Tatizo la Kukosa Usingizi (Insomnia) na tiba yake

Tatizo la Kukosa Usingizi (Insomnia) na tiba yake

Pole sana.
Fanya mazoezi na hakikisha unalala around same time kama ulivyoshauriwa. Pia usile chakula late. Muda mzuri wa kula ni saa moja usiku.
 
nawashukuru nyooote kwa mchango na ushauri wenu, nitazingatia na kufanyia kazi. M/MUNGU awabariki.
 
Habari,nilikuwa naomba ushauri wa kitaalam ,nimekuwa nikipatwa na matatizo ya mwili kukosa nguvu na maumivu ya mgongo kwa muda sasa na kukusa usingizi mara kwa mara,uzito wangu pia umekuwa mdogo kwani kwa sasa nina miaka 27 na kilo zangu ni 41 je hii inaweza ikawa ndio sababu ya maradhi hayo! Au kuna tatizo jingine,najitahidi sana kula ila wakati mwingine sipati hamu ya kula,nimeshaenda hospital kadhaa na wanasema hawaoni ugonjwa wowote,please nahitaji ushauri wenu!
 
Mkuu sina hakika unafanya kazi gani,lakini inawezekana maumivu ya mgongo yanatokana na kazi ngumu au aina ya kitanda/godoro unalolalia.Lakini sina hakika umefanyiwa vipimo gani kuhusiana na tatizo hilo. Kwa uelewa wangu maumivu ya mgongo origin yake inaweza kuwa misuli ya mgongoni(tatizo dogo),inawezakuwa ni mifupa inayojenga uti wa mgongo(tatizo kubwa kiasi) au inawezakuwa kwenye joints za pingili za mifupa ya uti wa mgongo(tatizo kubwa). Matatizo yote haya yanaweza tu kutatuliwa ikiwa utafanyiwa vipimo sahihi ili kuweza kujua ni lipi kati ya hayo;kwakuwa kila moja lina namna yake ya kutibiwa.

Kuna tatizo lingine linaweza kufikiriwa pia,hili ni TB ya mifupa. Ingawa kuna dalili nyingine pia,ila hata yenyewe inasababisha maumivu ya mgongo,kupungua uzito,kujisikia mchovu n.k. Lakini pia hata hili litatibiwa ikiwa vipimo sahihi vimefanyika na kuweza kutambua tatizo hilo.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba matatizo mengine uliyotaja hapo kama kukosa usingizi,kupungua uzito na uchovu is just psychological. Hii inaweza kutokana na kukata tamaa baada ya kuona umezunguka hospt. nyingi bila kupona na hivyo unajikuta unatumia muda mwingi sana kuwaza juu ya tatizo lako! Haya matatizo matatu yanaweza kuwa yanategemeana.Look.. mawazo mengi>>unakosa usingizi>>uzito unaanza kupungua>>mwili unakosa nguvu!
Kuna mengine yanaweza kujitokeza kama vile kukosa hamu ya kula na wakiti mwingine hata vidonda vya tumbo.

Ushauri wangu: nenda kwenye hospitali kubwa ufanyiwe vipimo. Tena itakuwa vizuri ikiwa unaweza kumwona daktari wa mifupa.

Pole sana ndugu yangu.
 
GOLDEN SIX
Golden Six imetokana na mimea sita(six golden herbs) inamaanisha mimea sita yenye thatmani.
Golden six inahusika na sehemu zifuatazo;

  1. Mishipa ya hisia
  2. Figo
  3. Kuinua kinga ya mwili na kinga ikiwa nyingi kwenye mwili inasaidia uroto kwenye mifupa(born marro), ndiyo inatengeneza cell za mwili.
  4. Inapunguza kasi ya kuzeeka kwa kuondoa madhara ya uzee.
Utendaji kazi wa Golden six;

  • Golden six ina kinga kubwa kwenye mwili, ukiitumia vizuri inakwenda kusawazisha kinga kwenye mwili.
  • Inarutubisha uroto kwenye mifupa nah ii hutengeneza chembechembe nyeupe za damu kwa haraka.
  • Golden six inasafisha figo kwa kuipa nguvu ya kusafisha damu, kuondoa sumu mwilini kama vile uric acid.
Uric acid ikiwa kwenye viungo husababisha kuumwa kwa viungo.

  • Kuhisi uchovu
  • Kutokwa na jasho sana
  • Kuumwa sehemu ya chini ya mgongo na pia kukosa usingizi.
Inapunguza kasi ya kuzeeka kwa kuondoa madhara ya uzee mfano;

  • Kupoteza kumbukumbu
  • Kutoona vizuri
  • Misuli kukosa nguvu
  • Chembechembe za mwili kufa kwa haraka
  • Inajenga mishipa ya hisia na kuondoa matatizo ya kupooza
  • Kwa waliopooza na kuathirika kwenye mdomo (mdomo kupinda) katika mazungumzo inawasaidia na kurekebisha mazungumzo yao.
FAIDA ZA GOLDEN SIX

  • Stroke(kupooza)
  • Kukosa usingizi
  • Hypomnesis
  • Kupoteza kumbukumbu
  • Kuumwa na viungo
  • Kusafisha damu
  • Husaidia presha ya kupanda inayosababisha mishipa kubana hii hutokana na aina Fulani ya Adrino gland ambayo hutoa kemikali, husababisha kubana kwa mishipa ya damu.
  • Matatizo ya wanawake na ukomo wa wanawake
WASIOPASWA KUTUMIA
Wajawazito;
Ukitumia Golden Six mwili hutengeneza chembechembe nyeupe kwa wingi ambazo husaidia kinga za mwili, kwa hiyo mama mjamzito akinywa Golden six itasababisha kinga kuwa juu na kupambana na kiumbe kwa sababu ni kitu kigeni kwenye mwili, husababisha kutoka kwa mimba.

Kwa yeyote anayehitaji hii product muhimu, kuuliza pamoja na ushuri anaweza kunipigia kwa namba 0776491294 au kuniandikia barua pepe kupitia ishealthy@hotmail.com
Gharama yake ni Tsh 38000/- tu
 

Attachments

  • GOLDEN SIX.jpg
    GOLDEN SIX.jpg
    148.8 KB · Views: 77
naombeni dawa ya usingizi kwani nachelewa kupata usingizi sana nalala saa tisa usiku kila siku
 
Pole sana. Fanya mazoezi walau mara tatu kwa wiki. Hakikisha unakula chakula cha jioni mapema. Na kunywa maji ya kutosha.
 
Aaah sasa umenisifia tembo atalitia maji.
Ngoja niongezee:
Mtoa mada, jifunze kutokuwa na stress na kuacha nature iflow. Kuna mambo huwezi kuyabadili na kuna mambo sio kazi yako. Pia unapaswa kuwa na ratiba ya kuingia kitandani na wa kuamka. Unaweza pia kuhakikisha unakipenda kitanda chako (nhnua mashuka mazuri na godoro zuri, labda na pazia zuri pia na nightie dress nzuri). Namaanisha kulala isiwe ni basi tu bali tukio zuri kwako.
Ushauri mzuri na effective. Ubarikiwe!
 
Saa moja kabla ya kulala kunywa maziwa fresh motomoto
 
wana jamii forum naombeni mwenye dawa au ushauri kunusiana na tatizo la kukosa usingizi(usingizi wa mang'am mang'am)
 
Usingizi ni kitu muhimu katika maisha ya mwanadamu.Mtu mzima(adult) anatakiwa alale masaa 6-7 kwa siku.
Tatizo la usingizi limegawanywa katika makundi matatu
1.Tatizo la kuanza kulala
2.Tatizo la kushtuka hovyo(kutokulala usingizi mzito)HIGH RAPID EYE MOVEMENT
3.Kushindwa kulala kabisa
Zipo dawa za usingizi kwenye group linaloitwa BENZODIAZEPINE na BENZODIAZEPINE LIKE DRUGS.mfano ZOPICLONE/ZOLPIDEM,SOBRIL...ila hazitakiwi kutumiwa kwa muda mrefu zaidi ya wiki 2-4 kwasababu unakuwa addicted nazo yaani utakuwa huwezi kulala bila kula hizo dawa.
Jinsi ya kutatua tatizo la usingizi
1.Lala kila siku kwa wakati maalum mfano kila siku saa nne
2.Epuka kulala mchana
3.Epuka kunywa chai/kahawa usiku
4.Weka chumbani katika madhari nzuri kuwe na hewa safi ya kutosha
5.Epuka kutumia computer,ipad,simu kitandani/chumbani
6.Kabla kulala jaribu kuupumzisha mwili ili iwe tayari kiakili kwaajili ya kulala sio uanze kupiga deki robo saa kabla kulala
7.Epuka kulala na njaa au ukiwa na shibe
8.Jaribu kuepuka kufikiria sana ukiwa uko katika harakati ya kulala,andika dairy kama una vitu unahitaji kuvisuluhisha jaribu kuvisuluhisha siku ifuatayo.
9.Jaribu kufanya mazoezi/kuwa na activities ili kuuchosha mwili na ubongo
10.Chumba kitumike kwaajili ya kulala tu sio shughuli nyingine 🙂
 
Usingizi ni kitu muhimu katika maisha ya mwanadamu.Mtu mzima(adult) anatakiwa alale masaa 6-7 kwa siku.
Tatizo la usingizi limegawanywa katika makundi matatu
1.Tatizo la kuanza kulala
2.Tatizo la kushtuka hovyo(kutokulala usingizi mzito)HIGH RAPID EYE MOVEMENT
3.Kushindwa kulala kabisa
Zipo dawa za usingizi kwenye group linaloitwa BENZODIAZEPINE na BENZODIAZEPINE LIKE DRUGS.mfano ZOPICLONE/ZOLPIDEM,SOBRIL...ila hazitakiwi kutumiwa kwa muda mrefu zaidi ya wiki 2-4 kwasababu unakuwa addicted nazo yaani utakuwa huwezi kulala bila kula hizo dawa.
Jinsi ya kutatua tatizo la usingizi
1.Lala kila siku kwa wakati maalum mfano kila siku saa nne
2.Epuka kulala mchana
3.Epuka kunywa chai/kahawa usiku
4.Weka chumbani katika madhari nzuri kuwe na hewa safi ya kutosha
5.Epuka kutumia computer,ipad,simu kitandani/chumbani
6.Kabla kulala jaribu kuupumzisha mwili ili iwe tayari kiakili kwaajili ya kulala sio uanze kupiga deki robo saa kabla kulala
7.Epuka kulala na njaa au ukiwa na shibe
8.Jaribu kuepuka kufikiria sana ukiwa uko katika harakati ya kulala,andika dairy kama una vitu unahitaji kuvisuluhisha jaribu kuvisuluhisha siku ifuatayo.
9.Jaribu kufanya mazoezi/kuwa na activities ili kuuchosha mwili na ubongo
10.Chumba kitumike kwaajili ya kulala tu sio shughuli nyingine 🙂

thanx for ur advise
 
wana jamii forum naombeni mwenye dawa au ushauri kunusiana na tatizo la kukosa usingizi(usingizi wa mang'am mang'am)

.....Nenda SERAGIM iko mtaa wa Lindi nyuma ya jengo la ushirika ukitokea kariakoo .... kuna mazoezi yatakayoondoa tatizo lako ... ni bure....
 
"Akili nzuri hupatikana kwa siha nzuri". Usingizi ni moja katika jambo la ibada, na kila ibada ina muda wake maalum kwa vile usingizi ni ibada bila shaka una muda wake maalum wa kuitekeleza ibada hii. Wanasayansi wamependezesha kuwa mtu alale masaa 8. Pia ni uzuri kulala mwanzo wa usiku (yaani baada ya isha) na ukaamka nusu ya usiku na kufanya ibada.

Kutopata usingizi husababisha wazimu (sio kukesha siku moja kwa wale wenye tabia ya kukosa usingizi siku zote). Kukesha kunaweza kumkondesha mtu na hudhurika ubongo.


YENYE KULETA USINGIZI:

1. Miongoni mwa vinvyosababisha usingizi ni mafuta ya tango, hufaa sana kwa wale wenye usingizi mchache wajipake mafuta hayo.

2. Vilevile mafuta ya busanji yanasaidia kuleta usingizi, pia ukitia miguu katika maji ya dafidafi (warm water).

3. Pia kunusa manemane na kunywa maji yaliorowekwa manemane.

4. Kunusa zafarani na tufaha (apple) na pia maji ya zafarani ukayatia kichwani husaidia kuleta usingizi.

5. Kunya maziwa huleta usingizi

6. Asali safi ya nyuki kunywa kabla kulala kwa saa huleta usingizi.

7.
BIRINGANYA(EGGS PLANTS)-

-Tunda la biringanya ukilipika kama mboga linatibu vidonda tumbo na linasaidia kupata usingizi.Kwa wale wenye tatizo la kukosa usingizi

(INSOMNIA)wanashauriwa kula biringanya kwa wingi.


-Biringanya huharakisha kupona magonjwa na kuleta afya nzuri mwilini.Ikumbukwe kuwa usingizi ni kitu muhimu sana kwa afya ya mwili wa

binadamu na ustawi wake.@
radiation
 
Mimi ni muathirika mkubwa wa usingizi,na ninapokosa usingizi unakuwa ndo wakati wa kuwaza yote yanayofaa na yasiyofaa.hata hiyo egg plant nilishajaribu kwa kuipika na mayai kama chips according to dr. Ndodi ila hata haikunisaidia. Nitajaribu tena hizo ulizoandika hapo. Thank u..
 
11. ..Jaribu kula samaki kwenye mlo wa jioni...mie nkila sato/sangara huwa napata usingizi muruwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom