TBC aibu tupu kwa taifa

Tido uko wapi bado tunakuhitaji. Hawa jamaa waliobaki wanaburuzwa tu hawana ubunifu
 
Tido uko wapi bado tunakuhitaji. Hawa jamaa waliobaki wanaburuzwa tu hawana ubunifu

Mmmh...

Hivi ndugu yangu, huoni hata management iliyopo pale TBC, nani mbunifu? Kilichopo ni kilio tu kwa Taifa la Tanzania!

Binafsi sijui na ninajiuliza maswali mengi bila majibu juu ya Taifa hili na wanao jiita viongozi wanaweza nini. Eti tumethubutu, tumeweza na tunazidi kusonga mbele kwa lipi lenye tija kwa Taifa la Tanzania? Nyimbo nyingine ....hah!
 
Ni aibu kubwa sana kwa Taifa au jamii kukosa vazi la taifa ambao ndio unakuwa utambulisho wenu mnapokuwa ndani au nje ya mipaka ya nchi yenu.

Hebu nitazameni mimi hapo kwenye avatar yangu nikiwa na vazi letu la taifa. Je kwa vazi hilo si unaweza kujua natoka nchi gani.

Fungukeni na mtafute utambulisho wenu kitaifa na kimataifa.

Siyo lazima kuchangia. Kama hauna la kuchangia soma tu michango ya wenzako na utulie!
 
Mkuu unajadili TBC hapa tena ? Ni sawakutaka tumjadili Sitta , Mwakyembe , Kilango eyi wapambanaji na ufisadi au Napena porojo zake .Okoa muda wako mkuu fanya la maana au acha kuandika juu ya hawawatu .
 
Heh mi nilijua kikao kimekua postponed, maana nilikua kila nikichungulia hamna kitu! Kumbe ni mambo tu ya tv ya taifa dah!
 
Aibu tupu kuita tbc tv ya taifa, tv za taifa za mataifa yote africa zinaonesha mashinda ya mpira ya africa lakini tbc hawaoneshe, Toka Tido mhando alipo ondolewa tbc hakuna jipya tena

Tido aliondoka na mvuto wote wa tbc,sasa hv wamebaki kuonekana ni kichekesho tu!tbc+clouds = bure kabisa!
 
tbc hakuna kitu,taalifa ya habar ina stack kila siku samahan tumewachoka
 
Kikao Muhimu cha bunge kinaendelea Dodoma na TV ya taifa ni lazima si ombi kuwaonyesha wananchi wake kitu ambacho wawakilisho wao wanakijadili Bungeni.
Cha ajabu hii tv inakatika katika na tangazo kubwa wanalotuwekea ni VAZI LA TAIFA. no excuse nothing, So shame for the great Nation which we are all proud of it.
DR's still on strike to wake up the Government
TBC Mbwa wa polisi wa CC Magamba!
 
hiyo TBC ilishakufa tangu walipomtoa TIDO MHANDO sasa hivi imekuwa kaputi wanauza ving'amuzi vya STARTIMES tu, sasa hilo vazi la taifa wanalolishadadia eti rangi zake lazima ziwe za bendera sas hapo wanatafuta nini kama rangi za bendera zajulikana si washone magauni, sketi, kaptura na suruali? NIGERIA hata wakivaa rangi nyeusi wanatambulika nayo iko kwenye bendera yao? UPUUZI MTUPU KAMA SIO WIZI MTUPU!.
 
ukitaka kujua uzembe wa TBC angakia website yao, Check updates zao, hawana schedule za TV nk - halafu wenyewe wanaiita tbc international!
 
Ni aibu kubwa sana kwa Taifa au jamii kukosa vazi la taifa ambao ndio unakuwa utambulisho wenu mnapokuwa ndani au nje ya mipaka ya nchi yenu.

Hebu nitazameni mimi hapo kwenye avatar yangu nikiwa na vazi letu la taifa. Je kwa vazi hilo si unaweza kujua natoka nchi gani.

Fungukeni na mtafute utambulisho wenu kitaifa na kimataifa.
Si kitu cha ajabu kukusikia wewe ukisema mambo kwa kuzingatia tumbo lako litavimbiwaje na si maslahi ya watanzania, kwa sababu waliokutuma wanajua wanachokifanya na wanajua hilo vazi la taifa ni njia mojawapo kati ya njia nyingi ambozo wamekuwa wakijaribu kuzitumia kuwasahaulisha au kuwatoa watanzania katika kujadili vitu mhimu zaidi vinvyo athiri maisha yao. Sasa hiyo posho unayoipata itakutokea puani siku moja watanzania si wale wa zamani wa kuyumbishwyumbishwa tuna msimamo na tunaelewa kinachoendelea ni nini!! Labda kwa ushauri wangu mwambie mwajiri wako kuwa kazi unayoifanya ina impact katika kuwabadilisha watanzania ili uendelee kutwaa posho ya kujaza tumbo lako na watu wa jamii yako. itakusaidia walau kwa kipindi kifupi kabla boss wako kugundu alikuwa anadanganya, huu ni ushauri wa bure
 
Hapa Zanzibar mambo nje kabisa ,msongo mzima wa baraza la Wawakilishi unaonyweshwa LIVE na hata redio nazo zinatangaza ,hongera station za Hapa kijiweni.
 
Hivi nchi zenye vazi la taifa zilipataje vali hilo? Walifuata utaratibu kama huu tunaopewa sisi? Vazi linapigiwa kura kama mbunge!!
Lakini nani atavaa hilo vazi na kwa uda upi? Kazini au katika sherehe?
Kwa nini vazi la taifa sasa na si kabla?

Mkuu naunga mkono mashaka yako.
Hilo linalosemekana ati ni vazi la taifa ni kupoteza muda na rasilimali za taifa.
Ni muono wangu, hakuna atakayelivaa ukiondoa waliolibuni.
Jaribu kurudisha fikra zako kipindi Tanganyika tunapata uhuru kutoka kwa Mwingereza.
Viongozi wetu wakuu enzi hizo Mwl. Nyerere na Mzee Kawawa walijaribu sana kuwavutia japo si kwa shuruti watanganyika kuvaa migoroli mfano wa mavazi ya nchi ya Ghana. Nini kilitokea? hawakupata kuungwa mkono.
Mwl. Nyerere baadaye akaja na vazi maarufu la waziri mkuu wa China al maarufu CHOU EN LAI, baadhi walijitahidi kulivaa miaka michache wakarudi katika mavazi wanayoyapenda.

Vazi la taifa halibuniwi, bali ni muendelezo wa utamaduni wa walivyokuwa wanavaa mababu, zaidi ni uboreshaji tu. Kwa nchi yenye makabila mengi kama Tz, ni vigumu sana.

Hivyo nakuhakikishia, watapiga kelele na hilo vazi, watatumia raslimali lukuki za wa-Tz kulibuni, lakini halitavaliwa na wengi. Na mwisho litaishia.
 
ni kweli kabisa tangu tido aondolewe TBC imeshuka sana tarifa za habari ni aibu tupu, watangazaji wanapata aibu pale mchanganya picha za matukio anaposhindwa kuunganisha picha za matukio yanayofuata.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom