Tatizo la Rais Magufuli ni hili

Tatizo la Rais Magufuli ni hili

Hakuna reform inayogusa huduma muhim za jamii halaf reform gan inafanywa na mtu asiyejua hata anachokifanya?
Inawezekana kiongozi wewe ndio hujui rais anafanya nini. Wengine tunaelewa. Anaboresha mfumo wa uwajibikaji, anaimarisha uendeshaji wa mashirika ya umma, anatetea haki za wanyonge katika ardhi na mengineyo. Wewe umeangalia maslahi yako nenda kiundani zaidi utaelewa
 
Inawezekana kiongozi wewe ndio hujui rais anafanya nini. Wengine tunaelewa. Anaboresha mfumo wa uwajibikaji, anaimarisha uendeshaji wa mashirika ya umma, anatetea haki za wanyonge katika ardhi na mengineyo. Wewe umeangalia maslahi yako nenda kiundani zaidi utaelewa
Anatetea haki za wanyinge wapi?wanyonge washamuona anawatumia kujikosha,watoto wa udom aliowafukuza ni wa nani?kazuia ajira,mikopo hakuna yaani huyu anaaribu mazuri aliyoyakuta kwa kujifanya anabana matumizi.huyu ndugu ni mzigo tz sasa
 
Naogopa sana mbona manung'uniko yamekuwa mengi?? Maana hata waliokuwa wanasupport wananung'unika...ngoja tuone
😀😀😀😀
Mambo si mambo huku mtaani, ndio sababu hata watawala wa zamani wananung'unika kimya kimya.
Tumpe muda
 
Tatizo umezoea dili, kwa hiyo aendelee kuzurura, ahachane na wafanyakazi hewa watafune hela zetu, aliyekuambia serikali anaajiri wahitimu wote ni nani??? NAKUULIZA????? Kama tuna wahitimu ambao hawawezi kutumia ujuzi wao kupambana na mazingira wanayoishi wanasubiri ajira ya serikali! Maendeleo yatakuwa mbali sana
Unasahau pia elimu inayotelewa Na serikali ya ccm ndio inawafanya waone kuajiriwa ndio only option sababu elimu walioipata haiwanyi kujiajiri
 
Inawezekana kiongozi wewe ndio hujui rais anafanya nini. Wengine tunaelewa. Anaboresha mfumo wa uwajibikaji, anaimarisha uendeshaji wa mashirika ya umma, anatetea haki za wanyonge katika ardhi na mengineyo. Wewe umeangalia maslahi yako nenda kiundani zaidi utaelewa
Kuna haki za wanyo ge zaid ya huduma za afya?
 
Tutalia na nani?.nani atatufuta machozi?eee mungu baba utuhurumie waja wako,kama ni kweli raisi analetwa na mungu vp mbona sie umetuletea huyu?
[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] Tanzania I love you.
 
Watakatifu wote ni binaadamu na sio malaika. Hakuna binaadamu yoyote ambaye ni mkamilifu.
Pasco
Iman inakupotosha!! Hakuna binadam mtakatifu wewe tafuta biblia nzima msidanganywe na mapadri wenu !! Mtakatifu ni Mungu
 
Watumishi wa umma mmeambiwa muendelee kuvuta subira hadi February mwakani. Kuweni Na subira

Mkuu kuna official ststement imetolewa inasema hivyo au ni zile threads za Nkanga Chief zilizopelekea apigwe BAN?
 
Inawezekana kiongozi wewe ndio hujui rais anafanya nini. Wengine tunaelewa. Anaboresha mfumo wa uwajibikaji, anaimarisha uendeshaji wa mashirika ya umma, anatetea haki za wanyonge katika ardhi na mengineyo. Wewe umeangalia maslahi yako nenda kiundani zaidi utaelewa
Anatetea haki gani ya wanyonge?
Km mnyonge leo hii umezuia ajira zake, umeondoa mkopo, umeondoa fao la kujitoa, hospital hazina dawa, watu hawajalipwa mishahara miezi 7, umeondoa posho na hajapandisha watu madaraja.
Haki gani hiyo anayoipaigania? Angekuwa anapigania hiv vyote vingeenda sambamba .
He is a sadist na ana uwezo mdogo wa kufikiria na kufanya kazi.

