Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Kuna muda ni lazima ukweli usemwe maana usiposemwa lazima kumbukumbu zitakuwa za upotoshaji Mkubwa
Kwenye Tatizo linaloikumba Tanzania la ukame na ukosefu wa Maji kwa sasa lawama zangu zote nazipeleka kwa watu wafuatao
1. William Lukuvi
Akiwa Waziri wa Ardhi kuanzia Awamu ya Tano, nchi yetu imeshuhudia urasimishaji mkubwa sana wa Mapori ya akiba pamoja na hifadhi kuwa makazi ya watu!
Jambo hili limepelekea kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana uharibifu wa Mazingira hasa ukataji Miti wa kutisha kwenye mapori mengi yaliyokuwa yanategemewa kuleta mvua uliofanywa na Jamii za wafugaji na wakulima hasa kwenye mikoa ya Katavi, Rukwa, Tabora, Morogoro, Pwani na kusini mwa Tanzania.
Mfano wa hili nimejionea kwenye Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora inayoongoza kwa kuwa na Misitu mingi.
Kwenye mikoa hii kumekuwa na uvamizi sana wa maeneo yenye mapori na misitu ya asili unaofanywa na Jamii za watu wa mikoa ya kanda ya ziwa na nchi jirani za Rwanda na Burundi. Watu hawa wamekuwa wakikata miti kwenye mapori kwa Kiwango cha kutisha na hata sasa takwimu zimeanza kuonesha hivi karibuni mito iliyokuwa ikititirisha maji mwaka mzima kwenye mikoa ya Kigoma na Katavi bila kusahau Rukwa imeanza kukauka kutokana na shughuli hizi za binadamu.
Waziri Lukuvi akiwa waziri wa Ardhi badala ya kushauri Serikali watu hawa waondolewe kwenye maeneo haya na kurudishwa kwenye maeneo yao ya asili yeye amezidi kushauri serikali watu hawa kurasinishwa kwenye maeneo hayo. Hivyo tusilaumu mtu. Tatizo ni Lukuvi
2. Mawaziri wa Mazingira kuanzia Awamu ya 3, 4, 5 na huyu wa Awamu ya 6
Hii ni Kwa sababu Nchi yetu imekuwa na Mawaziri wa Mazingira kwenye Awamu zote. Ila kamwe nchi hii haijawai kuwa na kampeni kubwa ya upandaji Miti.
Kila siku watu wamekuwa wakisema juu ya ukame na ukataji mkubwa wa Miti Ila kusema kweli Mawaziri wa Mazingira hawajawai kuanzisha kampeni ya Kitaifa kubwa inayohusu upandaji miti yenye lengo la kuhakikisha nchi inakuwa na misitu mingi, mapori mengi ivyo kuwa salama dhidi ya majanga ya ukame.
Kwa Waziri wa Sasa wa Mazingira Suleiman Jaffo huyu ndo naona ameshindwa kabisa kazi yake maana hata suala la mifuko ya plastiki naona linaanza kurejea kwa kasi sana. Ukitembea kwa basi kutoka Dar kuelekea mikoani hali unayoikuta barabarani inasikitisha. Kuna mifuko mingi ya plastic na materials nyingine za plastiki zimetupwa kando ya Barabara hadi unafikia kujiuliza Kama kucontrol plastiki au usafi tu inatushinda kwa nini tuwe wa Waziri wa Mazingira au Wakuu wa Mikoa na Wilaya?
Nilikuwa Mkoani Dodoma siku si nyingi nikaona hadi Kuna vibanda vya chips vimeanza kuwafungia wateja wake chips kwenye mifuko ya plastiki. Waziri Jafo lawama zangu haziwezi kukuacha kwenye hili maana unamuangusha Mama Samia. Kama huwezi kazi sema.
Hatari ninayoiona mbeleni
1. Sasa tumeanza ona baadhi ya sehemu zinapata mgao wa maji na umeme kutokana na ukame unaosababishwa na maamuzi mabovu pamoja na usimamizi mbovu ubaofanywa na watu walioaminiwa na kupewa madaraka. Hali ikienda hivi ninaona nchi ya Tanzania ikishindwa kuzalisha umeme wa kutosha na baadae chakula cha kutosha.
Tukishindwa kuzalisha umeme wa kutosha kutokana na ukame Mradi wa Bwawa la Nyerere utaonekana rasmi kuwa mradi ulioliingizia Taifa hasara kutokana na kushindwa kuzalisha umeme uliotarajiwa pamoja na kujengwa kwa gharama kubwa.
2. Naona baadae Taifa litakuwa tegemezi na gharama za maisha kuongezeka maradufu jambo linaloweza kuleta hatari kwa kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kutokana na nchi kuanza kuwa tegemezi kwenye nishati na chakula!
Tuchukue hatua sasa