Tatizo la kuchangisha walimu mchango wa mwenge

kasahunga

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
215
33
Hili suala la kuchangisha walimu mchango wa mwenge limekuwa endelevu Kwa sababu Kila mwaka walimu wanakuwa wakichangia Kwa kulazimisha.
Mbaya zaidi Kila mwaka fedha inakuwa ikiongezeka mfanonkutoka sh. 2000 kwenda sh. 5000. Hapa walimu wanatakiwa kujua nini Kilichosababisha ongezeko hilo.
Hii siyo sawa Kwa walimu kuchangishwa fedha.
 
siyo walimu tu.. ni wafanyakazi wa halmashauri, walio chini ya Mkurugenzi wakiwepo wauguzi , madaktari mpaka madereva.

Sasa ukilalamika sana mwalimu itaonekana walimu walalamishi, na itaonekana unataka hiyo michango iondolewe kwa walimu tu..
hoja ya ku discuss hapa
1 . Nini umuhimu wa mwenge kwa kizazi cha leo.?

2. je ni kweli mwenge ni zindiko la nchi, kana kwamba hata CHAUMA wakiingia madarakani hawawezi kuugusa .. si umeona Jiwe, shujaaa. aliona bora afute hata ajira za ualimu lakini hajawahi gusa gharama za mwenge.
soma kuhusu F.Ganze Masta mchawi wa Taifa.

3. vipi kama kuna CAG, kuna viongozi , kwa nini hasa mwenge uzindue miradi?

Mi naona mwenge ni kama sherehe flani za kitaifa, ni kama Carnival festival za kule Brazil, ama ma dragon ya kule china. sema wabongo wengi tuna potezea...

NYONGEZA. NJE YA MADA KIDOGO.
Njiani porini huko ni kweli mwenge huwa una zimwa ku save wese?

baada ya kukimbiza mwenge hawa wakimbizaji huwa "wanapotea"?
 
Hili suala la kuchangisha walimu mchango wa mwenge limekuwa endelevu Kwa sababu Kila mwaka walimu wanakuwa wakichangia Kwa kulazimisha.
Mbaya zaidi Kila mwaka fedha inakuwa ikiongezeka mfanonkutoka sh. 2000 kwenda sh. 5000. Hapa walimu wanatakiwa kujua nini Kilichosababisha ongezeko hilo.
Hii siyo sawa Kwa walimu kuchangishwa fedha.

Walimu mtaendelea kunyanyasika mpaka mtakapokuwa na akili
 
Ulozi wa ccm kutoleta maendeleo. Mwenge wa uhuru ni mambo ya kufikirika ya kutazamani sababu

Watu wengi zamani walikua wanaishi sehemu zisizofikika kwa urahisi. So jukumu la mwenge lilikua kukumbusha serikali ipo, walau ata mara moja kwa mwaka wakiona.
 
Hivi walimu huwa wanatumia ubongo wao kujiuliza kwa nini wao ni kundi la wanyonge?
Hivi wanajiuliza kuwa watawala wanao wanyanyasa ni CCM na kuwa nafasi ya kuwaondoa huwa ipo ila wao huwa ndio kikwazo?
Nadhani hiyo kazi ni ya WASIO JITAMBUA SIKU HIZI
 
Swala la mwenge ni la kitaifa kila ofc huwa zinakuja barua za kuchagua mwenge unapokuwa kwenye wilaya husika.
Ni tamaduni nadhani.
 
siyo walimu tu.. ni wafanyakazi wa halmashauri
Hata baadhi ya wafanyabiashara pia wanachangishwa. Kimsingi hiyo michango imekaa kifisadi. Kila mwaka huo mwenge umekuwa ukitengewa bajeti ya kuukimbiza.

Na kama unakosa fedha za kuukimbizia kiasi cha kuwasumbua wafanyakazi na wafanyabiashara, basi ifikie wakati uwekwe tu kwenye jumba la makumbusho. Maana tija yake kwa wananchi wa dunia ya sasa, kwa mtazamo wangu naona ni ndogo sana.
 
Hili suala la kuchangisha walimu mchango wa mwenge limekuwa endelevu Kwa sababu Kila mwaka walimu wanakuwa wakichangia Kwa kulazimisha.
Mbaya zaidi Kila mwaka fedha inakuwa ikiongezeka mfanonkutoka sh. 2000 kwenda sh. 5000. Hapa walimu wanatakiwa kujua nini Kilichosababisha ongezeko hilo.
Hii siyo sawa Kwa walimu kuchangishwa fedha.
Mpwayungu village njoo huku,sasa naanza kumuelewa jamaa kwamba walimu hawajitambui wanahitaji kukombolewa
 
Hivi hizo pesa wanazochukuwa kwa Walimu huwa CAG hazioni mbona sjawahi kuskia hesabu zake.

NB
Ukiona jambo limeibuliwa na Wananchi lakini mamlaka husika haijalitolea ufafanuzi wowote au kukemea ujue nyuma yake ipo mamlaka isiyokemea/kutoa ufafanuzi.
 
Mkiambiwa muiunge mkono CHADEMA kuhusu katiba mpya na kukubali kushiriki kuleta mabadiliko mnasema haliwahusu.

Ipo hivi, kuwa serikali yoyote sikivu ya kidemokrasia ina mkataba na wananchi kuwa kupitia sheria rasmi walipe kodi ili iwapatie huduma

Sasa hiyo michango ya kuchangia mwenge, shule ya lazima ni aina ya kodi mpya ya shurti ambayo haipo kisheria na CHADEMA inasisitiza kodi na tozo lazima ziwe zile rasmi kisheria na CHADEMA inakwenda mbali kuwa makusanyo ya kodi halali zitumike vizuri siyo kwa kununua magari ya kifahari kwa watawala wala kutumika kukimbiza mwenge n.k

Tawala dhaifu Afrika au nchi zisizofuata utawala bora Colombia, Guatemala, DR Congo n.k ndiyo utakuta magenge ya kiuhalifu huwa na kodi hizi zisizo rasmi, maana nchi zinazotumia kodi zake vizuri za kaskazini mwa dunia raia hawawezi kushurutishwa kulipa kodi za aina ya mwenge. Nchi hizo za Ulaya na Marekani ya kaskazini Kodi zote zipo wazi kisheria na serikali zao hujitahidi kuwahudumia walipa kodi wake vizuri.

Kazi kwenu waalimu mfanye uamuzi kunyoa au kusuka katika kupigania katiba mpya ili haki, uhuru, demokrasia na Maendeleo ya Watu ya kweli yawafikie walipa kodi na raia wote waTanzania.
 
Huo mchango wa mwenge ni haramu na wizi mkubwa.
Ili uelewe nia mbaya ya mwenge jiulize maswali haya:
1. Ukilipa huo mchango unapewa stakabadhi?
Kama hupewi maana yake zile pesa zinaenda kutumia hovyo hovyo.
Mfano kununulia pombe, nyama na kuhonga wanawake.
2. Bajeti ya mwenge haitoshi?
Kama haitoshi tujue ili ifanyike namna bora ya kutatua tatizo hili na SI kuchangisha.
wafanyakazi, tena kwa vitisho.
3. Kwa nini baadhi ya halmashauri hazichangishi mchango huu?
Mfano halmashauri ya jiji la Mbeya sijjawahi kuona huu wizi.
Maana yake kuna halmashauri hazijiandai kuupokea mwenge, na badala yake
zinawasukumia mzigo huu wafanyakazi ambao wengi ni maskini.
MAOMBI YANGU:
Mheshimiwa rais hili suala liangalie maana limekuwa kero kwa muda mrefu.

NB: Kuwa mzalendo hakukufanyi uwe mjinga. Tuchangie michango halali. Na tukatae michango haramu.
 
Hili suala la kuchangisha walimu mchango wa mwenge limekuwa endelevu Kwa sababu Kila mwaka walimu wanakuwa wakichangia Kwa kulazimisha.
Mbaya zaidi Kila mwaka fedha inakuwa ikiongezeka mfanonkutoka sh. 2000 kwenda sh. 5000. Hapa walimu wanatakiwa kujua nini Kilichosababisha ongezeko hilo.
Hii siyo sawa Kwa walimu kuchangishwa fedha.
Kwani ni walimu tu? HALMASHAURI zote chini ya Hawa wakurugenzi wanachangia mwenge, kuanzia wakuu wa Idara hadi watumishi wa ngazi za kawaida.
 
Hili suala la kuchangisha walimu mchango wa mwenge limekuwa endelevu Kwa sababu Kila mwaka walimu wanakuwa wakichangia Kwa kulazimisha.
Mbaya zaidi Kila mwaka fedha inakuwa ikiongezeka mfanonkutoka sh. 2000 kwenda sh. 5000. Hapa walimu wanatakiwa kujua nini Kilichosababisha ongezeko hilo.
Hii siyo sawa Kwa walimu kuchangishwa fedha.
Hapa Tanganyika watumishi wote walio chini ya mkurugenzi tunamchangia mwenge,siyo walimu tu
 
Changieni nyie ndio wanufaika wa sensa na usimamizi wa uchaguzi ndani ya Tanzakiza
JamiiForums-1814590334.jpg
 
Back
Top Bottom