Tatizo la WiFi hotspot na USB teethering kwenye HTC naomba msaada

Tatizo la WiFi hotspot na USB teethering kwenye HTC naomba msaada

kijumbamshale

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2011
Posts
267
Reaction score
88
Wadau naombeni msaada nina simu yangu hapa HTC nimeagiza Marekani ilikua inatumia mtandao wa verizon. Simu hii wameifunga haiwezi kufanya teethering ya usb wala kutengeneza wifi hotspot wakati mimi nahitaji sana hizi huduma nifanyeje?

Nb: Vitu vingine vyote viko poa kabisa.
 
Nenda Play store na udownload application yaitwa FoxFi...

Bila shaka baada ya hapo utakuwa umetatua tatizo lako...

Jamaa wa Verizon wamezuia feature ya tethering ili tu data plan zao zitumike kwa device moja pekee...
 
Nilikutana na hilo tatizo kwenye htc Verizon, wakati matumiz yangu 50% lazma nifanye tethering. Ikabid niuze nitafute hata ka s4
 
Samahani kwa kuingilia thread, mi simu sumsang duos muundo kama blackberry tangu jana nikiwasha data connection inakubali lakini haifanyi kazi yaani haileti alama ya H au E pale kwenye sehemu ya mtandao, ni setting gani nimevuruga ndugu zangu?
 
Nilikutana na hilo tatizo kwenye htc Verizon, wakati matumiz yangu 50% lazma nifanye tethering. Ikabid niuze nitafute hata ka s4

Pole...

Hukufanya uamuzi sahihi kuuza maana solution ipo...
 
Samahani kwa kuingilia thread, mi simu sumsang duos muundo kama blackberry tangu jana nikiwasha data connection inakubali lakini haifanyi kazi yaani haileti alama ya H au E pale kwenye sehemu ya mtandao, ni setting gani nimevuruga ndugu zangu?

Pamoja na alama hizo kutoonekana, je unaweza kufungua mitandao?
 
watu8 solution ni nini maana niliyopewa hapo juu haikufanikiwa
 
Inaniletea maandishi hayo hapo hata baada ya kutumia foxify na ile chief aliyoshauri
 
Attachments

  • 1422160967957.jpg
    1422160967957.jpg
    43.7 KB · Views: 211
Inaniletea maandishi hayo hapo hata baada ya kutumia foxify na ile chief aliyoshauri

ina maana kubypass imeshindikana, endelea na foxfi ya watu8 ina option ya usb tethering ila itahitaji uichakachue/ulipie then udownload na software yake ya pc. nafkiri wanatumia driver tofauti hawa jamaa huwenda ukafanikiwa kubypass verizon security.

pia kama umeroot unaweza kumodify system file mwenyewe ila njia hii tumia ikiwa njia zote zimeshindikana maana ni hatari kwa simu yako
Hotspot bypass for Verizon Kit Kat? : lgg2
 
Last edited by a moderator:
Wakuu naomba niingilie uzi huu.

Smart phone HUAWEI y- 518 haishiki 3g wala H ila inashika E muda wote na mahali ambapo hata 3g inapatikana. Nimewasiliana na tigo pia voda wamenipa setting lkn hata baada ya ku install tatizo bado Lipo.

Msaada wenu.
 
Kichwa Ngumu

Naomba kuuliza H na E humaanisha nini waungwana yangu huandika E WHAT THAT MEANS? Wengi humu hatufahamu mambo mengi sana
 
Last edited by a moderator:
Naomba kuuliza H na E humaanisha nini waungwana yangu huandika E WHAT THAT MEANS? Wengi humu hatufahamu mambo mengi sana

H ni internet yenye speed kubwa

E ni internet yenye speed ndogo

ila H inakula sana battery hivyo husababisha simu kutokukaa na charge wakati E yenyewe haili sana battery hivyo simu hukaa na charge
 
H ni kifupi cha HSPDA na E ni Edge maelezo mengine ni kama alivyoeleza chief
 
Wakuu naomba niingilie uzi huu.
Smart phone HUAWEI y- 518 haishiki 3g wala H ila inashika E muda wote na mahali ambapo hata 3g inapatikana. Nimewasiliana na tigo pia voda wamenipa setting lkn hata baada ya ku install tatizo bado Lipo.
Msaada wenu

configuration za mtandao za internet haziwezi kusaidia kuchange baina ya 2g na 3g unatakiwa uchange setting za simu

nenda setting kwenye simu yako halafu angalia juu kama kuna option ya mobile network kama hakuna click more network then utaiona mobile network, click hio then chagua network mode

wcdma/umts/hspa hii ndio 3g

edge/gsm/gprs hii ni 2g

chagua unapotaka utakuwa umewezesha simu yako kutumia 3g
 
H ni internet yenye speed kubwa

E ni internet yenye speed ndogo

ila H inakula sana battery hivyo husababisha simu kutokukaa na charge wakati E yenyewe haili sana battery hivyo simu hukaa na charge

Heshima mkuu nashukuru!
 
Wakuu naomba niingilie uzi huu.
Smart phone HUAWEI y- 518 haishiki 3g wala H ila inashika E muda wote na mahali ambapo hata 3g inapatikana. Nimewasiliana na tigo pia voda wamenipa setting lkn hata baada ya ku install tatizo bado Lipo.
Msaada wenu

Huawei Y518 ni dual SIM ambapo slot moja ni kwa ajili ya GSM network na ya slot ya pili ni kwa ajili ya TD-SCDMA.

TD-SCDMA ni aina ya 3G network ambayo inatumiwa huko China...

Tanzania hatupo katika standard hiyo pamoja na kwamba carriers wetu wana 3G network. Bongo sisi tumekuwa standardized kwa WCDMA kwa traffic zote za 3G...

Hivyo wewe unapata data kwa kupitia slot ya GSM pekee na utakuwa limited kwenye Edge (E) pekee...

Kabla ya kununua simu hizi za Wachina au Wakorea muwe mnafanya review ya matoleo ya simu.

cc Chief-Mkwawa
 
Last edited by a moderator:
Inaniletea maandishi hayo hapo hata baada ya kutumia foxify na ile chief aliyoshauri

Mkuu hebu ngoja nifuatilie zaidi kujua nini tatizo...so far kwa US hiyo option ina work.

Labda niulize, HTC yako ni toleo gani?
 
Back
Top Bottom