Hiv kwa mfano. Ww ni dokta halafu unawaambia wagonjwa warudi nyumbani na huwezi kutibu kwa miezi 3 sbb unafanya ukarabati wa majengo ya hospitali na kununua vifaa. Je, wagonjwa watakuelewa? Ma je, utakuwa mtetezi wa wagonjwa?
Je, kwann usikarabati majengo na kununua vifaa huku unatibu wagonjwa?

HAPO NDIYO HUJUE KUWA UNA UWEZO MDOGO WA KUFIKIRIA NA KUFANYA KAZI
 
Alikuwa Nyerere Watanzania mlimuona mbaya mkampa na jina la Musa,,
1: Akaja Mwinyi na sera yake ya Ruksa naye hakutoka salama kwa kulalamikiwa kuwa uchumi wa nchi ulishuka fedha yetu akaiporomosha thamani yke,,
3: Akaingia Mkapa,, akajitahidi kuinua uchumi wetu na kuifanya fedha yetu irudishe heshima yke mipakani mwa jirani zetu,, hata alipo ondoka akasema bila kumung,unya maneno kwamba ameacha Hazina yetu imejaa fedha tele za nje na ndani,, aliye mrithi naye akakili mbele yetu kuwa ni kweli amekuta fedha nyingi ndani ya Hazina ya taifa,,
Lakini Mkapa pia hakutoka salama walimwita ,,Ukapa ,,na lawama nyingi zisizo andikika hapa.
4:Akaja Kikwete ,, huyu sina haja ya kueleza mengi alifanya nchi kuwa ni shamba la bibi,, kila mwenye kucha na meno makali alijikatia apendavyo mali za umma. Huyu Ufisadi wa aina zote ulifanyika ktk utawala wake ,, yeye akatoka na jina la mzee wa Trip na kucheka cheka.
Eti kwamba muda mwingi alikuwa anazurura nje huku watu Waki Escrow,, Epa,na Kurichmond mali za umma.
5: Sasa kaja Msukuma ana uchungu wa ardhi ya kwao ilivyo achwa mashimo baada ya wajanja kuondoka na madini yote waliyoyakuta kule Ardhini,,
Amekuja na machungu ya wizi wa makontena na mafuta pale bandarini,, amekuta nchi imejaa hewa kila kona ya sekta ya umma,, amekuta Hazina haina hata Sumuni ndani yake,,
Amekuta Madeni yamejaa kila kona ya ndani na nje.,
Kwa kifupi amekuta nchi imeoza ngozi yote inatoa harufu,, sasa anaanika juani ngozi ikauke apunguze harufu ndani pado tena Watanzania tunalalamika tu,,

Hivi tunataka tupewe Rais wa namna gani?kama wote Hawakutufaa na huyu naye tunaona hafai tunataka aje malaika kutuongoza?
 
Sio kwamba ni mtu mbaya au ana nia mbaya ila tatizo lake sina uhakika anajua anachokifanya. Tatizo lake kubwa ni kuharibu mema aliyoyakuta kuwa mapya, haimaniishi waliopita waliyotenda yote ni mabaya ila kuna mazuri.

Tatizo lake ni pale anapoharibu yale mazuri aliyoyakuta kama vile
Mikopo ya elimu
Madawa hospitalini
Demokrasia
Uhuru wa habari
Ajira kila mwaka
Kupanda madaraja na mishahara

Angeweza kuwa bora na kuonekana bora sana kama angefanya anayoyafanya bila kuathiri aliyoyakuta. Sasa unapotafuta watumishi hewa huku hutaki kuajiri na kupandisha watu madaraja hatuwezi kuona umuhimu wa kutoa watumishi hewa.

Sasa unaponunua ndege ilihali watu wanakosa madawa hatuwezi kuona kama kununua ndege kuna umuhimu. Sasa unapopunguza mishara ya wakubwa wakati ya wadogo inakushinda kupandisha hatuwezi kukuelewa.

Rais acha kuharibu mazuri uliyoyakuta bali yaendeleze.
Sio rahisi kumjua kichaa ila kwa maneno na matendo yake, tumeingia choo cha kike
 
Back
Top Bottom