Tatizo la simu kuonesha 'internal memory full'

Abuwhythum

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
829
500
Nina simu aina ya Samsung Galaxy A30, kila mara inaonesha internal memory full, na inashindwa ku-operate kabisa, hadi ninalazimika kuzima simu na kuiwasha tena ndio kidogo inakuwa na free space.

Ikizingatiwa sijaweka vitu vingi vya kuifanya ijae. Sasa ninashindwa kuelewa iwapo hii simu ni fake au tatizo ni nini? Maana simu ina internal ya 64GB.

MSAADA JAMANI KWA MWENYE USHAURI WA JUU YA NINI NIFANYE ILI KUONDOA TATIZO HILI.
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
25,978
2,000
Nina simu aina ya Samsung Galaxy A30, kila mara inaonesha internal memory full, na inashindwa ku-operate kabisa, hadi ninalazimika kuzima simu na kuiwasha tena ndio kidogo inakuwa na free space.

Ikizingatiwa sijaweka vitu vingi vya kuifanya ijae. Sasa ninashindwa kuelewa iwapo hii simu ni fake au tatizo ni nini? Maana simu ina internal ya 64GB.

MSAADA JAMANI KWA MWENYE USHAURI WA JUU YA NINI NIFANYE ILI KUONDOA TATIZO HILI.
Nenda setting Kisha tafuta storage Iache sekunde kadhaa itakuonesha stats muhimu za storage yako kutokea hapo utapata mwanga vitu gani vinajaza simu.
 
cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
25,332
2,000
Ukiitimazama bila kuchukua hatua.. itazima kabisa..

Kwa haraka nenda settings - Apps- fungua moja moja - clear cache

Sort kwa size uanze na kubwa..
 
danielhipoliti

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
533
1,000
Nenda settings then apps chagua zile unazotumia sna
Mfano Instagram I click then then kuna sehemu mbili clear storage na clear caches

Uki clear storage ni sawa kbsa na app ambayo umeidownload then unaanza upya data zote zinafutika

Uki clear app baadhi ya data muhimu aziwezi kufutika ila junk files zote zina kuwa cleared
Caches zinapatikana wapi mkuu kwenye simu..?
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,072
2,000
ukiona others,maana yake apps unazotumia zimekuwa na kitambi.

kama una telegram ni ya kwanza inawezakuwa na mafile makubwa sana ila hujaruhusu yaonekane kwenye gallary.

ya pili whatsapp,nayo ni hivyo.

ya tatu ni snapchart,nayo mnajaza sana mapicha na mavideo linanenepa sana.

hakafu kuna facebook,hii sio sana maana ni ngumu kula gb nzima hata inenepeje.

kagua hizo halafu uone mabdiliko
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom