DOKEZO Viongozi hawa Mamlaka ya Maji Singida (SUWASA) ni tatizo, Waziri Aweso sikia kilio chetu Watumishi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) ni Taasisi ya Serikali inayotoa huduma ya maji safi katika Mkoa wa Singida kwa zaidi ya miaka 20 sasa, ipo chini ya Wizara ya Maji inayoongozwa na Waziri Jumaa Aweso.

SUWASA inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Sebastian V. Warioba ambaye katika majukumu hayo ana mwaka mmoja na nusu, awali alikuwa DUWASA (Dodoma) akiwa Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano.

Binafsi ninaona huyu mtu hatoshi kabisa katika nafasi hiyo kutokana na tabia zake ambazo haziendani na nafasi ya cheo alichonacho kwa kuwa kama kiongozi kuna baadhi ya mambo unapoyafanya ni wazi yanaonesha hauna uwezo wa kuongoza jumuiya ya watu.

Moja ya changamoto zake ni kuwa ni mbishi na anapenda sana ligi kama yuko kijiwe cha kahawa.

Wanaokumbuka huyu bwana alitumbuliwa na JPM kwa kumtishia Askari wa usalama barabarani kwa matusi na maneno ya shombo ikiwemo kumnyooshea bastola.

Baada ya kukaa benchi muda mrefu, akaonewa huruma, karejea kwenye kazi anaanza kurejesha dharau na mienendo yake kama ilivyokuwa awali.

Kibaya zaidi amekuwa mgumu kupitisha stahiki za wafanyakazi lakini yeye anasafiri hadi anajilipa siku za ziada ambazo siyo sahihi.

Mfano anasafiri kwa siku 3 ila anajilipa malipo ya siku 8, hafanyi vikao na Wafanyakazi anaowaongoza, mara nyingi amekuwa kiongozi anayeogopa vikao.

Watumishi waliochini yake wanaishi na malalamiko chungu mzima.

Uongozi wa juu umtazame kwa mara ingine, kuna shida inakuja ikiwa hili halitafanyiwa kazi mapema.

Wafanyakazi hawamtaki anapenda majungu, amewagawa Wasaidizi wake hadi imefikia hatua kila mtu anaishi kama mkimbizi.

Mkurugenzi Mtendaji huyu amejiunga na Afisa Manunuzi, Anthony Kenyunko kukwapua fedha za SUWASA na akishazichota inadaiwa anaenda Nchini Marekani ila anadanganya kuwa yuko kwao.

Magari yamekufa gereji kwa ununuaji wa vifaa visivyo na ubora, tunaomba viongozi hawa wawili wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuwa pamoja na kufanyiwa vetting lakini bado hakuna la maana wanalofanya.

Hatutachoka kupaza sauti hadi kilio chetu kisikike, juzi Mama SSH amekuja na kwa kuwa vilio vyetu viko katika pipeline, tunakuwa wavumilivu kwa kipindi fulani, baadaye tutaamua vinginevyo.

Kiongozi huyo anaamini anajua sana na anajua kila kitu, amekuwa akikiuka maadili ya kazi kwa ulevi kiasi kwamba kuna muda anashindwa kufika kazini.

Haki zetu zinazuiwa kwa maneno ya kashfa, kiongozi mkuu wa taasisi anaturekodi na simu yake tukiwa tunaongea nae ana kwa ana, je hayo mazungumzo anampelekea nani na ili iweje?

Kila kiongozi huwa anachangamoto zake, ila hawa wawili wamezidi na HATUWATAKI, Waziri Aweso ingilia hii changamoto.
 
Back
Top Bottom