chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,805
- 29,436
Usingizi ni kitu muhimu katika maisha ya mwanadamu.Mtu mzima(adult) anatakiwa alale masaa 6-7 kwa siku.
Tatizo la usingizi limegawanywa katika makundi matatu
1.Tatizo la kuanza kulala
2.Tatizo la kushtuka hovyo(kutokulala usingizi mzito)HIGH RAPID EYE MOVEMENT
3.Kushindwa kulala kabisa
Zipo dawa za usingizi kwenye group linaloitwa BENZODIAZEPINE na BENZODIAZEPINE LIKE DRUGS.mfano ZOPICLONE/ZOLPIDEM,SOBRIL...ila hazitakiwi kutumiwa kwa muda mrefu zaidi ya wiki 2-4 kwasababu unakuwa addicted nazo yaani utakuwa huwezi kulala bila kula hizo dawa.
Jinsi ya kutatua tatizo la usingizi
1.Lala kila siku kwa wakati maalum mfano kila siku saa nne
2.Epuka kulala mchana
3.Epuka kunywa chai/kahawa usiku
4.Weka chumbani katika madhari nzuri kuwe na hewa safi ya kutosha
5.Epuka kutumia computer,ipad,simu kitandani/chumbani
6.Kabla kulala jaribu kuupumzisha mwili ili iwe tayari kiakili kwaajili ya kulala sio uanze kupiga deki robo saa kabla kulala
7.Epuka kulala na njaa au ukiwa na shibe
8.Jaribu kuepuka kufikiria sana ukiwa uko katika harakati ya kulala,andika dairy kama una vitu unahitaji kuvisuluhisha jaribu kuvisuluhisha siku ifuatayo.
9.Jaribu kufanya mazoezi/kuwa na activities ili kuuchosha mwili na ubongo
10.Chumba kitumike kwaajili ya kulala tu sio shughuli nyingine 🙂
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/460682-suluhisho-la-kukosa-usingizi.html#post6480726
Shukrani mkuu!!!!!!