kuna rafiki yangu anafanya kazi tanesco wakati tunapata kilaji nilimuuliza sababu za kukata umeme wakati mwingine zaidi ya masaa 36 wakati ijumaa ya wiki iliyopita mlitamba kuwa mmewasha mitambo mingi na sasa hakutakuwa na kukatikakatika kwa umeme tena lakini hali ndo imekuwa mbaya kuliko, si afadhari watujulishe kama kuna mgao tujipange .majibu yake yalikuwa kama ifuatavyo:-
" mgao wa umeme hakuna ila tumechoka kabisa na serikali ya ccm kwani shirika letu ndilo limekuwa kichwa cha mwendawazimu . We jaribu kuona kashifa zote kubwakubwa utazikuta tanesco, kuanzia iptl, richmond, escrow n.k., pia kuna kashfa ndogondoga zinazohusu ununuzi wa mafuta mazito , nguzo, ununuzi wa misumari badala ya spea n.k. Tuna muda sasa hatujaongezwa mishahara ukilinganisha na baadhi ya wakala wa serikali tukiomba nyongeza tunaambiwa shirika linajiendesha kwa hasara, tumeona adui yetu ni ccm hivyo tunakata makusudi hasa kipindi hiki cha kampein ili kuwachonganisha ccm na wapiga kura ili wasiichague oktoba 25" . Je hii inaweza kuwa kweli au kuna tatizo jingine la kiufundi.