Tatizo la Kukosa Usingizi (Insomnia) na tiba yake

kutopata usingizi husababisha wazimu (sio kukesha siku moja kwa wale wenye tabia ya kukosa usingizi siku zote). Kukesha kunaweza kumkondesha mtu na hudhurika ubongo.

yenye kuleta usingizi:

1. Miongoni mwa vinavyosababisha usingizi ni mafuta ya tango, hufaa sana kwa wale wenye usingizi mchache wajipake mafuta hayo kichwani.

2. Vilevile mafuta ya busanji ujipake kichwani busanji kwa lugha ya kiingereza inaitwa ( violet) yanasaidia kuleta usingizi, pia ukitia nyayo zako katika maji ya uvuguvugu .

3. Pia kunusa manemane na kunywa maji yaliorowekwa manemane.

4. Kunusa zafarani na tufaha (apple) na pia maji ya zafarani ukayatia kichwani husaidia kuleta usingizi.

5. Kunywa maziwa yaliyochemshwa ukatia kidogo sukari huleta usingizi

6. Asali safi mbichi ya nyuki kunywa kabla kulala kwa saa huleta usingizi.

7. Tafuta dawa hii (
melatonin) - inatibu maradhi ya alzheimer's, kansa saratani, mfadhaiko, ukimwi, na kukosa usingizi

8.
hatua nyingine ni kulala kwa wakati uleule sikuzote.
oga nusu saa hivi kabla ya kulala.
usinywe chai au kahawa au soda kama pepsi au cocacola kabla ya kulala.
usifanye mazoezi karibu ya wakati wa kulala bora ufanye mapema.
kunywa maziwa ya fukuto kiasi.

Jaribu kutumia hizo dawa mkuu kisha unipe
feedback.@
mwitakesowani

asante sana ndugu...nitajaribu yote ndugu yangu. Hebu niambie busanji ni kitu gani na kinapatikana wapi hasa kwa urahisi. Pia manemane kwakweli kwangu ni misamiati hii.........nifahamishe ndugu nianze dozi mapema shukrani sana ndugu
 
kwani unalala masaa mangapi kwa siku?
Maana yawezekana anafikisha masaa 8 lakini anataka aendelee kulala na atazua gonjwa jingine.
Tuambie kwa siku unalala masaa mangapi. Tuanzie hapo then tukushauri

kiukweli hata sifahamu mana napoingia kitandani natafuta usingizi sipati kabisa nikipitiwa ni ndoto tu.... Yani sijifill kabisa mwili kulala mana zamani nikilala najijua kabisa yani kifupi silali mkuu hata sielewi y nimekuwa hivi full kuhangaika mapaka nahisi nimelogwa
 
asante sana ndugu...nitajaribu yote ndugu yangu. Hebu niambie busanji ni kitu gani na kinapatikana wapi hasa kwa urahisi. Pia manemane kwakweli kwangu ni misamiati hii.........nifahamishe ndugu nianze dozi mapema shukrani sana ndugu
Mkuu.@mwitakesowani dawa hizo zinapatikana Kama upo Dar nenda Sokoni kariakoo mtaa wa pemba kwa wauza Dawa za kiarabu wapemba au kama unaye jirani yoyote muarabu muulize atakufahamisha wapi waweza kupata. Basi mkuu unahindwa hata kusema (like) Ukipata nipe feedback.
 
UKOSEFU WA USINGIZI NI HATARI KWA AFYA YAKO

KITENDO cha kukosa usingizi mara kwa mara wakati wa kulala kuna weza kuonekana ni jambo ambalo halina madhara kiafya, lakini ukweli ni kwamba unapokosa usingizi, hasa kwa muda mrefu, kuna athari kubwa katika afya yako yote, hata kama unakula na kufanya mazoezi vizuri.

Madhara ya ukosefu usingizi huathiri mfumo mzima wa mwili, mathalan, mbali ya kuathiri kinga ya mwili na kuongeza hatari ya kupatwa na magonjwa ya saratani, ukosefu wa usingizi huweza kusababisha madhara mengine yafutayo:

HATARI YA KUPATWA NA UGONJWA WA MOYO
Unapokosa usingizi, mfumo wa uzalishaji homoni huvurugika ambapo uzalishaji wa homoni za

‘stresi’ (stress hormones) huongezeka. Pia husababisha vidonda vya tumbo na hali ya kusikia njaa hata kama umetoka kula muda mfupi. Uko hatarini kusumbumbuliwa na hasira na ghadhabu kila mara.

ONGEZEKO LA SHINIKIZO LA DAMU

Ukosefu wa usingizi huchangia pia ongezeko la shinikizo la damu, pia huchangia kuzeeka kwa mtu kutokana na kuvurugika kwa uzalishaji wa homoni za ongezeko la umri. Humfanya mtu kuonekana mzee ili hali bado ana umri mdogo.

KUZIDISHA TATIZO LA UKOSEFU WA CHOO

Ukosefu wa usingizi huchangia pia tatizo la ukosefu wa choo na huweza hata kusababisha kifo kama tatizo likiwa sugu.

EPUKA KUTUMIA DAWA ZA USINGIZI

Kama unasumbuliwa na tatizo la ukosefu wa usingizi, jua kwamba hauko peke yako. Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani na Taasisi ya Taifa ya Usingizi (National Sleep Foundation –NSF), umegundua kuwa kati ya watu 10, ni wanne tu hupata usingizi mzuri kila wiki.
Pamoja na kuonekana kwa athari nyingi za kukosekana kwa usingizi, lakini utakuwa unajiweka katika madhara na hatari zaidi iwapo utalazimisha kupata usingizi kwa kumeza dawa za usingizi, kwa sababu ni hatari na mara nyingi dawa hizo huwa hazisaidii kuondoa tatizo.

JINSI YA KUFANYA ILI UPATE USINGIZI

Kwa asili yake, kichocheo cha usingizi mwilini kijulikanacho kama ‘melatonin’ hupatikana kwa ulaji wa mboga za majani na matunda mbalimbali ya kuongeza virutubisho mwilini na hupatikana pia kwa kupata mwanga wa jua wa kutosha wakati wa mchana. Hivyo huna haja ya kumeza vidonge badala yake zingatia uzalishaji wa kirutubisho hicho kwa mlo na mwanga wa jua.
Ili kujiwekea mazingira mazuri ya kupata usingizi mzuri, unashauriwa kuepuka kufanya yafuatayo muda mfupi kabla ya kupanda kitandani kulala:

Epuka kuangalia TV au kompyuta muda mfupi au saa moja kabla ya kulala, kwani teknolojia hizi siyo nzuri sana kwa macho kutokana na mwanga wake, hasa kwa mtu mwenye matatizo ya kupata usingizi.

Epuka kulala huku taa inawaka, hakikisha unalala huku taa zote zikiwa zimezimwa, licha ya mwanga wa taa usiku kusababisha madhara mengine, lakini huchangia kuharibu mtiririko wa usingizi. Hata uamkapo usiku kwenda msalani, ikiwezekana usiwashe taa ili kuepuka kuvuruga usingizi wako.

Usilale karibu na vifaa vya umeme na vyenye sumaku kama vile saa, simu, au redio kwani huchangia kudhoofisha uzalishaji wa homoni za usingizi. Hata saa yako yenye ‘alarm’ ya kukuamsha, unashauriwa kuiweka mbali nawe kabisa.

Mwisho, hakikisha unakuwa na ratiba ya kulala inayoeleweka na hakikisha unalala muda huohuo kila siku. Kwa kawaida mtu anatakiwa kulala kati ya saa tatu na saa nne usiku. Iwapo utazingatia vyote vilivyoelezwa hapo juu, bila shaka utaweza sasa kulala usingizi mnono.IRENE MWAMFUPE JAMII: Saikolojia

Same yo me, na baadhi ya symptoms ulizozitaja i got them comrade, so dawa ni nini?
 
Kutopata usingizi husababisha wazimu (sio kukesha siku moja kwa wale wenye tabia ya kukosa usingizi siku zote). Kukesha kunaweza kumkondesha mtu na hudhurika ubongo.

YENYE KULETA USINGIZI:

1. Miongoni mwa vinavyosababisha usingizi ni mafuta ya tango, hufaa sana kwa wale wenye usingizi mchache wajipake mafuta hayo kichwani.

2. Vilevile mafuta ya busanji yanasaidia kuleta usingizi, Pia ukitia nyayo za miguu katika maji ya Uvuguvugu .

3. Pia kunusamanemane na kunywa maji yaliorowekwa manemane.

4. Kunusa zafarani na tufaha (apple) na pia maji ya zafarani ukayatia kichwani husaidia kuleta usingizi.

5. Kunya maziwa yaliyochemshwa ukatia kidogo sukari huleta usingizi

6 Kunywa mtindi utiye ndani yake sukari
7 Asali safi ya nyuki kunywa kabla kulala kwa saa huleta usingizi.@
kijanamakini
 
Au Tumia dawa hii itakusaidia. Dawa ya kutibu Ukosefu wa usingizi:
Chukua kijiko kimoja cha habbat-Sauda, changanya na glasi ya maziwa moto yaliyochanganywa na kijiko kimoja kikubwa cha Asali, kunywa yakiwa yamepoa kiasi utapata usingizi mnono.
 
Ndugu MziziMkavu nikosapo usingizi kitandani, huwa nachukua simu au laptop na kuanza kuchat ndipo napata usingizi.
Na jambo hlo huwa nalifanya huu ni mwaka wa 2 sasa.
Na huwa nalala kbs,
na nisipochezea basi naweza kesha hadi asubuhi pasi na kulala.
Je,kuna madhara ninayoweza kuyapata hapo baadae?
 
Last edited by a moderator:

kama hupati usingizi unaweza kupata madhara, la kama unapata usingiz kwa kutumia laptop na simu huwezi kupata madhara ila unapotumia laptop hakikisha unawasha taa ndipo waweza kutumia laptop usitumie Laptop usiku wakati upo chumbani giza utapata madhara ya macho kutoona vizuri haswa herufi ndogo baada ya miaka 2 ukitumia hiyo Laptop kwenye sehemu ya giza macho yako yataharibika hutoweza kuona herufi ndogo mpaka uvae miwani Madame B
 
Shukrani mkuu,
nimekuelewa manake tatizo la kukosa usingizi huwa linanisumbua sana.
 
Mkuu.@mwitakesowani dawa hizo zinapatikana Kama upo Dar nenda Sokoni kariakoo mtaa wa pemba kwa wauza Dawa za kiarabu wapemba au kama unaye jirani yoyote muarabu muulize atakufahamisha wapi waweza kupata. Basi mkuu unahindwa hata kusema (like) Ukipata nipe feedback.

kaka asante nitazifatilia na pia nitakupa feedback nipo morogoro kwasasa afu mi mgeni kidogo ndani ya jamii forum kuweka likes hata cjui nafanyeje ntajifunza taratibu mpaka nizoee, asante na ubarikiwe ndugu kwa ushauri na msaada wako
 
Wan JF nawaomba msaada, nina natizo la kukosa usingizi(usiku) , nikiamua kulala basi hupata takriban dk kumi ama nusu saa tu, nikiisha shtuka basi ndo silali tena hadi mapambazuko. nawaomba mnisaidie ninini tatizo labda na ufumbuzi wake pia.
 
pole sana nina ze same problem heli yako unahisi unalala mimi chisi kulala kuna wengi wamenipa ushauri naendelea kuufatilia MUNGU c athumani atajaalia tutapona kula bilinganya every day
 
Una umri gani na unafanya shughuli gani nieleze kama ni mfanyakazi au mfanya biashara au mkulima au mwanafunzi etc.nijue jinsi ya kukusaidia.
 
Wahenga watakuwa wanaanza kukurisisha uwanga wewe!
Nenda kafanyiwe maombi...
 
UKOSEFU WA USINGIZI NI HATARI KWA AFYA YAKO

sleep0410.jpg

KITENDO cha kukosa usingizi mara kwa mara wakati wa kulala kuna weza kuonekana ni jambo ambalo halina madhara kiafya, lakini ukweli ni kwamba unapokosa usingizi, hasa kwa muda mrefu, kuna athari kubwa katika afya yako yote, hata kama unakula na kufanya mazoezi vizuri.

Madhara ya ukosefu usingizi huathiri mfumo mzima wa mwili, mathalan, mbali ya kuathiri kinga ya mwili na kuongeza hatari ya kupatwa na magonjwa ya saratani, ukosefu wa usingizi huweza kusababisha madhara mengine yafutayo:

HATARI YA KUPATWA NA UGONJWA WA MOYO
Unapokosa usingizi, mfumo wa uzalishaji homoni huvurugika ambapo uzalishaji wa homoni za ‘stresi’ (stress hormones) huongezeka. Pia husababisha vidonda vya tumbo na hali ya kusikia njaa hata kama umetoka kula muda mfupi. Uko hatarini kusumbumbuliwa na hasira na ghadhabu kila mara.

ONGEZEKO LA SHINIKIZO LA DAMU

Ukosefu wa usingizi huchangia pia ongezeko la shinikizo la damu, pia huchangia kuzeeka kwa mtu kutokana na kuvurugika kwa uzalishaji wa homoni za ongezeko la umri. Humfanya mtu kuonekana mzee ili hali bado ana umri mdogo.

KUZIDISHA TATIZO LA UKOSEFU WA CHOO
Ukosefu wa usingizi huchangia pia tatizo la ukosefu wa choo na huweza hata kusababisha kifo kama tatizo likiwa sugu.

EPUKA KUTUMIA DAWA ZA USINGIZI

Kama unasumbuliwa na tatizo la ukosefu wa usingizi, jua kwamba hauko peke yako. Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani na Taasisi ya Taifa ya Usingizi (National Sleep Foundation –NSF), umegundua kuwa kati ya watu 10, ni wanne tu hupata usingizi mzuri kila wiki.
Pamoja na kuonekana kwa athari nyingi za kukosekana kwa usingizi, lakini utakuwa unajiweka katika madhara na hatari zaidi iwapo utalazimisha kupata usingizi kwa kumeza dawa za usingizi, kwa sababu ni hatari na mara nyingi dawa hizo huwa hazisaidii kuondoa tatizo.

JINSI YA KUFANYA ILI UPATE USINGIZI

Kwa asili yake, kichocheo cha usingizi mwilini kijulikanacho kama ‘melatonin’ hupatikana kwa ulaji wa mboga za majani na matunda mbalimbali ya kuongeza virutubisho mwilini na hupatikana pia kwa kupata mwanga wa jua wa kutosha wakati wa mchana. Hivyo huna haja ya kumeza vidonge badala yake zingatia uzalishaji wa kirutubisho hicho kwa mlo na mwanga wa jua.
Ili kujiwekea mazingira mazuri ya kupata usingizi mzuri, unashauriwa kuepuka kufanya yafuatayo muda mfupi kabla ya kupanda kitandani kulala:

Epuka kuangalia TV au kompyuta muda mfupi au saa moja kabla ya kulala, kwani teknolojia hizi siyo nzuri sana kwa macho kutokana na mwanga wake, hasa kwa mtu mwenye matatizo ya kupata usingizi.
Epuka kulala huku taa inawaka, hakikisha unalala huku taa zote zikiwa zimezimwa, licha ya mwanga wa taa usiku kusababisha madhara mengine, lakini huchangia kuharibu mtiririko wa usingizi. Hata uamkapo usiku kwenda msalani, ikiwezekana usiwashe taa ili kuepuka kuvuruga usingizi wako.
Usilale karibu na vifaa vya umeme na vyenye sumaku kama vile saa, simu, au redio kwani huchangia kudhoofisha uzalishaji wa homoni za usingizi. Hata saa yako yenye ‘alarm’ ya kukuamsha, unashauriwa kuiweka mbali nawe kabisa.

Mwisho, hakikisha unakuwa na ratiba ya kulala inayoeleweka na hakikisha unalala muda huohuo kila siku. Kwa kawaida mtu anatakiwa kulala kati ya saa tatu na saa nne usiku. Iwapo utazingatia vyote vilivyoelezwa hapo juu, bila shaka utaweza sasa kulala usingizi mnono.
 
Kutopata usingizi husababisha wazimu (sio kukesha siku moja kwa wale wenye tabia ya kukosa usingizi siku zote). Kukesha kunaweza kumkondesha mtu na hudhurika ubongo.

YENYE KULETA USINGIZI:

1. Miongoni mwa vinavyosababisha usingizi ni mafuta ya tango, hufaa sana kwa wale wenye usingizi mchache wajipake mafuta hayo.

2. Vilevile mafuta ya busanji yanasaidia kuleta usingizi, pia ukitia miguu katika maji ya Uvuguvugu .

3. Pia kunusa manemane na kunywa maji yaliorowekwa manemane.

4. Kunusa zafarani na tufaha (apple) na pia maji ya zafarani ukayatia kichwani husaidia kuleta usingizi.

5. Kunya maziwa yaliyochemshwa ukatia kidogo sukari huleta usingizi

6. Asali safi ya nyuki kunywa kabla kulala kwa saa huleta usingizi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom