mxyo16
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 1,243
- 760
- Thread starter
- #101
#MXYO16 shukrani maana kwenye nyuzi joto chini ya 0 na zaidi (-ve) pia kuna viumbe wanaishi pia nahisi the same applied kwenye nyuzi joto kubwa zaidi kama kwenye jua....mashaka yangu ni kwamba wanasanyansi wanaweza kuja na kubisisha juu ya uwepo wa viumbe huko sababu hawajawai kufika huko wala hawajafikiria kufika huko....kusema hivyo naamanisha kama hujafika huwezi jua kuna nini huko....na kama kuna kiumbe kinachaomudu kuishi kwenye joto kali hivyo pasi na shaka kwenye hali kama yetu hapa Dunian au sayari nyingine yeyote haviwezi kuishi...ni ngumu kuonekana na wanasayansi.
katika sayari ya kwanza baada ya Jua nikimaanisha ZEBAKI "Mercury" waweza kuta pana viumbe pia, japo cha kujiuliza mbona sayari hiyo haiyeyuku kwa joto kali hivyo?! wakati huku duniani ni shida saana kwa mateso ya joto la jua tumeshuhudia visiwa vikipotea watu kufa huko India kwa joto kali barafu kuyeyuka...hali ipoje Venus na Mercury??
Kilichombo sijui space ship ilituma picha ya mwonekano mpya wa sayari ya Pluto kimefikia wapi kwa safari yake ya kwenda huko pluto?? wanasayansi wakati mwingine nashindwa waelewa....are they done with Mars na Mwezi so leo wamefunga safari ya kwenda Pluto?? au possibility ya uhai ni kubwa huko pluto kuliko hapo Mars, Jupita?
Kwakweli nia mojawapo ya uchunguzi wa anga ni kujifunza nivipi mwanadamu atawezaje kuishi comfortable na kutatua matatizo yake kiurahisi kila yanapotokea....kitu kimoja kinacho fanya tuishi ni kuwepo kwa atmosphere....hii inatulinda sana na miale hatari ya jua kama unavyoona katika picha ya mwanzo...hii amosphere haipo kwenye sayari zingine na maisha yetu ya kisasa hivi atmosphere layer yake inapungua, kwahiyo ni hatari kwa maisha yetu baada.....sasa tukaishi wapi?
either tutafute mbinu za kujiokoa hapahapa duniani au kutafuta sayari mbadala, mercury na mars hazisapoti mwanadamu kuishi huko, lakini kuna mission inaandaliwa kupeleka watu mars. nadhani ipo mission nyingine ya kupeleka mtu mwezini...
kuna majaribio kisayansi kuona je upo uwezekano wa kuhamia sayari nyingine na kutengeza atmosphere, maji, oxygen, gravitation force na kuishi huko.......hii inawezekana ila iwe yakutosha na sustainable...nadhani ndio dili la wanasayansi in the future.
Hii kuhangaika kote ku explore anga ni kutazama possibilties kwamba siku ikionekana solar system, jua au dunia haitaweza kusapoti maisha ya binaadamu then tusepe sehemu itakayo kua bora zaidi.....Au kama time travel itakuja kuwezekana basi watu wataweza kusafiri future na kujua yanayokuja na kurudi nyuma either kuzuia yatakayo tokea future au ku improve....Imagine unasafiri miaka ya nyuma kuzuia ajali, au kupeleka dawa iliyogundulika kipindi hiki....ni mawazo ya kisayansi zaidi....
Kama ulivyodokeza kwamba viumbe wanaishi kwenye mazingira magumu, hili jambo kwa wanasayansi linaleta opportunity kujifunza viumbe hawa wana features zipi....ili kutuwezesha ku develop hizo features kumsaidia mwanandamu kupambana na mazingira hayo...katika kutengeneza vifaa mbalimbali ambavyo kwasasa vinaathirika vikikutana na hali hizo.....tatizo mfano uokoaji wa watu panapozuka moto....
Chombo ambacho kinaleta picha za pluto kwasasa na hata majuzi, kinaitwa new horizon, kilitoka hapa duniani mwaka 2006, kwa spidi ya 36000 mph kiliupita mwezi ndani ya masaa 9. kilifika Pluto zaidi ya maili 3 billions, July 2015, imetuma picha ambazo ili caputure mwezi huo zinafanyiwa kazi kwasasa mabara na kutolewa kila zinapokua tayari, majuzi hapa wametoa picha hizi hapa kwasasa chombo kinaenda eneo lingine
cheki safari ya hiki chombo na kilipo kwasasa