoma, alipokwenda Ubelgiji akakutana na Tundu Lissu, aliporejea nchini, akamwachia Freeman Mbowe, na mara baada tuu ya kuachiwa, breki ya kwanza ya Mbowe, ikawa ni kubisha hodi Ikulu, kumshukuru Mama Samia. Juzi kati kabla ya Kikao cha Baraza Kuu Chadema, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, alikwenda Ikulu kumuona Rais Mama Samia, Rais Mama Samia akiwa ziarani Tabora, Alimwalika Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba kuhutubia mkutano wa rais!.Jana kawakaribisha Chadema Ikulu ya Chanwino.
Leo nilikuwa naangalia kipindi cha Mizani, TBC, ambacho ni kipindi cha Dr. Ayub Rioba, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe, amealikwa akiwa na a political veteran, Mzee Stephen Masatu Wasira. Kiukweli kipindi kilikuwa kizuri, wameizungumzia mambo mengi makubwa ya msingi.
Karibu uangalie kipindi hiki hapa
Mpinzani vocal kama Zitto Kabwe, kualikwa kipindi cha TBC sio mchezo!. Hata Tundu Lissu na Godbless Lema wakirejea nyumbani wana alikika.
Big up sana kwa TBC
Paskali